15-Imaam Ibn Baaz: I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?
Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
15. Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
a. Kauli ya sahihi kabisa ya Ahlul-‘Ilm ni kwamba haina wakati maalumu.
b. Na Sunnah ni mtu aingie akiwa Mu’takif pindi anapotia niyyah kwa ajili ya I’tikaaf na atoke baada ya kumaliza muda wake alionuiya.
c. Na anaweza kuikata ikiwa atahitaji kufanya hivyo kwa sababu I’tikaaf ni Sunnah haipasi kujiwajibisha nayo ikiwa ni mwenye udhuru.
d. Na I’tikaaf inapendekezeka katika makumi ya mwisho ya Ramadhwaan na ni mustahabu kwa mwenye kuingia I’tikaaf aingie akiwe Mu’takif baada ya Swalaah ya Alfajiri kuanzia siku ya ishirini na moja, kama alivyofanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atoke inapomalizika masiku kumi (ya mwisho).
[Majmu’w Al-Fataawaa (15/442)]