Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Hajj: Chukua Fursa Kutenda Mema Masiku Kumi Dhul-Hijjah

 

 Chukua Fursa Kutenda Mema Masiku Kumi Dhul-Hijjah

 

  Imaam Ibn ‘Uthaymiynn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Nami kwa munaasabah huu napenda kuwanasihi ndugu zangu wa Kiislamu kuchukua fursa kuchuma thawabu katika masiku kumi haya, kwani Waislamu wengi wako katika mghafiliko wa fadhila zake, na fadhila za kutenda amali humo, basi masiku yanawapita kama kwamba ni masiku ya kawaida hawayafanyi makhsusi kutokana na fadhila zake.

 

Basi inapasa katika masiku kumi ya Dhul-Hijjah kukithirisha utiifu, na matendo mema, kwa Swalaah na Swiyaam na Swadaqah na mengineyo yanayomkurubisha mtu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

[Silsilah Fataawaa Nuwr Alad-Darb Kanda 179]

 

 

 

Share