Imaam Ibn Baaz: Kutumia Tasbihi Kuhesabu Adhkaar
Kutumia Tasbihi Kuhesabu Adhkaar
Imaam Bin Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kutumia tasbihi kwa ajili ya kumdhukuru Allaah?
JIBU:
Hatujui dalili yake katika Shariy’ah kutumia shanga kwa ajili ya kusabbih, kwa hiyo ni bora kuacha na kufuata Sunnah ambayo ni kuhesabu kwa kutumia vidole.
[Fataawaa Islaamiyyah (8/368)]
Tasbihi: Shanga zinazofungwa katika uzi au kamba; kawaida hufungwa ima 33 au 100.
