09-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayefurahika Zaidi Kwa Shafaa Ya Nabiy Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Kwa Niyyah Safi Moyoni Au Nafsini Mwake

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

09-Atakayefurahika Zaidi Kwa Shafaa Ya Nabiy Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Kwa Niyyah Safi Moyoni Au Nafsini Mwake

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  قُلْتُ يَا رَسُولَ اللهِ مَنْ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ؟ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلى اللهُ عليهِ وَسَلَّمَ: ((لَقَدْ ظَنَنْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ أَنْ لا يَسْأَلَني عَنْ هذَا الْحَدِيِثِ أَحَدٌ أَوَّلَ مِنْكَ لِما رَأَيْتُ مِنْ حِرْصِكَ عَلَى الْحَدِيثِ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَنْ قَالَ: لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ خَالِصَاً مِنْ قَلْبِهِ أَوْ نَفْسِهِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nani atakayefurahika kabisa kwa Shafaa’ah (uombezi) wako Siku ya Qiyaamah: Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Nlidhani ee Abaa Hurayrayh kwamba hakuna yeyote asiyekuwa wewe atakayeniuliza maelezo haya kwa vile jinsi nilivyoona himma yako juu ya jambo hili. Atakayefurahika zaidi kati ya watu kwa Shafaa’ah yangu Siku ya Qiyaamah ni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, kwa niyyah safi moyoni mwake au nafsi yake)). [Al-Bukhaariy]

 

Share