068-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anfaal Aayah 068: لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Al-Anfaal: 68

 

 

 

068- Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni..

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾

Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu. [Al-Anfaal: 68]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) :  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ghanima hazipasi kuchukuliwa na yeyote yule wa vichwa vyeusi (vichwa vyeusi imekusudiwa ni wana wa Aadam kwa vile wengi ya watu vichwa vyao ni vyeusi kutokana na nywele nyeusi), bali moto kutoka mbinguni utateremka kuzila ghanima.”  Sulaymaan Al-A’mash akasema: Hakuna asemaye haya sasa isipokuwa Abuu Hurayrah. Basi siku ya Badr pindi ghanima za vita zilipoletwa, zilifanywa halali kwao. Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾

Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu. [Al-Anfaal: 68] [At-Tirmidhiy (Abuu ‘Iysaa) amesema: Hii Hadiyth Hasan Swahiyh Ghariyb katika Hadiyth ya Al-A’mash]  

 

 

 

Share