Imaam Ibn Baaz: Maana Ya Duaa Ya Ufunguzi Wa Swalaah Wa Ta’aalaa Jadduka
Maana Ya Duaa Ya Ufunguzi Wa Swalaah Wa Ta’aalaa Jadduka
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini maana ya kauli yetu katika du’aa ya ufunguzi wa Swalaah:
وَتَعـالى جَـدُّكَ
Wwa Ta’aalaaa Jadduka
Na Umetukuka Ujalali Wako
JIBU:
Maana yake ni: Ukubwa, Uadhama, Ujalali kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Suwratul Jinn kuhusu majini:
وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾
“Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.” [Al-Jinn: 3]
[Majmuw’ Al-Fataawaa 11/74]
Du’aa hiyo ya ufunguzi wa Swalaah kikamilifu ni:
سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمْـدِكَ وَتَبارَكَ اسْمُـكَ وَتَعـالى جَـدُّكَ وَلا إِلهَ غَيْرُك
Subhaanaka-LLaahumma wabihamdika watabaarakas-Smuka wa Ta’aalaaa Jadduka walaa ilaaha Ghayruka
Utakasifu ni Wako Ee Allaah, na Himdi ni Zako, na Limebarikika Jina Lako, na Umetukuka Ujalali Wako, na hapana muabudiwa wa haki, ghairi Yako