20-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?
Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
20. Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Yanayopendekeza kwake ni mtu kujishughulisha na utiifu kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kusoma Qur-aan, na dhikru-Allaah, na Swalaah na kadhaalika, na wala asipoteze muda wake katika yasiyokuwa na faida humo.’
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/175)]