067-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anfaal Aayah 067: مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

Al-Anfaal: 67- 69

067-Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٧﴾

Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno kuwaua na kuwajeruhi (maadui wa Allaah) nchini. Mnataka vitu vya dunia, na hali Allaah Anataka (mpate vya) Aakhirah. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾

Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu.

فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٦٩﴾

Basi kuleni katika ghanima mlizozipata, ni halali na ni vizuri, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Anfaal: 67-69]

Sababun-Nuzuwl: 

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtaka ushauri Abuu Bakr (رضي الله عنه)  kuhusu  mateka akamwambia: “Ni watu wako na jamaa zako waachilie.” Alipomtaka ushauri ‘Umar (رضي الله عنه) alisema: “Waue.”  Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoza fidia. Allaah (عز وجل) Akateremsha:

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٧﴾

Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno kuwaua na kuwajeruhi (maadui wa Allaah) nchini. Mnataka vitu vya dunia, na hali Allaah Anataka (mpate vya) Aakhirah. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾

Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu.

فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٦٩﴾

Basi kuleni katika ghanima mlizozipata, ni halali na ni vizuri, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Anfaal: 67-69] [Al-Haakim (2/239)]

Share