21-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?

 

 

Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

21. Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ama kutoka kwake kutoka Masjid, ‘Ulamaa wameigawa katika sehemu tatu:

 

  1. Inafaa: nayo ni kutoka kwa jambo lisokuwa na budi kutendwa linalokubalika ki-shariy’ah mfano kutoka kuswali jamaa’ah au jambo la kimaumbile kama kukidhi haja kama vile kwenda msalani kukojoa na chooni.

 

  1. Kutoka kwa ajili ya utiifu isiyomwajibika kama kumtembelea mgonjwa, au kuhudhuria janaazah basi hiyo ikiwa alijiwekea sharti mwanzo wa I’tikaaf yake, basi haina ubaya. Lakini ikiwa hakujiwekea sharti  basi haipasi.

 

  1. Kutoka katika jambo linalopinga hukmu ya I’tikaaf kama vile kufanya biashara, na kujamiiana na ahli yake na kadhaalika. Haya hayajuzu ikiwa kwa kuweka sharti au kutokuwekea sharti (I’tikaaf yake).

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/157)]

 

Share