06-Imaam Ibn 'Uthaymiyn Na Al-Lajnah Ad-Daaimah: Nini Kinasemwa Baina Ya Kila Takbiyrah Na Takbiyrah Katika Swalaah Za ‘Iyd Mbili?
Nini Kinasemwa Baina Ya Kila Takbiyrah Na Takbiyrah Katika Swalaah Za ‘Iyd Mbili?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) Na Al-Lajnah Ad-Daaimah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hakuna dhikr (utajo) maalumu bali ni kumhimidi Allaah na kumtukuza na kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aina yoyote apendayo na ikiwa ataacha kufanya hivyo basi hakuna ubaya kwani hiyo ni mustahab."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/241)]
Al-Lajnah Ad-Daimah wamesema:
Inapaswa amhimidi Allaah (AlhamduliLLaah) na amsabbih (Subhaana Allaah) na Amkabbir (Allaahu Akbar) na amswalie Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baina ya kila Takbiyrah mbili.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/302)]