052-Asbaabun-Nuzuwl: Al-An'aam Aayah 052: وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-An’aam: 52
06Al-An'aam: 52-Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢﴾
52. Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze ukaja kuwa miongoni mwa madhalimu. (6:52).
Sababun-Nuzuwl:
Sa’ad (رضي الله عنه) amehadithia: Tulikuwa watu sita pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na Ibn Mas’uwd alikuwa mmoja wao. Washirikina wakamwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Usiwaweke watu hawa karibu yako.” (Katika riwaayah nyingine ya Muslim): “Wafukuze.” Hapo ikateremka Aayah hii: