13-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah:Moto Hautamgusa Atakayeruzukiwa Kauli Hiyo Katika Mauti Yake

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

13- Moto Hautamgusa Atakayeruzukiwa Kauli Hiyo Katika Mauti Yake

 

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ، وَأَبِي سَعِيدٍ، أَنَّهُمَا شَهِدَا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((إِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ. يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَأَنَا أَكْبَرُ. وَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا وَحْدِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَا شَرِيكَ لَهُ. قَالَ : صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا شَرِيكَ لِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ  قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، لِي الْمُلْكُ، وَلِيَ الْحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِي. ثم قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  مَنْ رُزِقَهُنَّ عِنْدَ مَوْتِهِ لَمْ تَمَسَّهُ النَّارُ))

 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah na Abuu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wameshuhudia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((Mja akisema: “laa ilaaha illa Allaah wa Allaahu Akbar – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa.”  Allaah ‘Azza wa Jalla Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Nami ni Mkubwa.” Akisema mja: “Laa ilaaha illa Allaah Wahdahu – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee.” Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Pekee.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu laa shariyka Lahu - hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hana mshirika.” Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi sina Mshirika.”.Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, ufalme na Himdi ni Zake.” Husema: Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, Ufalme na Himdi ni Zangu.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu, walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah.” Husema: Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka Kwangu.” Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Atakayeruzukiwa [kauli] hiyo wakati wa mauti yake, An-Naar [Moto] hautomgusa)). [Ibn Maajah (3794) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (713)]

 

 

 

Share