096-Asbaabun-Nuzuwl: Al-'Alaq Aayah 06-19: كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ
Sababu Za Kuteremshwa
Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan
096-Suwrah Al-'Alaq Aayah 6 - 19
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾
Laa hasha! Hakika mwana Aadam bila shaka amepindukia mipaka kuasi.
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾
Kwa kuwa amejiona amejitosheleza.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾
Hakika kwa Rabb wako ni marejeo.
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾
Je, umemuona yule anayekataza?
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾
Mja pale anaposwali?
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾
Je, umeona kama alikuwa katika Uongofu?
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾
Au ameamrisha kuhusu taqwa?
أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾
Je, unaonaje! Kama amekadhibisha na akakengeuka?
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾
Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾
Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa nywele za paji la uso.
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾
Paji la usio linalokadhibisha lenye hatia.
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
Basi na aite timu yake.
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah Malaika wa adhabu.
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾
Laa hasha! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Allaah). [Al-Alaq: 6-19]
Sababun-Nuzuwl:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ أَبُو جَهْلٍ هَلْ يُعَفِّرُ مُحَمَّدٌ وَجْهَهُ بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ قَالَ فَقِيلَ نَعَمْ . فَقَالَ: وَاللاَّتِ وَالْعُزَّى لَئِنْ رَأَيْتُهُ يَفْعَلُ ذَلِكَ لأَطَأَنَّ عَلَى رَقَبَتِهِ أَوْ لأُعَفِّرَنَّ وَجْهَهُ فِي التُّرَابِ. قَالَ: فَأَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُصَلِّي زَعَمَ لِيَطَأَ عَلَى رَقَبَتِهِ. قَالَ: فَمَا فَجِئَهُمْ مِنْهُ إِلاَّ وَهُوَ يَنْكِصُ عَلَى عَقِبَيْهِ وَيَتَّقِي بِيَدَيْهِ. قَالَ: فَقِيلَ لَهُ: مَا لَكَ؟ فَقَالَ: إِنَّ بَيْنِي وَبَيْنَهُ لَخَنْدَقًا مِنْ نَارٍ وَهَوْلاً وَأَجْنِحَةً . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((لَوْ دَنَا مِنِّي لاَخْتَطَفَتْهُ الْمَلاَئِكَةُ عُضْوًا عُضْوًا)) . قَالَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ - (لاَ نَدْرِي فِي حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ أَوْ شَىْءٌ بَلَغَهُ) - ((كَلاَّ إِنَّ الإِنْسَانَ لَيَطْغَى * أَنْ رَآهُ اسْتَغْنَى * إِنَّ إِلَى رَبِّكَ الرُّجْعَى * أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَى * عَبْدًا إِذَا صَلَّى * أَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ عَلَى الْهُدَى * أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَى * أَرَأَيْتَ إِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى)) يَعْنِي أَبَا جَهْلٍ ((أَلَمْ يَعْلَمْ بِأَنَّ اللَّهَ يَرَى * كَلاَّ لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ * نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ * فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ * سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ * كَلاَّ لاَ تُطِعْهُ)) زَادَ عُبَيْدُ اللَّهِ فِي حَدِيثِهِ قَالَ: وَأَمَرَهُ بِمَا أَمَرَهُ بِهِ . وَزَادَ ابْنُ عَبْدِ الأَعْلَى ((فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ)) يَعْنِي قَوْمَهُ .
Kutoka kwa Abuu Hurayrah amesema, siku moja Abuu Jahal aliuliza kama Muhammad ameutia vumbi uso wake mbele yenu? Wakajibu: Ndio! Abuu Jahal akasema: Naapa kwa Al-Laatta na Al-‘Uzzaa nikimuona anafanya hivyo basi nitamkanyaga shingo lake au nitamsigina uso wake kwenye mchanga. (Abuu Hurayrah) Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akafika akaswali na yule aliyeazimia kumsiga uso wake kwenye mchanga akawa ameanguka chini akiegemea mikono yake. Akaulizwa: Una nini Abuu Jahal? Akajibu: Baina yangu na Muhammad niliona khandaki la moto na kati yetu kuna Malaika mwenye mbawa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Lau angenisogelea basi Malaika yule angemkatakata na kumchania mbali viungo viungo. (Hatujui kama ni Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Hurayrah au yoyote iliyofikishwa kwake kutoka chanzo kingine) Akasema Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾ إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾ أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾ عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾ أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾ أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾ أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾
Laa hasha! Hakika mwana Aadam bila shaka amepindukia mipaka kuasi. Kwa kuwa amejiona amejitosheleza. Hakika kwa Rabb wako ni marejeo. Je, umemuona yule anayekataza? Mja pale anaposwali? Je, umeona kama alikuwa katika Uongofu? Au ameamrisha kuhusu taqwa? Je, unaonaje! Kama amekadhibisha na akakengeuka? [Al-‘Alaq: 6-13]
Yaani Abuu Jahal.
Na,
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾ كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾ نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾ فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾ سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾ كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾
Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona? Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa nywele za paji la uso. Paji la usio linalokadhibisha lenye hatia. Basi na aite timu yake. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah Malaika wa adhabu. Laa hasha! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Allaah). [Al-‘Alaq: 14-19]
‘Ubaydullaah amezidisha katika Hadiyth yake amesema: Na akamuamrisha kwa kile alichomuamrisha yeye. Na akazidisha Ibn ‘Abdil Al-A’laa:
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
17. Basi na aite timu yake.
[Muslim Kitaab Swiffatil Qiyaamah Wal-Jannah Wan-Naar]
Pia,
Ibn Hanbal, Muslim, An-Nasaaiy, na Ibn Abi Haatim kutoka katika Hadiyth ya Mu’tamar bin Sulaymaan, na kupokewa vile vile na Ibn Jurayj Juz 30 uk 256 na Al-Bayhaqiy Juz 1 uk 438 miongoni mwa dalili za Manabii (min dalaail an-nubuwat) na ameipokea Ibn Jariyr kwa Isnaad Swahiyh kutoka kwa Ibn ‘Abaas mfano wake na ndani yake Allaah (سبحانه وتعالى) Aliteremsha:
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾
9. Je, umemuona yule anayekataza?
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾
10. Mja pale anaposwali?
Hadi kauli Yake:
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾
16. Paji la usio linalokadhibisha lenye hatia.
Akasema: Kwa hakika yeye anajua kuwa mimi ndiye mwenye watu wengi katika bonde hili. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaghadhibika na akazungumza kitu. Daawuwd (mmoja ya watu katika Isnaad) amesema: Sikuhifadhi na Allaah Akateremsha:
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
17. Basi na aite timu yake.
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah Malaika wa adhabu.
Ibn ‘Abaas amesema: Lau angefanya hivyo basi Malaika angemchukua kutoka sehemu ile. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na akasema Hadiyth hii ni Hassan Ghariyb Swahiyh (4/216) na Ibn Jurayj (3/256) na Ahmad kama ilivyo katika Majma’ Az-Zawaaid (7/139) na akasema watu wake (Rijaal) ni watu Swahiyh.
Pia,
Kutoka kwa Ibn ‘Abaass amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali akaja Abuu Jahal akamwambia, Je, sikukutaza hili? Je sikukukataza hili? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaondoka. Abuu Jahal akasema: Wewe unajua kuwa katika bonde hili hakuna mwenye watu wengi kuliko mimi. Allaah Akateremsha:
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
17. Basi na aite timu yake.
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah Malaika wa adhabu.
Ibn ‘Abbaas amesema: Lau angejaribu kuita watu wake basi jeshi la Malaika la Allaah (Az-Zabaaniyah) wangemchukua. [Hili ni tamko la At-Tirmidhiy].