08-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Nini Hukmu Ikiwa Imaam Amenitangulia Nikakosa Takbiyrah Za Ziada?
Nini Hukmu Ikiwa Imaam Amenitangulia Nikakosa Takbiyrah Za Ziada?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ikiwa ameingia pamoja na Imaam akiwa katika Takbiyrah basi akabbir (Allaahu Akbar) kwanza, kisha amfuate Imaam katika yaliyobakia na itamuondokea kwake yaliyompita yatakuwa hayampasi tena."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/245)]