26-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Mu’takif Katika Al-Haram Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?
Mu’takif Anayekuwa Katika Al-Haram Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
26. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Anayekuwa Katika Al-Haram (Makkah) Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Kupanda sakafu za juu ya Msikiti hiyo haidhuru kwani kutoka katika mlango wa Msikiti wa chini kupanda juu kwenye sakafu si chochote bali ni hatua chache, na pia anakusudia kurudi (chini) Msikitini pia. Basi hakuna ubaya katika hili.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/181)]