07-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atatoka Motoni Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akiiwa Moyoni Mwake Kuna Kheri (Iymaan) Kiasi Cha Uzani Wa Shairi Au Mbegu Au Punje

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

07-Atatoka Motoni Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akiwa Moyoni Mwake Kuna Khayr (Iymaan) Kiasi Cha Uzani Wa Shairi Au Mbegu Au Punje

 

 

عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ شَعِيرَةٍ مِنْ خَيْرٍ، وَيَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ بُرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ، وَيَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ))  الْبخاري ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atatoka motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah (hakuna muabudiwa wa haki ila Allaah)) akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha uzani wa shairi. Na Atatoka motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha mbegu moja. Na atatoka motoni anayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha uzani wa punje)). [Al-Bukhaariy (44) Muslim (193)]

 

Share