Imaam Ibn Baaz: Mume Hafungi Ramadhwaan Nami Nampikia Chakula Je Napata Dhambi?

Mume Hafungi Ramadhwaan Nami Nampikia Chakula Je Napata Dhambi?

 

Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mume wangu hataki kufunga zaidi ya miaka ishirini. Kipindi chote hicho nilikuwa nikimpikia chakula wakati mimi mwenyewe nimefunga. Je ninapata madhambi?

 

JIBU:

 

Ndiyo, ni dhambi. Lazima utubu kwa Allaah  kwa kitendo hicho.  Wakati wewe unampikia chakula mchana wa Ramadhwaan, unamsaidia kumuasi Allaah (’Azza wa Jall). Allaah (Jalla wa 'Alaa) Anasema:

  وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah : 2]

Kumpikia chakula au kumtengea chakula na kumpa mchana wa Ramadhwaan au kumpa sigara au pombe n.k. ni dhambi, na ni maovu juu ya maovu. Hupaswi kabisa kumsaidia kutofunga sawa ikiwa ni (kwa kumpa) chakula, kinywaji, sigara au pombe. Yote haya ni madhambi juu ya madhambi, Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. Bali ni juu yako kumnasihi na kukataa kumtii na kumwambia huwezi kumsadia kwa hilo, na arudie kubeba madhambi mwenyewe.

 

[Mawqi' Ar-Rasmiy li-Imaam bin Baaz]

 

Share