03-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Sifa Ya Swalaah Ya ‘Iyd
Sifa Ya Swalaah Ya ‘Iyd
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
i-Inaletwa Takbiyrah Al-Ihraam na inafunguliwa kwa du’aa kisha zinaletwa Takbiyrah sita (jumla zitakuwa saba) kisha inasomwa Al-Faatihah na Suwrah ima (Sabbihisma) au (Qaaf) katika Raka’ah ya kwanza.
ii-Katika Raka’ah ya pili, atakaposimama kutoka katika kusujudu, atainuka huku akileta Takbiyrah kisha ataleta Takbiyrah tano baada ya kusimama kwake. Kisha atasoma Al-Faatihah na Suwrah. Ikiwa atasoma katika Rakaa ya kwanza (Sabbihismaa) basi asome katika Rakaa ya pili (Al-Ghaashiyah). Na pindi akiwa amesoma katika Rakaa ya kwanza (Qaaf), basi asome katika Rakaa ya pili (Iqtarabatis-Saa’ah .. Suwrah Al-Qamar)
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/223)]
