Nini Fadhila Za Swalah Ya Tahajjud?

Nini Fadhila Za Swalah Ya Tahajjud?

 

SWALI:

Asalam Aleikum

Nini fadhila ya sala ya Tahajud?

WABILAHI TAUFIQ

 


JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Aliyetukuka Mola

wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.

 

Fadhila za kuswali Swalah ya Tahajjud zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah. Katika Qur-aan aghalabu huambatanishwa na Jannah. Na hakika kuamka kuswali usiku humzidishia Muislamu iymaan yake, akapata utulivu, furaha ya nafsi na kuridhika kwa nafsi, na vile vile ni njia mojawapo njema ya kumshukuru Allaah (Subhaana wa Ta'aala). Kumshukuru Allaah (Subhaana wa Ta'aala) sio kwa kukiri pekee bali iwe ndani ya moyo pia na kwa kutumia viungo vyetu katika ibada zaidi. Ikiwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amefutiwa madhambi yake yaliyotangulia na yaliyofuatia alikuwa akiswali Tahajjud hadi miguu yake ikifura, kwa nini basi sisi tusiitimiza Swalah hii?

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida tele:

 

Fadhila Na Faida Za Qiyaamul-Layl

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

Share