Imaam Ibn Rajab: Ramadhwaan: Kuomba Al-‘Afwu Kwa Allaah Laylatul-Qadr Na Kusameheana
Kuomba Al-‘Afwu Kwa Allaah Laylatul-Qadr Na Kusameheana
Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Allaah)
Al-‘Afuww (Mwingi wa Kusamehe) ni katika Majina ya Allaah (Ta’aalaa) Naye Hayachukulii makosa ya waja Wake. Yeye Ndiye Anayeyafuta makosa yao. Anapenda Kusamehe na kwa hiyo Anapenda kuwasamehe waja Wake.
Basi hali kadhaalika Hupenda kwamba waja Wake wasameheane. Basi pindi wanaposameheana, Yeye Hupeleka msamaha Wake juu yao. Na Anapenda msamaha Wake juu yao zaidi kuliko adhabu Yake.
[Latwaaif Wal-Ma’aarif, uk. 279]