25-Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah
Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
25. Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
- Ikiwa I’tikaaf yake ameiwekea nadhiri kwa wakati maalumu basi inamlazimika kuikamilisha, kwa sababu kutimiza nadhiri ni katika utiifu na jambo la kulazimika.
- Na ikiwa ni ya kujitolea tu basi akitaka ataikamilisha na akitaka ataikata aende ‘Umrah.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/446)]