27-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?
Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
27. Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
- Ikiwa mtu ana majukmu ya ahli zake na ikiwa amewajibika nayo, basi ni waajib kwake kuyatimiza na hivyo basi, kutekeleza I’tikaaf huwa ni dhambi kwake.
- Na ikiwa si yenye kuwajibika kwake, basi hata hivyo kuyatimiza huwa ni bora kwake kuliko I’tikaaf.
- Ama mtu aliyekuwa huru, basi I’tikaaf inakuwa ni haki kwake ki-shariy’ah. Lakini ikiwa ana majukumu katika makumi ya mwanzo, lakini kisha akawa huru kisha akataka kutekeleza I’tikaaf masiku yaliyobakia basi hakuna neno.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]