04-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah:Mlango Wa Wudhuu
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتابُ الطَّهارَة
Kitabu Cha Twahaarah
بَابُ اَلْوُضُوءِ
04-Mlango Wa Wudhuu
29.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: { لَوْلَا أَنْ أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي لَأَمَرْتُهُمْ بِالسِّوَاكِ مَعَ كُلِّ وُضُوءٍ } أَخْرَجَهُ مَالِكٌ، وأَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة َ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau nisingeuogopea uzito ummah wangu, ningeliwaamrisha mswaki[1] kabla ya kila Swalaah.” [Imetolewa na Maalik, Ahmad na An-Nasaaiy. Akaisahihisha Ibn Khuzaymah]
30.
وَعَنْ حُمْرَانَ; { أَنَّ عُثْمَانَ رضى الله عنه دَعَا بِوَضُوءٍ، فَغَسَلَ كَفَّيْهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ مَضْمَضَ، وَاسْتَنْشَقَ، وَاسْتَنْثَرَ، ثُمَّ غَسَلَ وَجْهَهُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ يَدَهُ اَلْيُمْنَى إِلَى اَلْمِرْفَقِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ اَلْيُسْرَى مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ مَسَحَ بِرَأْسِهِ، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَهُ اَلْيُمْنَى إِلَى اَلْكَعْبَيْنِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ اَلْيُسْرَى مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ قَالَ: رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَوَضَّأَ نَحْوَ وُضُوئِي هَذَا } مُتَّفَقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa Humraan[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) mtumwa aliyeachwa huru na ‘’Uthmaan[3] amesema kuwa: “’Uthmaan alitaka maji ya kutawadhia. Akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akasukutua na akatia maji puani, na kisha akapenga. Kisha akaosha uso wake mara tatu. Kisha akaosha mkono wake wa kuume hadi kwenye kiwiko cha mkono wake (fundo kati ya kiganja na bega) mara tatu[4], kisha akauosha hivyo hivyo mkono wake wa kushoto. Kisha akapaka maji kichwa chake. Kisha akauosha mguu wake wa kuume hadi kwenye vifundi viwili mara tatu, kisha akauosha mguu wake wa kushoto hivyo hivyo. Kisha akasema: Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akitawadha mfano wa wudhuu wangu huu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
31.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه فِي صِفَةِ وُضُوءِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: { وَمَسَحَ بِرَأْسِهِ وَاحِدَةً. } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُد
Kutoka kwa ‘Aliy[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu wasifu wa wudhuu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuwa: “Nabiy alipangusa kichwa chake kwa maji mara moja tu[6].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]
32.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ بْنِ عَاصِمٍ رضى الله عنه فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ قَالَ: { وَمَسَحَ صلى الله عليه وسلم بِرَأْسِهِ، فَأَقْبَلَ بِيَدَيْهِ وَأَدْبَرَ. } مُتَّفَقٌ عَلَيْه
وَفِي لَفْظٍ: { بَدَأَ بِمُقَدَّمِ رَأْسِهِ، حَتَّى ذَهَبَ بِهِمَا إِلَى قَفَاهُ، ثُمَّ رَدَّهُمَا إِلَى اَلْمَكَانِ اَلَّذِي بَدَأَ مِنْهُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd bin ‘Aaswim[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema akielezea sifa ya wudhuu: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipangusa kichwa chake kutoka katika paji la uso mpaka kisogoni na kisha mpaka kwenye paji la uso[8].” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika riwaayah nyengine ya Al-Bukhaariy na Muslim: “Ameanza mwanzo wa kichwa chake kwa mikono yake hadi akaipeleka kisogoni mwake, kisha akairudisha mahali alipoanza.”
33.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ قَالَ: { ثُمَّ مَسَحَ صلى الله عليه وسلم بِرَأْسِهِ، وَأَدْخَلَ إِصْبَعَيْهِ اَلسَّبَّاحَتَيْنِ فِي أُذُنَيْهِ، وَمَسَحَ بِإِبْهَامَيْهِ ظَاهِرَ أُذُنَيْهِ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr[9] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu sifa za wudhuu: “Kisha Rasuli wa Alllaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipangusa kichwa chake, akaingiza vidole vyake vya Shahaadah katika masikio yake, na akapangusa nje ya masikio yake kwa vidole gumba.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na ameisahihisha Ibn Khuzaymah]
34.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِذَا اِسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَنَامِهِ فَلْيَسْتَنْثِرْ ثَلَاثًا، فَإِنَّ اَلشَّيْطَانَ يَبِيتُ عَلَى خَيْشُومِهِ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakapoamka mmoja wenu usingizini, apenge pua mara tatu, kwani shaytwaan hulala kwenye mionzi ya pua[10] yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
35.
وَعَنْهُ: { إِذَا اِسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلَا يَغْمِسُ يَدَهُ فِي اَلْإِنَاءِ حَتَّى يَغْسِلَهَا ثَلَاثًا فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدَهُ } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ. وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Rasuli wa Allah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Akiamka mmoja wenu usingizini, asizamishe mikono yake katika chombo chochote, hadi aioshe mara tatu[11], kwani hajui mkono wake ulilala wapi.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
36.
وَعَنْ لَقِيطِ بْنُ صَبْرَةَ، رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أَسْبِغْ اَلْوُضُوءَ، وَخَلِّلْ بَيْنَ اَلْأَصَابِعِ، وَبَالِغْ فِي اَلِاسْتِنْشَاقِ، إِلَّا أَنْ تَكُونَ صَائِمًا } أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة
وَلِأَبِي دَاوُدَ فِي رِوَايَةٍ: { إِذَا تَوَضَّأْتَ فَمَضْمِضْ }
Kutoka kwa Laqiytw bin Swabrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tawadha kikamilifu, na pitisha kati ya vidole vyako vya mikono na miguu[12], zidisha katika kuyapandisha maji puani isipokuwa utakapokuwa uko katika Swawm.” [Imetolewa na Al-Arba’ah; Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah na ameisahihisha Ibn Khuzaymah]
Na katika riwaayah ya Abuu Daawuwd: “Ukitawadha, sukutua mdomo wako.”
37.
وَعَنْ عُثْمَانَ رضى الله عنه { أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يُخَلِّلُ لِحْيَتَهُ فِي اَلْوُضُوءِ } أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة
Kutoka kwa ‘Uthmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akitawadha, alikuwa akipitisha vidole kati ya ndevu[13] zake.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Ibn Khuzaymah]
38.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ رضى الله عنه { أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم أَتَى بِثُلُثَيْ مُدٍّ، فَجَعَلَ يَدْلُكُ ذِرَاعَيْهِ } أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliletewa thuluthi mbili za Mudd[14] (kibaba cha maji), akawa anasugua mikono yake.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]
39.
وَعَنْهُ، { أَنَّهُ رَأَى اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَأْخُذُ لِأُذُنَيْهِ مَاءً غَيْرَ اَلَّذِي أَخَذَ لِرَأْسِهِ. } أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيّ
وَهُوَ عِنْدَ "مُسْلِمٍ" مِنْ هَذَا اَلْوَجْهِ بِلَفْظٍ: وَمَسَحَ بِرَأْسِهِ بِمَاءٍ غَيْرَ فَضْلِ يَدَيْهِ، وَهُوَ اَلْمَحْفُوظ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akichukua maji kupangusa masikio, tofauti na maji aliyopangusia kichwa.” [Imetolewa na Bayhaqqiy]
Na katika riwaayah ya Muslim: “Alipangusa kichwa chake kwa kuchukua maji yasiyokuwa yaliyosalia kutoka katika maji ya kuoshea mikono.” [Hadithi hii ni Mahfuwdh]
40.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: { "إِنَّ أُمَّتِي يَأْتُونَ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ غُرًّا مُحَجَّلِينَ، مِنْ أَثَرِ اَلْوُضُوءِ، فَمَنْ اِسْتَطَاعَ مِنْكُمْ أَنْ يُطِيلَ غُرَّتَهُ فَلْيَفْعَلْ. } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Ummah wangu utakuja siku ya Qiyaamah na viungo vinavyong’aa (nyuso, mikono, miguu) kwa sababu ya alama za wudhuu, basi mwenye kuweza miongoni mwenu kuirefusha mng’aro wake[15], basi afanye hivyo.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
41.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: { كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يُعْجِبُهُ اَلتَّيَمُّنُ فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهُ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ. } مُتَّفَقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anapendezwa sana na kuanza na upande wa kuume katika kuvaa kwake viatu; na katika kuchana nywele, na katika kujitwaharisha kwake, na katika mambo yote[16].” [Al-Bukhaariy, Muslim]
42.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِذَا تَوَضَّأْتُمْ فابدأوا بِمَيَامِنِكُمْ } أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnapotawadha, anzeni kulia kwenu.” [Imetolewa na Al-Arba’ah; Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]
43.
وَعَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةٍ رضى الله عنه { أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم تَوَضَّأَ، فَمَسَحَ بِنَاصِيَتِهِ، وَعَلَى اَلْعِمَامَةِ وَالْخُفَّيْنِ } أَخْرَجَهُ مُسْلِم
Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah[17] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitawadha na akawa ni mwenye kupangusa maji utosi wake na juu ya kilemba, na juu ya soksi (khofu) mbili za ngozi[18].” [Imetolewa na Muslim]
44.
وَعَنْ جَابِرٍ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا فِي صِفَةِ حَجِّ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ صلى الله عليه وسلم { اِبْدَؤُوا بِمَا بَدَأَ اَللَّهُ بِهِ } أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ، هَكَذَا بِلَفْظِ اَلْأَمْر وَهُوَ عِنْدَ مُسْلِمٍ بِلَفْظِ اَلْخَبَر
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu Hijjah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anzeni kwa Alichoanza nacho Allaah[20].” [Imetolewa na An-Nasaaiy kwa tamshi hili la amri na imepokewa na Muslim kwa tamko la Al-Khabar[21]]
45.
وَعَنْهُ قَالَ: { كَانَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم إِذَا تَوَضَّأَ أَدَارَ اَلْمَاءَ عَلَى مُرْفَقَيْهِ. } أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادِ ضَعِيف
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anapotawadha hutiririsha maji hadi kwenye kiwiko.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy kwa Isnaad dhaifu]
46.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { لَا وُضُوءَ لِمَنْ لَمْ يَذْكُرِ اِسْمَ اَللَّهِ عَلَيْهِ } أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ، بِإِسْنَادٍ ضَعِيف
وَلِلترْمِذِيِّ: عَنْ سَعِيدِ بْنِ زَيْد ٍ
وَأَبِي سَعِيدٍ نَحْوُه ُ
قَالَ أَحْمَدُ: لَا يَثْبُتُ فِيهِ شَيْء
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna wudhuu kwa asiyetaja Jina la Allaah wakati wa kutawadha[22].” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na Ibn Maajah, kwa Isnaad dhaifu]
Na katika At-Tirmidhiy: “amepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa Sa’iyd bin Zayd[23].”
Na Abuu Sa’iyd na Ahmad wamesema: “Hakujathibitika chochote ndani yake Hadiyth hiyo.”
47.
وَعَنْ طَلْحَةَ بْنِ مُصَرِّفٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: { رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَفْصِلُ بَيْنَ اَلْمَضْمَضَةِ وَالِاسْتِنْشَاقِ. } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادِ ضَعِيف
Kutoka kwa Twalhah bin Muswarrif[24] amemnukuu baba yake kwa upokezi wa babu yake[25] aliyesema: “Nimemuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akitenganisha kati ya kusukutua na kupandisha maji puani[26].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad dhaifu]
48.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ { ثُمَّ تَمَضْمَضَ صلى الله عليه وسلم وَاسْتَنْثَرَ ثَلَاثًا، يُمَضْمِضُ وَيَنْثِرُ مِنْ اَلْكَفِّ اَلَّذِي يَأْخُذُ مِنْهُ اَلْمَاءَ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَالنَّسَائِيّ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu wasifu wa kutawadha, “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisukutua kisha akavuta maji puani na kupenga mara tatu. Alisukutua na akapenga pua yake kwa kiganja kilekile alichochukulia maji.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nassaiy]
49.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ رضى الله عنه فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ { ثُمَّ أَدْخَلَ صلى الله عليه وسلم يَدَهُ، فَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ مِنْ كَفٍّ وَاحِدَةٍ، يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلَاثًا } مُتَّفَقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu wasifu wa kutawadha: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitumbukiza mkono wake (katika chombo), akasukutua na akapandisha maji puani kwa fumbo moja (maji). Alifanya hivyo mara tatu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
50.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: { رَأَى اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم رَجُلًا، وَفِي قَدَمِهِ مِثْلُ اَلظُّفْرِ لَمْ يُصِبْهُ اَلْمَاءُ. فَقَالَ: "اِرْجِعْ فَأَحْسِنْ وُضُوءَكَ" } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيّ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuona mtu katika unyayo wake kuna mfano wa kucha (baka) haikupata maji. Akamwambia: ‘Rejea vizuri wudhuu wako[27].’” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]
51.
وَعَنْهُ قَالَ: { كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَتَوَضَّأُ بِالْمُدِّ، وَيَغْتَسِلُ بِالصَّاعِ إِلَى خَمْسَةِ أَمْدَادٍ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitawadha kwa kibaba[28] kimoja cha maji, na akikoga kwa pishi[29] moja hadi vibaba (Mudd) vitano.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
52.
وَعَنْ عُمَرَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ، فَيُسْبِغُ اَلْوُضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ اَلْجَنَّةِ" } أَخْرَجَهُ مُسْلِم
وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَزَادَ: { اَللَّهُمَّ اِجْعَلْنِي مِنْ اَلتَّوَّابِينَ، وَاجْعَلْنِي مِنْ اَلْمُتَطَهِّرِينَ }
Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu anayetawadha vizuri, kisha akasema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, wa ash-hadu anna Muhammad ‘Abduhuu wa Rasuwluhu” (Nashuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake, hana mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake) ila atafunguliwa milango minane ya Jannah.” [Imetolewa na Muslim na At-Tirmidhiy]
At-Tirmidhiy aliongezea: “Allaahummaj-‘alniy minat-tawaabiyna Waj-‘alniy minal-mutatwahhiriyna (Ee Rabi! Nijaalie niwe miongoni mwa wenye kutubia na unijaalie niwe miongoni mwa wenye kujitwaharisha)”
[1] Hii inamaanisha kuwa matumizi ya mswaki kila mtu anapotawadha ni Sunnah, na Hadiyth hii iliyoripotiwa na Muslim inatuambia kwamba, ni sharti kutumia mswaki kabla ya kila Swalaah. Inamaanisha kuwa, haya tule anayekuenda kuswali na ‘udwuu ule ule aliotawadha safari iliyopita, hata hivyo sharti atumie mswaki. Ahadiyth hizi zinathibitisha mkazo mkubwa sana unaowekwa katika matumizi ya mswaki kila mara kwa ajili ya kusafisha meno. Hiyo ni Sunnah na siyo waajibu
[2] Humraan bin Aban alikamatwa na Khaalid bin Al-Waliyd katika vita wakati wa Ukhalifa wa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), naye akampeleka akamtumikie ‘Uthmaan ambaye alimuacha huru. Ni mwaminifu wa daraja la pili katika kuripoti Hadiyth. Alifariki mwano mwaka wa 75 A.H.
[3] ‘Uthmaan ni Khalifa wa tatu kati ya wanne walio wakuu au walioongozwa. Alisilimu mapema na akamuoa Ruqayyah bint wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na baada ya kufariki kwake akaozwa bint mwingine wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Ummu-Kulthum na hivyo anaitwa Dhun-Nurayn (yaani mwenye nuru mbili, maana yake mabinti wawili wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)). ‘Uthmaan aliuliwa shahidi siku ya Ijumaa tarehe 18 Dhul-Hijjah mwaka 35 A.H.
[4] Katika Hadiyth hii, kuosha uso, mikono na miguu, imetajwa kuwa vioshwe mara tatu kila kiuongo, lakini viungo vingine, inatosha kuviosha mara mbili au hata mara moja kila kiungo. Imaam Nawawi ameandika kuwa maafikiano ya pamoja ni kwamba kuosha mara moja ni faradhi yaani lazima.
[5] ‘Aliy ni Khalifa wa nne walioongozwa. Alipigana vita zote isipokuwa ya Tabuwk, kwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuacha akikaimu kule Madiynah. Mtu mmoja muovu aitwae ‘Abdur-Rahmaan bin Muljam, alimuua ‘Aliy akafa kama ni Shahidi asubuhi siku ya Ijumaa tarehe 17 mwezi Ramadhwaan mwaka 40 A.H huko Kufa.
[6] Hii maana yake ni kwamba kupangusa maji kichwa wakati wa kutawadha mara moja tu ndiyo faradha.
[7] ‘Abdullaah bin Zayd alikuwa Answaar (watu wa Madiynah waliowapokea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na wenziwe wa Makkah waliohajiri Madiynah), aliyetoka kwa akina Bani Maazin kutoka katika ukoo wa An-Najaar. Alipigana katika vita vya Uhud alimuua Musailimah Al-Kadhdhaab na pia alimuua Wahshi mnamo Siku ya Al-Yamama. Aliuwawa mnamo siku ya Al-Harraah mnamo mwaka 63 A.H.
[8] Hadiyth hii inatuambia kupangusa maji (mas-h) kichwani sharti kuanzie mbele.
[9] ‘Abdullaah bin ‘Amr mwana wa ‘Amr bin Al-‘Aasw Al-Qurayshiy. Yeye alisilimu kabla ya babake ambaye alikuwa mkubwa kuliko yeye kwa miaka 13. Alikuwa ni ‘Aalim (msomi), alihifadhi Hadiyth na alikuwa mwenye taqwa sana. Alifariki mnamo mwaka 63 au 70 A.H.
[10] Kwa shaytwaan kulala ndani ya pua za mtu kunawezekana, lakini hali halisi inayotokea inajulikana na Mwenyewe Allaah (عز وجل) na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Huenda huo ni usemi wa kimethali, kwa sababu kamasi mbaya hukusanyika puani na kusababisha uzembe, uvivu, kusahau au kupuuza. Hali hizi zote ni za kishaytwaan.
[11] Hii inamaanisha kuwa, mikono isitumbukizwe katika chombo cha maji ya kutawadhia, kwa kuwa neno “kutawadha” limo katika Hadiyth zilizoandikwa na Al-Bukhaariy. Ibn Hajar, katika kitabu chake cha Fat-h Al-Baariy amesema kuwa: “Ingawa Hadiyth hii inataja vyombo vya kutawadhia, lakini inajumuisha vyombo vyote vingine pamoja na vyombo vya kuogea. Lakini kukiweko bwawa kubwa au tanki la maji, basi inaruhusiwa kutumbukiza mkono humo.”
[12] Hii inamaanisha kuwa vidole vya mikononi na miguuni sharti vioshwe taratibu na kikamilifu.
[13] Wakati wa tendo la kutawadha, kuchanua ndevu zako kwa vidole vyako ni Sunnah na siyo lazima (wajibu).
[14] Katika Hadiyth zingine, Mudd kamili ni zaidi kidogo ya gram 600. Hii ndio idadi ndogo kuliko idadi zote zilizotajwa kwa ajili ya kutawadha, vinginevyo itakuwa tabu kubwa kutawadha kwa maji kidogo zaidi ya hivi. Hakijatajwa kiwango cha juu cha maji. Kiasi chochote cha maji kinaweza kutumika kwa kutawadha na kuoga, lakini inakatazwa kufanya israfu ya maji.
[15] Hii inaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Inaweza kumaanisha kuosha viungo zaidi ya kiwango cha chini, kwa mfano, kuosha mikono hadi mabegani, na kuosha miguu hadi magotini. Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) anaiafiki hii maana ya pili. Pia inaweza kumaanisha kuosha kila kiungo mara tatu, badala ya kuosha viungo kama vile viganja, mdomo na pua kwa uchache mara moja. Pia inaweza kumaanisha kutawadha tena na tena, au hata kubaki na wudhuu huo huo mmoja saa zote.
[16] Mtindo huu (wakuanzia kiungo cha kuume) wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ulikuwa ni kwa matendo mema. Lakini kwa matendo mengine kama kuenda nje ya Msikiti, au kuingia chooni, ambapo mtu ni sharti atangulize mguu wa kushoto kwanza.
[17] Al-Mughiyrah ndiye Abuu ‘Abdillaah au Abuu Lisa. Al-Mughiyrah bin Shu’bah bin Mas-‘uwd Ath-Thaqaaf alikuwa Swahaba maarufu. Alisilimu mnamo mwaka wa vita ya Khandaq (Handaki), na akahajiri. Kwanza alishiriki katika vita ya Hudaybiyah. Alifariki mnamo mwaka 50 A.H. kule Kufa.
[18] Hadiyth hii inaweka wazi wazi kwamba, kupangusa maji kidogo juu ya kilemba (kofia) ni sahihi. Kuna aina mbili za tendo hili. Kwanza ni kupangusa kidogo juu ya kilemba na kidogo juu ya kichwa. Hakuna tofauti ya maoni juu ya tendo hili. Pili ni kupangusa juu ya kilemba peke yake. Kuna tofauti ya maoni kwa hili, lakini hii inathibitishwa pia na Hadiyth Swahiyh ya At-Tirmidhiy.
[19] Jaabir alikuwa Answaar aliyetoka katika ukoo wa Sulamiy, na alipewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Alikuwa mmoja wa Swahaba maarufu. Alipigana katika vita vya Badr, ingawa wengine wanasema kuwa hakuwahi kuishuhudia vita vya Badr wala ya Uhud, lakini alishiriki katika vita zilizofuata hizo. Pia alikuwako kule Siffin. Alikuwa mmoja wa watu waliohifadhi Hadiyth nyingi. Alipata upofu mnamo mwisho wa maisha yake, alifariki mnamo mwaka wa 74 A.H akiwa na umri wa miaka 94. Inasemekana kuwa yeye ndiye aliyekuwa Swahaba wa mwisho kufariki pale Madiynah.
[20] Qur-aan tukufu imetaja kwanza Asw-Swafaa katika kutaja Asw-Swafaa na Al-Marwaa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliianza Saa’i (kutembea na kukimbia kati ya Asw-Swafaa na Al-Marwaa wakati wa kuhiji Hijjah kubwa (Hajj) na Hijjah ndogo (‘Umrah) kutokea upande wa Asw-Swafaa). Kwa hivyo anzeni kutawada kwa namna hiyo hiyo – kuanzia kuosha uso, kisha mikono mpaka katika kiwiko, kisha pangusa kichwa, na kisha osha miguu (kama alivyovifanya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).
[21] Katika Hadiyth hii limetumika neno “bada-a” katika maandishi ya Kiarabu, kwa maana ya kutoa taarifa (kwa mfano naanza kwa) na siyo kwa kuamrisha (anza kwa).
[22] Kuhusu kadhia hii, zipo Ahaadiyth zinazopingana ambazo zinaashiria maoni yanayopishana kuhusu kuitamka “BismiLlaah” kabla ya kuanza kutawadha. Jibu sahihi la kadhia hii ni kusema kuwa, kutamka BismiLlaah ni Sunnah.
[23] Sa’iyd huyu ndiye Sa’iyd bin ‘Amr Al-Qurayshiy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), aliyepewa jina la utani la Abuu Al-A’war. Naye ni mmoja wa wale watu kumi waliyoahidiwa Al-Jannah. Alisilimu mapema sana, na akamuoa Faatwimah, dada wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), na wote hawo (Faatwimah na Sa’iyd) walisababisha ‘Umar kujaaliwa na Allaah (عز وجل) kusilimu. Alipigana vita vyote isipokuwa ya Badr, kwa sababu hakuwepo kwa kuwa alikuwa akiutafuta msafara. Alifariki mnamo mwaka 51 A.H na akazikwa Al-Baqi’.
[24] Huyu Twalhah ndiye Abuu Muhammad au Abuu ‘Abdillaah Twalhah bin Muswarrif. Alikuwa Taabi’ (mfuasi au mrithi ambaye alionana na au aliongozana na Swahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) mtegemewa sana wa daraja la tano. Alikuwa ni mwenye taqwah na msomaji wa Qur-aan. Alifariki mnamo mwaka wa 112 A.H. Baba yake Muswarrif, hajulikani na hilo limeifanya Hadiyth yake kuwa dhaifu.
[25] Babu wa Twalhah anaitwa Ka’b bin ‘Amr au ‘Amr bin Ka’b bin Juhdub Al-Yami anayetokana na kabila la Yemen linaloitwa Yam la Hamadan. Ibn ‘Abdil-Bar alisema kuwa, yeye (Ka’b) alilowea kule Kufa, naye ni Swahaba.
[26] Hii inamaanisha kwamba, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitwaa maji kwa mikupuo mbalimbali kwa kuosha pua na kusukutua mdomo. Kwa mujibu wa mwandishi, Hadiyth hii ni dhaifu. Kwa mujibu wa Al-Bukhaariy na Muslim, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitumia mkono mmoja tu wa maji kwa kuosha pua na kusukutua mdomo. Imaam Nawawi ameelezea aina zake tano, na akasema hiyo iliyotajwa na Al-Bukhaariy na Muslim ndiyo Swahiyh.
[27] Hadiyth hii inaweka wazi msimamo kwamba, kuuosha mguu mzima kikamilifu ni tendo la lazima. Katika Hadiyth iliyorikodiwa na Muslim inasema kuwa, ni moto kuacha eneo la mguu likiwa kavu. Katika Hadiyth hii kuna kukana kwa watu wanaosema kuwa kupangusa (mas-h) mguu pamoja na kuuosha vyote ni lazima; au watu wanaosema kuwa kupangusa na kuosha vyote vinaruhusiwa.
[28] Mudd moja ni sawa na takribani gram mia sita, na Sai’ moja ni sawa na zaidi kidogo ya kilo mbili unusu, na hiki ndicho kiasi cha chini kabisa cha kutumia. Hii inamaanisha kuwa kila mtu awe muangalifu sana katika matumizi ya maji (bila israaf).
[29] Sai’ moja ni sawa na mudd nne au gram 2660.