07-Imaam Ibn Baaz Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Mwenye Deni La Ramadhwaan Atapata Thawabu Za Sitta Shawaal Kabla Kufunga Deni Lake?
Je, Mwenye Deni La Ramadhwaan Atapata Thawabu Akifunga Sitta Shawwaal Kabla Kulipa Deni Lake?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ni waajib kukimbilia kulipa deni hata kama Sitta Shawwaal zitampita kutokana na Hadiyth iliyotajwa na kwa sababu fardhi inatangulizwa kabla ya naafil (Sunnah)."
[Al-Fataawaa (15/393)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Hawezi mtu kupata thawabu za Swiyaam za Sitta Shawwaal isipokuwa ikiwa amemaliza Swiyaam za mwezi wa Ramadhwaan.
[Al-Fataawaa (18/20)]