Imaam Ibn Baaz: Kupiga Picha Na Kuweka Kwa Ajili Ya Kumbukumbu
Kupiga Picha Na Kuweka Kwa Ajili Ya Kumbukumbu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nnapokwenda kutembea sehemu kadhaa pamoja na kundi la marafiki huwa napiga picha kuziweka kama kumbukumbu. Nini hukmu ya kupiga picha kwa ajili hii?
JIBU:
Hukmu ya kupiga picha kwa ajili hii ni haramu yaani ikiwa picha ni yenye roho (bin Aadam au mnyama).
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watu watakaoadhibiwa vikali Siku ya Qiyaamah ni wenye kuchora picha.” [Al-Bukhaariy na Muslim].
Pia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelaani wachoraji picha.
Ama kupiga picha vitu ambavo havina roho kama gari, ndege, miti n.k., hivi hakuna ubaya. Wa biLLaahi At-Tawfiyq.
[Fataawa Islaamiyyah (8/125)]