Swalatul-Haajah Ni Swahiyh? Kama Swahiyh Ni Ipi Du'aa Yake?

 

Swalatul-Haajah Ni Swahiyh? Kama Swahiyh Ni Ipi Du'aa Yake?

 

Alhidaaya.com

 

Swali:

 

Naomba unifahamishe dua za kuomba katika sala za usiku? (salat alhaja)

 

Wasalam alykum.

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Katika Swali la muulizaji kuna mas-ala mawili; Swalah ya Usiku (Tahajjud) na Swala ya Haja (Swalaatul-Haajah). Kuna tofauti ya Swalah mbili hizi.

 

Swalah ya Usiku:

 

Swalah za usiku zote ni za Sunnah, na zinajulikana kuwa ni "Qiyaamul-layl" (kisimamo cha usiku). Nazi ni ima Swalah ya Tarawiyh, au Witr au  Tahajjud. Katika Swalaatul-Witr kuna Du'aa ya Qunuut, tafadhali soma katika kiungo kifuatacho kilichomo katika ALHIDAAYA kupata maelezo kamili:

 

Du'aa za Qunut Ziko Ngapi Na Je Lazima Zisomwe Katika Swalah Ya Alfajiri?

 

Na kuhusu Swalaatut-Tahajjud haikuthibiti kuwa kuna du'aa hasa ya kusoma katika Swalah hii isipokuwa imethibiti kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa salam) alipokuwa akiamka usiku kabla ya kuingia kwenye Swalah husoma Aayah katika Suwraah Al-'Imraan ambazo ndani yake zimo Du'aa. Aayah hizo ni kuanzia namba 190 mpaka mwisho wa Suwraah hiyo tukufu: 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara,zingatio) kwa wenye akili. [Al-Imraan: 190].

 

Kisha soma katika kiungo kifuatacho kupata maelezo zaidi ya  Swalah hiyo ya Tahajjud.  

 

Wakati Wa Swalah Ya Tahajjud Na Vipi Kuswali

 

Nini Fadhila Za Swalah Ya Tahajjud?

 

Swalaatul-Haajah (Swalah Ya Haja)

 

Ama kuhusu Swalah ya Haja, haikuthibitika kuwa imo katika sharia’h, ingawa Hadiyth iliyoeleza hayo baadhi ya Maulamaa wameikubali, lakini masimulizi yaliyotajwa ya Swalah hiyo yameonekana kuwa ni Hadiyth dhaifu isiyotegemewa nayo ni kutoka kwa At-Tirmidhiy kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Yeyote mwenye haja ya kitu kutoka kwa Allaah au kutoka kwa binaadamu, afanya wudhuu vizuri kisha aswali Raka'ah mbili, kisha amtukuze Allaah na amtakie Rahma na amani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha asome Du'aa: Laa ilaaha illa Allaah Al-Haliymul-Kariym. Subhaana Allaahi Rabbil-‘arshil-‘adhiym. Al-Hamdu Lillaahi Rabbil-‘Aalamiyn. As-aluka muujibaati Rahmatik wa 'azaaim Maghfiratik wal-Ghaniymatu min kulli ithm.  Laa tada' liy dhanban illa Ghafartah, wa laa hamman illa Farrajtah, wa la Haajatan hiya Laka Ridhwaa illa Qadhwaytahu Yaa Arhamar-Raahimiyn))

 

[Abu 'Iysa (yaani At-Tirmdhiy) amesema: Hii ni Hadiyth ghariyb. Na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hadiyth dhaifu sana.] [Al-Haakim amesema ni Hadiyth dhaifu iliyosimuliwa na Ibn Abi Awfaa (Mishkaatul-Maswaabiyh 1/417)  ambayo imesimuliwa na Ibn Maajah]

 

Hivyo Swalah hiyo haimo katika shari’ah na inapasa kutoiswali bali omba haja zako kwenye Du'aa katika hali na nyakati  zifuatazo kwa ufupi. Muhimu zaidi ni kuanzia Du'aa zako kwa kumtukuza Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa kisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kabla ya kuanza Dua'a na unapomaliza Du'aa yako.    

 

1.     Thuluthi ya mwisho ya usiku, kwani hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Huteremka tokea mbingu ya saba na kuja mbingu ya duniani yaani ya kwanza kutusikiliza tunayoyaomba ili Atupe kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:  ((ينزل ربنا تبارك وتعالى كل ليلة إلى السماء الدنيا حين يبقى ثلث الليل الآخر فيقول: من يدعوني فأستجيب له؟ من يسألني فأعطيه؟ من يستغفرني فأغفر له ))

Imetoka kwa Abu Hurayrah Radhwi Allaahu 'anhu kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: (Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa) Huteremka kila siku katika mbingu ya dunia (mbingu ya kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya  usiku   na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ana shida Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie? )) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

2.     Baina ya Adhaana na Iqaamah ya Swalah.

 

3.     Inaponyesha mvua (au barafu)

 

4.     Kwenye kusujudu.

 

5.     Du'aa baada ya Swalah (baada ya tashahhud kabla ya kutoa salaam).

 

6.     Unapokunywa maji ya Zam-zam kwa Niyah yake ya kuomba unachotaka.

 

7.  Unaposema Du'aa ya Nabii Yunus (Alayhis Salaam) nayo ni  "Laa Ilaaha Illa Anta Subhaanaka Inni Kuntu Minadhwaalimiyn"

 

8.    Unaposema Du'aa ya: "Allaahumma Inni As-aluka Bianniy Ash-hadu Annaka Anta Allaahu Laa Ilaaha Illa Antal-Ahadus-Swamadu-lladhiy Lam Yalid wa lam Yuulad wa Lam Yakun-Lahuu kufuwan Ahad"

 

9.     Saa katika siku ya Ijumaa (na aghlabu ya kauli ni baina ya Swalah ya Alasiri na Magharibi)

 

10.    Du'aa unapofunga (Swawm)

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share