121-Asbaabun-Nuzuwl: Al-An'aam Aayah 121: وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Al-An’Aam 121

 

 

 

121- Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa)...

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

  

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾

Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ukiukaji wa utiifu kwa Allaah. Na hakika mashaytwaan wanawashawishi marafiki wao wandani wabishane nanyi. Na kama mtawatii basi hakika mtakuwa washirikina. [Al-An’aam (6:121)]

 

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ

Na hakika mashaytwaan wanawashawishi marafiki wao wandani. (6:121).

 

 Walikuwa washirikina wakisema: Kilichochinjwa kwa ajili ya Allaah msile! Lakini mnachochinja nyinyi basi kuleni! Hapo Allaah Akateremsha:

 

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ

Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ukiukaji wa utiifu kwa Allaah. (6:121). [Imepokelewa na Abuu Daawuwd]  

 

 

Share