22-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?
Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
22. Je Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?
Imaam Ibn ‘Uthaymin (Rahimahu Allaah) amesema:
- Inajuzu kwa Mu’takif aende nyumbani kwake kwa ajili ya kula chakula ikiwa hakupata mwenye kumtayarishia chakula (au kumletea hapo Msikitini). Lakini ikiwa amepata wa kumtayarishia chakula Msikitini, basi asitoke kwa sababu Mu’takif hatoki isipokuwa kwa jambo ambalo hana budi nalo.
- Ama kuoga, ikiwa ni kutokana na janaba, basi inamuwajibika atoke, kwa sababu hakuna budi kuwa afanye ghuslu (ajitwaharishe). Lakini ikiwa si kutokana na janaba bali ni kwa ajili ya kujimwagia kujiburudisha kwa kuoga maji baridi, basi asitoke kwa sababu hili ni jambo amejiwajibisha mwenyewe. Lakini ikiwa kwa ajili ya kuondosha harufu inayomtia shaka kubakia kwake basi anaweza kutoka.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]