Sayyidul Istighfaar Du’aa Bora Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Na Fadhila Za Kuomba Tawbah
Sayyidul Istighfaar Du’aa Bora Kabisa Ya Kuomba Maghfirah
Na Fadhila Za Kuomba Tawbah
Alhidaaya.com
Du’aa hii imeitwa Sayyidul-Istighfaar (Du’aa bora au adhimu kabisa ya kuomba maghfirah kuliko istighfaar nyenginezo) kwa sababu imekusanya kukiri Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (‘ibaadah), Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Uola), kukiri dhambi za mja, kunyenyekea mja kwa Rabb wake, kutambua neemah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amghufurie madhambi yote.
اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .
Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘abduka wa anaa ‘alaa ‘ah-dika wawa’-dika mastatwa’-tu, a’uwdhu bika min sharri maa swana’-tu, abuw-u Laka bini’-matika ‘alayya wa abuw-u bidhanbiy, faghfir-liy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta
Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna wa kughufuria madhambi ila Wewe.
Hadiyth ya Shaddaad bin ‘Aws (Radhwiya Allaahu ’anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam amesema:
((مَنْ قَالَهَا مِنْ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، َنْ قَالَهَا مِنْ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ))
"Atakayesema mchana akiwa na yakini nayo, akafariki siku hiyo kabla kuingia jioni basi atakuwa mtu wa Jannah, na atakayesema usiku naye akiwa yakini nayo akafariki kabla hajafika asubuhi basi yeye ni mtu wa Jannah". [Al-Bukhaariy (7/150) [2306]- Sayyid Al-Istighfaar]
Na Anasema pia ('Azza wa Jalla) Anasema:
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾
Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua. [Aal-‘Imraan: 135]
Na kisa cha kusisimua kuhusu kuomba tawbah katika Hdiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
عن أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الَلَّهُ أَشَدُّ فَرَحًا بِتَوْبَةِ عَبْدِهِ حِينَ يَتُوبُ إِلَيْهِ مِنْ أَحَدِكُمْ كَانَ عَلَى رَاحِلَتِهِ بِأَرْضِ فَلاَةٍ فَانْفَلَتَتْ مِنْهُ وَعَلَيْهَا طَعَامُهُ وَشَرَابُهُ فَأَيِسَ مِنْهَا فَأَتَى شَجَرَةً فَاضْطَجَعَ فِي ظِلِّهَا قَدْ أَيِسَ مِنْ رَاحِلَتِهِ فَبَيْنَا هُوَ كَذَلِكَ إِذَا هُوَ بِهَا قَائِمَةً عِنْدَهُ فَأَخَذَ بِخِطَامِهَا ثُمَّ قَالَ مِنْ شِدَّةِ الْفَرَحِ: "اللَّهُمَّ أَنْتَ عَبْدِي وَأَنَا رَبُّكَ" أَخْطَأَ مِنْ شِدَّةِ الْفَرَحِ مسلم
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Allaah Hufurahikiwa mno na tawbah ya mja Wake wakati anapotubia Kwake kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa amempanda mnyama wake kwenye jangwa (la joto kali hakuna mtu), kisha mnyama huyo aliyebeba chakula chake na maji yake akampotea, na akakata tamaa kabisa ya kumpata tena. Akaenda kwenye mti, akalala chali ya kivuli chake huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpata tena mnyama wake. Akiwa katika hali hiyo (ya kutojua nini la kufanya), mara anashtuka kumwona huyo amesimama mbele yake, akaikamata hatamu yake, na kwa ile furaha akasema: "Ee Allaah, Wewe ni mja wangu na mimi ni Rabb wako.” Alikosea (kumshukuru Rabb wake) kwa wingi wa furaha aliyokuwa nayo.” [Muslim]
1-Allaah (‘Azza wa Jalla) Anawapenda Waja Wake Wanaomuomba Tawbah:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾
Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha. [Al-Baqarah: 222]
2-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Nyakati Za Usiku Hakuna Shaka Kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anapokea Tawbah:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم
Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia (mbingu ya kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani Ana shida Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
3-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kunasababisha Kujaaliwa Starehe Na Maisha Mazuri:
Ameamrishwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) awaambie watu wake:
وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ﴿٣﴾
Na kwamba: “Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake, Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliokadiriwa; na Atampa kila mwenye fadhila, fadhila Zake. Na mkikengeuka, basi hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa.” [Huwd: 3]
4-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kunasabisha Kuletewa neema ya mvua na kuzidishiwa nguvu:
Nabiy Huwd ('Alayhis-Salaam) aliwaambia watu wake:
وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْامُجْرِمِينَ﴿٥٢﴾
“Na enyi kaumu yangu! Mwombeni maghfirah Rabb wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu, na wala msikengeuke mkawa wahalifu.” [Huwd: 52]
5-Kuomba Maghfirah Na Tawbah kunasababisha kumiminiwa mvua tele, mali na watoto, na kupewa kila aina ya neema:
Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam) alipowalingania watu wake miaka ili awatoe katika shirki, aliwanasihi waombe maghfirah na tawbah na akawatajia fadhila na faida zake:
فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾
Nikasema: “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.
يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾
“Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”
وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾
“Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh: 10-12]
6-Kuomba Maghfirah Na Tawbah kunasababisha Kuingizwa Jannah:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾
Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.
أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾
Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema). [Aal-‘Imraan: 135-136]
7-Kuomba Maghfirah Na Tawbah kunasababisha Kuwekewa Nuru katika Swiraatw Siku ya Qiyaamah ambayo itammulika mtu atakapokuwa akiivuka hiyo njia:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾
Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli); asaa Rabb wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: “Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. [At-Tahriym: 8]
8-Kuomba Maghfirah Na Tawbah ni mojawapo wa Sifa Za Waja Wa Rahmaan na kunasababisha kubadilishiwa maovu ya mtu na badala yake kugezwa kuwa mema:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kutaja sifa za ‘Ibaadur-Rahmaah (Waja wa Rahmaan):
وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾
Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu.
يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾
Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Qiyaamah, na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika.
إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾
Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾
Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli. [Al-Furqaan: 68-71]
9-Kuomba Maghfirah Na Tawbah kabla ya Alfajiri ni ‘amali mojawapo za watakaoingia Jannah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿١٥﴾آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿١٨﴾
Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu. Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani.Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah. [Adh-Dhaariyaat: 15-18]
WabiLlaahi At-Tawfiyq