066-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anfaal Aayah 066: الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Anfaal: 65-66
066- Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ ۚ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿٦٥﴾
Ee Nabiy! Shajiisha Waumini kupigana vita. Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu ishirini basi watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu mia watawashinda elfu katika wale waliokufuru, kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.
الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ﴿٦٦﴾
Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu mia watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu (Waumini) elfu, wawatashinda (makafiri) elfu mbili kwa Idhini ya Allaah. Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri. [Al-Anfaal: 65-66]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه) kwamba ilipoteremka:
إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ
Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu ishirini basi watawashinda (makafiri) mia mbili. [Al-Anfaal:65] ikawa jambo gumu kwa Waislamu kwamba mtu mmoja hapaswi kukimbia (vita) mbele ya (makafiri) kumi. Basi ikaja takhfifu pindi (Allaah) Aliposema:
الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ
Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu mia watawashinda (makafiri) mia mbili.
Basi Allaah Alipowafanyia takhfifu kwa kuwapunguzia idadi (ya maadui ambao kila mmoja wao atapambana nao), kukapungua kuhimili kwao kadiri ya walivyofanyiwa takhfifu (ya idadi ya maadui watakaopigana nao). [Al-Bukhaariy na wengineo]