08-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Kauli Thabiti Ya Uhai Wa Dunia Na Aakhirah
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah
08-Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Kauli Thabiti Ya Uhai Wa Dunia Na Aakhirah
عَنْ الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر شَهِدَ أَنْ لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ))) البخاري وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة
Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha illa-Allaah wa anna Muhammadar-Rasuwlu-Allaah" [Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah] hiyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah: “Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah”)). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]