12-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Miongoni Mwa Mambo Matano Yatakayokuwa Mazito Katika Mizani Siku Ya Qiyaamah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

12-Miongoni Mwa Mambo Matano Yatakayokuwa Mazito Katika Mizani Siku Ya Qiyaamah

 

 

عن ثوبان رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((بَخٍ بَخٍ لِخمسٍ ما أثقلَهُنَّ في الميزانِ : لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ، والولَدُ الصالِحُ يُتوَفَّى للمرْءِ المسلِمِ فيَحتَسِبُهُ)) النسائي وابن حبان والحاكم ، وأحمد ، وصححه الألباني في صحيح  الترغيب والجامع    

 

Imetoka kwa Thuwbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Heko heko kwa vitu vitano, uzito gani vitakavyokuwa  katika Mizani; Laa Ilaah Illa  Allaah, Wa-Allaahu Akbar, Wa Subhaanah-Allaah, Wa-AlhamduliLLah, na mtoto mwema atakayekufa na wazazi wake wanatarajia thawabu kutoka kwa Allaah)) [An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Ahmad, na kaisahihisha Al-Albaaniy katika:  Swahiyh At-Targhiyb (1557), Swahiyh Al-Jaami'(2817)]

 

 

Share