09-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ikiwa Mtu Itampita Kitu Katika Takbiyrah Za ‘Iyd
Ikiwa Mtu Itampita Kitu Katika Takbiyrah Za ‘Iyd
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Yatamuondokea (hayatompasa) yale yaliyompita, na hivyo hivyo kama vile akisahau au mpaka akafikia kusoma (Suwrah) basi haleti tena (harudii tena), kwa sababu Sunnah imepita mahali pake Lakini ikiwa imempita pamoja na Imaam Rakaa kamili basi inabidi alete Takbiyrah za Rakaa hiyo iliyompita.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/241)]