Shaykh Fawzaan: Tahadhari Na Kitabu Cha Du’aa Al-Mustajaab Hakina Dalili Ni Kitabu Cha Kisufi

 

Tahadhari Na Kitabu Cha Du’aa Al-Mustajaab Hakina Dailili Ni Kitabu Cha Kisufi

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

 

“Kuna kitabu ambacho kimeenezwa sana kwa watu leo hii, na kinapatikana katika maduka ya vitabu, kinaitwa “Ad-Du’aa Al-Mustajaab” cha Muhammad ‘Abdil-Jawwaad. Ni kitabu kinachoelezea hekaya kilichokusanya du’aa za kuzushwa za Kisufi na Adhkaar ambazo zimenukuliwa bila dalili zozote kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

 

Jina la kitabu chenyewe lina maelezo ya ki ghayb kuhusu hukmu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Mwandishi  kakiita kitabu “Ad-Du’aa Al-Mustajaab (Du’aa Zenye Kujibiwa)” Je, ni nani kamjulisha huyo mwandishi kuwa du’aa hizo zinajibiwa? Ushahidi gani anao kwa hilo, zaidi tu ya kutaka kuwavutia watu ‘awwaam (wa kawaida wasio na elimu) na kuwahadaa kwa kitabu cha uzushi.

 

Nawashauri wasomaji (watafute na kuvitumia) vitabu vya du’aa na adhkaar vya kuaminika vilivyoandikwa na Wanachuoni weledi wenye kuaminika wa Ahlus-Sunnah:

 

1. Al-Waabil Asw-Swayyib cha Imaam Ibn Al-Qayyim

 

2. Al-Kalim Atw-Twayyib cha Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah

 

3. Al-Adhkaar cha Imaam An-Nawawiy

 

Vitabu hivi, havina ndani yake Adhkaar za uzushi; vimekusanya Adhkaar zilizopokelewa kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

 

Vinatosheleza na vinakidhi haja na hakuna haja ya vitabu vya masimulizi ya ngano vilivyoandikwa na wafanya mzaha.

 

[Majmuw’ Fataawa Fadhwiylat Ash-Shaykh Swaalih bin Fawzaan, (2/697)]

 

 

Share