022-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Nasaha
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النصيحة
022 – Mlango Wa Nasaha
قَالَ تَعَالَى:
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ
Hakika Waumini ni ndugu… [Al-Hujraat: 10]
وَأَنصَحُ لَكُمْ
Na nakunasihini… [Al-A’raaf: 62]
وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ ﴿٦٨﴾
Nami kwenu ni mtoaji nasiha mwaminifu. [Al-A’raaf:68]
Hadiyth – 1
عن أَبي رُقَيَّةَ تَمِيم بن أوس الداريِّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((الدِّينُ النَّصِيحةُ)) قلنا: لِمَنْ؟ قَالَ: ((لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلأئِمَّةِ المُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ)). رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Ruqayyah Tamiym ibn Aws Ad-Daariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Dini ni nasiha” Tukasema, kwanini? Akasema: “Kwa Allaah, na kitabu Chake, na Rasuli Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.” [Muslim]
Hadiyth – 2
عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: بَايَعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى إقَامِ الصَّلاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، والنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokelewa kutoka kwa Jariyr bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema kwamba: Nilimbay’ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) juu ya kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, na kumnasihi kila Muislamu. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: بَايَعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى إقَامِ الصَّلاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، والنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye kile anachopendelea nafsi yake.” [Al-Bukhariy na Muslim]