07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Sifa Ya Swalaah
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلصَّلَاةِ
Kitabu Cha Swalaah
بَابُ صِفَةِ اَلصَّلَاةِ
07-Mlango Wa Sifa Ya Swalaah
211.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِذَا قُمْتُ إِلَى اَلصَّلَاةِ فَأَسْبِغِ اَلْوُضُوءَ ، ثُمَّ اِسْتَقْبِلِ اَلْقِبْلَةَ، فَكَبِّرْ، ثُمَّ اِقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنْ اَلْقُرْآنِ ، ثُمَّ اِرْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا، ثُمَّ اِرْفَعْ حَتَّى تَعْتَدِلَ قَائِمًا، ثُمَّ اُسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ اِرْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، ثُمَّ اُسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ اِرْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، ثُمَّ اُسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ اِفْعَلْ ذَلِكَ فِي صَلَاتِكَ كُلِّهَا} أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
وَلِابْنِ مَاجَهْ بِإِسْنَادِ مُسْلِمٍ :{حَتَّى تَطْمَئِنَّ قَائِمًا}
وَمِثْلُهُ فِي حَدِيثِ رِفَاعَةَ عِنْدَ أَحْمَدَ وَابْنِ حِبَّانَ{حَتَّى تَطْمَئِنَّ قَائِمًا}
وَفِي لَفْظٍ لِأَحْمَدَ :{فَأَقِمْ صُلْبَكَ حَتَّى تَرْجِعَ اَلْعِظَامُ}
وَلِلنَّسَائِيِّ ، وَأَبِي دَاوُدَ مِنْ حَدِيثِ رِفَاعَةَ بْنِ رَافِعٍ :{إِنَّهَا لَنْ تَتِمُّ صَلَاةُ أَحَدِكُمْ حَتَّى يُسْبِغَ اَلْوُضُوءَ كَمَا أَمَرَهُ اَللَّهُ، ثُمَّ يُكَبِّرَ اَللَّهَ، وَيَحْمَدَهُ ، وَيُثْنِيَ عَلَيْهِ}
وَفِيهَا {فَإِنْ كَانَ مَعَكَ قُرْآنٌ فَاقْرَأْ وَإِلَّا فَاحْمَدِ اَللَّهَ ، وَكَبِّرْهُ ، وهلِّلْهُ}
وَلِأَبِي دَاوُدَ :{ثُمَّ اِقْرَأْ بِأُمِّ اَلْقُرْآنِ وَبِمَا شَاءَ اَللَّهُ}
وَلِابْنِ حِبَّانَ :{ثُمَّ بِمَا شِئْتَ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ukisimama kuswali, tawadha vizuri na kikamilifu, kisha elekea Qiblah, na piga takbiyra kisha soma unachoweza katika Qur-aan[1], kisha rukuu hadi utulie ukiwa katika rakaa, kisha inuka na usimame wima, kisha sujudu hadi utulie ukiwa katika sajdah, kisha inuka na utulie ukiwa umeketi[2], kisha sujudu tena na utulie katika sajdah, kisha ufanye vivyo hivyo katika Swalaah yako yote.” [Imetolewa na As-Sab’ah (Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Pia ni tamshi la Ibn Maajah kwa Isnaad ya Muslim: “Mpaka utulie ukiwa umesimama wima.”
Hadiyth ya Rifaa’ah[3] iliyoko kwa Ahmad na Ibn Hibbaan: “Mpaka utulie hali ya kuwa umesimama.”
Naye Ahmad amesema: “Unyooshe mgongo wako hadi mifupa irejee nafasi zake.”
Nao An-Nasaaiy na Abuu Daawuwd wamepokea Hadiyth ya Rifaa’ah bin Raafi’ inasema: “Swalaah ya mmoja wenu haitatimia hadi atawadhe sawasawa kama Allaah Alivyoamrisha, kisha apige takbiyra na amhimidi na kumsifu Yeye.”
Pia inatajwa katika Hadiyth hiyo kuwa: “Ukiwa unajua sehemu yoyote ya Qur-aan, isome, vinginevyo mhimidi Allaah (AlhamduliLLaah), mpigie takbiyra (Allaahu Akbar) na mpwekeshe kwa tahliyl (laa ilaaha illa-Allaah).”
Na Abuu Daawuwd amesema: “Kisha soma Ummul-Qur-aan[4] (Suwrah Al-Faatihah) na kisha kila Atakacho Allaah.”
Na Ibn Hibbaan akasema: “na (usome) chochote unachotaka”
212.
وَعَنْ أَبِي حُمَيْدٍ اَلسَّاعِدِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {رَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم إِذَا كَبَّرَ جَعَلَ يَدَيْهِ حَذْوَ مَنْكِبَيْهِ ، وَإِذَا رَكَعَ أَمْكَنَ يَدَيْهِ مِنْ رُكْبَتَيْهِ ، ثُمَّ هَصَرَ ظَهْرِهِ ، فَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ اِسْتَوَى حَتَّى يَعُودَ كُلُّ فَقَارٍ مَكَانَهُ ، فَإِذَا سَجَدَ وَضَعَ يَدَيْهِ غَيْرَ مُفْتَرِشٍ وَلَا قَابِضِهِمَا ، وَاسْتَقْبَلَ بِأَطْرَافِ أَصَابِعِ رِجْلَيْهِ اَلْقِبْلَةَ ، وَإِذَا جَلَسَ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ جَلَسَ عَلَى رِجْلِهِ اَلْيُسْرَى وَنَصَبَ اَلْيُمْنَى ، وَإِذَا جَلَسَ فِي اَلرَّكْعَةِ اَلْأَخِيرَةِ قَدَّمَ رِجْلَهُ اَلْيُسْرَى وَنَصَبَ اَلْأُخْرَى ، وَقَعَدَ عَلَى مَقْعَدَتِهِ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Humayd As-Saa’idiyy[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemuona Nabiy[6] (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akipiga Takbiyra aliweka mikono yake sambamba na mabega yake[7], na aliporukuu aliweka mikono yake kwenye magoti, na alikunja mgongo wake, alipoinuka alisimama wima hadi mifupa ya uti wa mgongo ikarejea mahali pake, aliposujudu, aliiweka mikono yake bila kuisambaza wala kuifumba; na ncha za vidole vyake vya miguu vikawa vinaelekea Qiblah, alipoketi katika rakaa mbili, alikalia mguu wake wa kushoto na kusimamisha wa kuume, na alipoketi katika rakaa ya mwisho alitanguliza mbele mguu wake wa kushoto na akasimamisha wa kuume na akakalia makalio yake.“ [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
213.
وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ كَانَ إِذَا قَامَ إِلَى اَلصَّلَاةِ قَالَ : "وَجَّهْتُ وَجْهِي لِلَّذِي فَطَّرَ اَلسَّمَوَاتِ " . . . إِلَى قَوْلِهِ : "مِنْ اَلْمُسْلِمِينَ ، اَللَّهُمَّ أَنْتَ اَلْمَلِكُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ ، أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ . . .} إِلَى آخِرِهِ . رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ : أَنَّ ذَلِكَ فِي صَلَاةِ اَللَّيْلِ
Kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akisimama kuswali, alikuwa akisema[8]: “Wajjahtu wajhiya li-LLadhiy fatwaras-samaawaati…” mpaka: “minal muslimiyna. Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illaa Anta, Anta Rabbiy wa anaa ‘abduka” mpaka mwisho wake. (Nimeelekeza uso wangu kwa Aliyeumba mbingu na ardhi”, hadi kauli yake: “miongoni mwa Waislamu. Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe ni Rabb wangu na mimi ni mja wako[9]).” [Imetolewa na Muslim]
Na katika mapokezi yake (Muslim) mengine: “Hayo ni katika Swalaah ya usiku.”
214.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا كَبَّرَ لِلصَّلَاةِ سَكَتَ هُنَيَّةً ، قَبْلِ أَنْ يَقْرَأَ ، فَسَأَلْتُهُ ، فَقَالَ : "أَقُولُ : اَللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ اَلْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اَللَّهُمَّ نقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى اَلثَّوْبُ اَلْأَبْيَضُ مِنْ اَلدَّنَسِ ، اَللَّهُمَّ اِغْسِلْنِي مِنْ خَطَايَايَ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akishasoma Takbiyra ya Swalaah alinyamaza kidogo kabla ya kusoma Qur-aan. Nikamuuliza juu ya hilo, akasema: Nasema:
“Allaahumma baa’id bayniy wa bayna khatwaayaaya kamaa baa’adta baynal-Mashriqi wal-Maghrib. Allaahumma naqqiniy min khatwaayaaya kamaa yunaqqath-thawbul abyadhwu minad-danasi. Allaahumma-ghsiliniy min khatwaayaaya bil-maai wath-thalji wal-barad.”
(Ee Allaah niweke mbali na makosa yangu kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi, Ee Allaah nisafishe makosa yangu kama vile inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu, Ee Allaah nisafishe makosa yangu kwa maji na theluji na barafu). [Al-Bukhaariy, Muslim]
215.
وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ : {سُبْحَانَكَ اَللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ ، تَبَارَكَ اِسْمُكَ ، وَتَعَالَى جَدُّكَ ، وَلَا إِلَه غَيْرُكَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ بِسَنَدٍ مُنْقَطِعٍ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ مَوْصُولاً وَهُوَ مَوْقُوفٌ
وَنَحْوُهُ عَنْ أَبِي سَعِيدٍ مَرْفُوعًا عِنْدَ اَلْخَمْسَةِ
وَفِيهِ : وَكَانَ يَقُولُ بَعْدَ اَلتَّكْبِيرِ : {أَعُوذُ بِاَللَّهِ اَلسَّمِيعِ اَلْعَلِيمِ مِنَ اَلشَّيْطَانِ اَلرَّجِيمِ ، مِنْ هَمْزِهِ ، وَنَفْخِهِ ، وَنَفْثِهِ }
Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema:
”Subhaanaka-LLaahumma wabihamdika wa Tabaarakas-Smuka wa Ta’aalaa Jadduka walaa ilaaha Ghayruka.”
(Utakasifu ni Wako Ee Allaah, na Himdi ni Zako, na Limebarikika Jina Lako, na Utukufu Wako uko juu, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako) [Imetolewa na Muslim kwa Isnaad iliyo Munqatwi’ (iliyokatika). Na katika Riwaayah ya Ad-Daaraqutwniy ina Isnaad Mawsuwl na Mawquwf]
Hadiyth kama hiyo ameisimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy ambayo ni Marfuw’ kwa Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) imesema: “(Nabiy) alikuwa akisema baada ya Takbiyra:
”‘Auwdhu biLLaahis-Samiy’il ‘Aliymi mina-sh-shaytwaanir-rajiym min hamzihi wa nafkhihi, wa nafthihi.”
(Najilindia na Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa na kulaaniwa, najilinda na kutokana na wazimu wake au ushauri wake muovu, na upulizaji wake, na kutabana kwake au uchawi wake).
216.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ :{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَسْتَفْتِحُ اَلصَّلَاةَ بِالتَّكْبِيرِ ، وَالْقِرَاءَةَ : بِـ (اَلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ اَلْعَالَمِينَ ) وَكَانَ إِذَا رَكَعَ لَمْ يُشْخِصْ رَأْسَهُ ، وَلَمْ يُصَوِّبْهُ ، وَلَكِنْ بَيْنَ ذَلِكَ . وَكَانَ إِذَا رَفَعَ مِنْ اَلرُّكُوعِ لَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَائِمًا . وَإِذَا رَفَعَ مِنْ اَلسُّجُودِ لَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَسْتَوِيَ جَالِسًا . وَكَانَ يَقُولُ فِي كُلِّ رَكْعَتَيْنِ اَلتَّحِيَّةَ . وَكَانَ يَفْرِشُ رِجْلَهُ اَلْيُسْرَى وَيَنْصِبُ اَلْيُمْنَى . وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقْبَةِ اَلشَّيْطَانِ ، وَيَنْهَى أَنْ يَفْتَرِشَ اَلرَّجُلُ زِرَاعَيْهِ اِفْتِرَاشَ اَلسَّبُعِ . وَكَانَ يُخْتَمُ اَلصَّلَاةَ بِالتَّسْلِيمِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ ، وَلَهُ عِلَّةٌ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akianza Swalaah kwa Takbiyra na kusoma:
“AlhamduliLlaahi Rabbil ‘Aalamiyn[10]
Na aliporukuuu, hakuinua kichwa chake wala hakiinamishi, bali alikiweka baina ya sehemu hizi mbili. Alipoinua kichwa chake kutoka katika kurukuu, hakusujudu hadi aliposimama wima, na alipoinua kichwa chake baada ya kusujudu, hakurudia kusujudu mpaka alipoinuka na kuketi kitako, alikuwa akisoma katika Rakaa mbili At-Tahiyyah. Na alikuwa akitandika mguu wake wa kushoto na kuusimamisha wima wa kuume; na alikuwa alikataza mkao wa shaytwaan wa kukalia[11] makalio, na akakataza watu kutandika mikono yao kama wanyama, na alikuwa akikhitimisha Swalaah kwa tasliym (Assalaamu ‘alaykum).” [Imetolewa na Muslim, na ina dosari]
217.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَرْفَعُ يَدَيْهِ حَذْوَ مَنْكِبَيْهِ إِذَا اِفْتَتَحَ اَلصَّلَاةَ، وَإِذَا كَبَّرَ لِلرُّكُوعِ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنْ اَلرُّكُوعِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي حَدِيثِ أَبِي حُمَيْدٍ، عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ: {يَرْفَعُ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِيَ بِهِمَا مَنْكِبَيْهِ، ثُمَّ يُكَبِّرَ}
وَلِمُسْلِمٍ عَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ نَحْوُ حَدِيثِ اِبْنِ عُمَرَ ، وَلَكِنْ قَالَ : {حَتَّى يُحَاذِيَ بِهِمَا فُرُوعَ أُذُنَيْهِ}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega[12] yake, anapoanza Swalaah, na anapopiga Takbiyra kwa ajili ya kurukuu, na aliponyanya kichwa chake baada ya kurukuu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Hadiyth aliyopokea Abuu Daawuwd kutoka kwa Abuu Humayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “(Nabiy) alikuwa akinyanyua mikono yake na kuiweka sambamba na mabega yake, kisha anapiga takbiyra.”
Katika Hadiyth ya Muslim iliyosimuliwa na Maalik bin Al-Huwayrith (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ni sawa sawa kama Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) lakini yeye (Maalik bin Al-Huwayrith) alitaja kuwa: “Nabiy alikuwa akinyanyua mikono yake sambamba na mwisho wa masikio yake.”
218.
وَعَنْ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَوَضَعَ يَدَهُ اَلْيُمْنَى عَلَى يَدِهِ اَلْيُسْرَى عَلَى صَدْرِهِ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa Waail bin Hujr[13] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mimi niliswali na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) naye aliweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, na kisha akaiweka juu ya kifua[14] chake.” [Imetolewa na Ibn Khuzaymah]
219.
وَعَنْ عُبَادَةَ بْنِ اَلصَّامِتِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَا صَلَاةَ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِأُمِّ اَلْقُرْآنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ ، لِابْنِ حِبَّانَ وَاَلدَّارَقُطْنِيِّ :{لَا تَجْزِي صَلَاةٌ لَا يُقْرَأُ فِيهَا بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ}
وَفِي أُخْرَى ، لِأَحْمَدَ وَأَبِي دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيِّ ، وَابْنِ حِبَّانَ:{لَعَلَّكُمْ تَقْرَءُونَ خَلْفَ إِمَامِكُمْ ؟ " قُلْنَا : نِعْمَ . قَالَ : "لَا تَفْعَلُوا إِلَّا بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ ، فَإِنَّهُ لَا صَلَاةِ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِهَا}
Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit[15] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Swalaah kwa mtu asiyesoma Ummul-Qur-aan (Suwrah Al-Faatihah)[16].” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Ibn Hibbaan na Ad-Daaraqutwniy: “Haijuzu Swalaah isiyosomwa ndani yake Suwrah Al-Faatihah.”
Na Riwaayah nyingine ya Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan: “Huenda mnasoma nyuma ya Imaam wenu? Tukasema: “Ndiyo.” Akasema: “Msifanye hivyo, isipokuwa kwa Suwrah Al-Faatihah kwani hana Swalaah asiyeisoma.”
220.
وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَأَبَا بَكْرٍ وَعُمَرَ كَانُوا يَفْتَتِحُونَ اَلصَّلَاةِ بِـ (اَلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ اَلْعَالَمِينَ)} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
زَادَ مُسْلِمٌ: {لَا يَذْكُرُونَ : (بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ ) فِي أَوَّلِ قِرَاءَةٍ وَلَا فِي آخِرِهَا}
وَفِي رِوَايَةٍ لِأَحْمَدَ ، وَالنَّسَائِيِّ وَابْنِ خُزَيْمَةَ :{لَا يَجْهَرُونَ بِبِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ}
وَفِي أُخْرَى لِابْنِ خُزَيْمَةَ :{كَانُوا يُسِرُّونَ}
وَعَلَى هَذَا يُحْمَلُ اَلنَّفْيُ فِي رِوَايَةِ مُسْلِمٍ ، خِلَافًا لِمَنْ أَعَلَّهَا
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) walikuwa wakianza Swalaah kwa: “AlhamduliLLaahi Rabbil ‘Aalamiyn.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na Muslim aliongezea: “Walikuwa hawasomi “BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym” mwanzoni, wala mwishoni wake.[17]”
Na katika Riwaayah ya Ahmad, An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah: “Hawadhihirishi BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym kwa sauti.”
Na katika Riwaayah ya Ibn Khuzaymah: “Walikuwa wanasoma (BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym)[18]”
Na juu ya hili katika Riwaayah ya Muslim, tofauti na wenye kuitia dosari.
221.
نُعَيْمٍ اَلْمُجَمِّرِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {صَلَّيْتُ وَرَاءَ أَبِي هُرَيْرَةَ فَقَرَأَ : (بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ) . ثُمَّ قَرَأَ بِأُمِّ اَلْقُرْآنِ ، حَتَّى إِذَا بَلَغَ : (وَلَا اَلضَّالِّينَ) ، قَالَ : "آمِينَ" وَيَقُولُ كُلَّمَا سَجَدَ ، وَإِذَا قَامَ مِنْ اَلْجُلُوسِ : اَللَّهُ أَكْبَرُ . ثُمَّ يَقُولُ إِذَا سَلَّمَ : وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنِّي لَأَشْبَهُكُمْ صَلَاةً بِرَسُولِ اَللَّهِ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَابْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa Nu’aym Al-Mujammir[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Niliswali nyuma ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisoma: “BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym”, kisha Ummul-Qur-aan (Al-Faatihah), alipofika: “Waladhw-dhwaalliyna” alisema: “Aamiyn.”[20] Akawa anasema: “Allaahu Akbar” kila aliposujudu na alipoinuka na kusimama kutoka katika Sijdah, na alipotoa salaam yaani kusema: “Assalaam ‘alaykum” alisema: “Ninaapa kwa Ambaye roho yangu iko Mkononi Mwake, Swalaah yangu inafanana sana na ile ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuliko yeyote miongoni mwenu.” [Imetolewa na An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah]
222.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا قَرَأْتُمْ اَلْفَاتِحَةِ فَاقْرَءُوا : ( بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ ) ، فَإِنَّهَا إِحْدَى آيَاتِهَا} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ ، وَصَوَّبَ وَقْفَهُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnaposoma Suwrah Al-Faatihah someni “BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym”, kwani hiyo ni moja ya Aayah zake.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy, aliyeipa daraja la Mawquwf]
223.
وَعَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا فَرَغَ مِنْ قِرَاءَةِ أُمِّ اَلْقُرْآنِ رَفَعَ صَوْتَهُ وَقَالَ: "آمِينَ".} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَحَسَّنَهُ ، وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ
ـ وَلِأَبِي دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيِّ مِنْ حَدِيثِ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ نَحْوُهُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipomaliza kusoma Ummul-Qur-aan alipaza sauti yake na kusema “Aaamiyn.”[21] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy, aliyeipa daraja la Hasan, na akaisahihisha Al-Haakim]
Na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy wamepokea masimulizi ya Waail bin Hujri mfano wake.
224.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : {جَاءَ رَجُلٌ إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : إِنِّي لَا أَسْتَطِيعُ أَنْ آخُذَ مِنْ اَلْقُرْآنِ شَيْئًا ، فَعَلِّمْنِي مَا يُجْزِئُنِيٌ مِنْهُ . قَالَ : "سُبْحَانَ اَللَّهِ ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَاَللَّهُ أَكْبَرُ ، وَلَا حَوْلٌ وَلَا قُوَّةً إِلَّا بِاَللَّهِ اَلْعَلِيِّ اَلْعَظِيمِ . . .} اَلْحَدِيثَ . رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَالْحَاكِمُ .
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa[22] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Mimi siwezi kuhifadhi chochote katika Qur-aan, kwa hivyo nifundishe kitakachonitosha humo, akasema: Sema:
“Subhaana-Allaah, (Utakasifu ni wa Allaah), “Wal-Hamdu liLLaah (Himdi ni za Allaah) wa laa ilaaha illa Allaah (na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah) wa-Allaahu Akbar (na Allaah ni Mkubwa Zaidi), wa laa hawla wa laa quwwata illa biLLaahil-‘Aliyyil-‘Adhwiym (na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allaah Aliyetukuka Aliye ‘Adhimu).[23]” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan, Ad-Daaraqutwniy na Al-Haakim]
225.
وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي بِنَا ، فَيَقْرَأُ فِي اَلظُّهْرِ وَالْعَصْرِ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ اَلْأُولَيَيْنِ بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ وَسُورَتَيْنِ ، وَيُسْمِعُنَا اَلْآيَةَ أَحْيَانًا ، وَيُطَوِّلُ اَلرَّكْعَةَ اَلْأُولَى ، وَيَقْرَأُ فِي اَلْأُخْرَيَيْنِ بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ.} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akituswalisha anasoma katika Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri, Suwrah Al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwanzo, pamoja na Suwrah zingine mbili, na mara nyingine alitusikilizisha Aayah[24], alikuwa akiirefusha Rakaa ya mwanzo, na alikuwa akisoma Suwrah Al-Faatihah tu katika Rakaa mbili za mwisho.[25]” [Al-Bukhaariy, Muslim]
226.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كُنَّا نَحْزُرُ قِيَامَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي اَلظُّهْرِ وَالْعَصْرِ ، فَحَزَرْنَا قِيَامَهُ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ اَلْأُولَيَيْنِ مِنْ اَلظُّهْرِ قَدْرَ : (الم تَنْزِيلُ) اَلسَّجْدَةِ . وَفِي اَلْأُخْرَيَيْنِ قَدْرَ اَلنِّصْفِ مِنْ ذَلِكَ . وَفِي اَلْأُولَيَيْنِ مِنْ اَلْعَصْرِ عَلَى قَدْرِ اَلْأُخْرَيَيْنِ مِنْ اَلظُّهْرِ ، وَالْأُخْرَيَيْنِ عَلَى اَلنِّصْفِ مِنْ ذَلِكَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa tukikisia urefu wa kisimamo cha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika Swalaah za Adhuhuri na Alasiri na tukapata ni kadiri ya kusoma Suwrah ya “Alif Laam Miym Tanziyl” (Suwrah As-Sajdah)[26], na katika Rakaa za mwisho mbili kadiri ya nusu ya hivyo, na katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalaah ya Alasiri, alikuwa akisimama kwa muda kadiri ya Rakaa mbili za Swalaah ya Adhuhuri, na Rakaa mbili za mwisho kadiri ya nusu ya urefu wa Rakaa mbili za mwanzo.” [Imetolewa na Muslim]
227.
وَعَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ فُلَانٍ يُطِيلُ اَلْأُولَيَيْنِ مِنْ اَلظُّهْرِ، وَيُخَفِّفُ اَلْعَصْرَ، وَيَقْرَأُ فِي اَلْمَغْرِبِ بِقِصَارِ اَلْمُفَصَّلِ وَفِي اَلْعِشَاءِ بِوَسَطِهِ وَفِي اَلصُّبْحِ بِطُولِهِ . فَقَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: "مَا صَلَّيْتُ وَرَاءِ أَحَدٍ أَشْبَهَ صَلَاةِ بِرَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنْ هَذَا} أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ
Kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar[27] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Fulani alikuwa akirefusha Rakaa mbili za mwanzo za Swalaah ya Adhuhuri, na akifupisha Alasiri na akisoma Suwrah fupi ya Mufasw-swal[28] wakati wa Swalaah ya Magharibi, na Suwrah za wastani kwa Swalaah ya ‘Ishaa, na Suwrah ndefu wakati wa Alfajiri.” Kisha Abuu Hurayrah akasema: “Sijaswali nyuma ya yeyote ambaye Swalaah yake inafanana zaidi na Swalaah ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuliko huyu.” [Imetolewa na An-Nasaaiy kwa Isnaad Swahiyh]
228.
وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي اَلْمَغْرِبِ بِالطُّورِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisoma Suwrah “Atw-Twuwr” katika Swalaah ya Magharibi.[29]” [Al-Bukhaariy, Muslim]
229.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي صَلَاةِ اَلْفَجْرِ يَوْمَ اَلْجُمْعَةِ : (الم تَنْزِيلُ ) اَلسَّجْدَةَ ، و (هَلْ أَتَى عَلَى اَلْإِنْسَانِ)} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِلطَّبَرَانِيِّ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ مَسْعُودٍ :{يُدِيمُ ذَلِكَ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Alfajiri siku ya Ijumaa “Alif-Laam-Miym Tanziyl...” (As-Sajdah) na “Hal ataa ‘alal Insaani” (ambayo pia huitwa Suwrah Ad-Dahr)?[30]” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Atw-Twabaraaniyy imepokea Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd ikiwa na nyongeza kuwa: “Rasuli akidumisha hivyo.[31]”
230.
وَعَنْ حُذَيْفَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَمَا مَرَّتْ بِهِ آيَةُ رَحْمَةٍ إِلَّا وَقَفَ عِنْدَهَا يَسْأَلُ، وَلَا آيَةُ عَذَابٍ إِلَّا تَعَوَّذَ مِنْهَا} أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
Kutoka kwa Hudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimeswali pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na hakuipita Aayah ya Rahmah ila alisimama hapo na kuomba (Rahmah), wala Aayah ya adhabu ila aliomba kinga nayo (adhabu hiyo).” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaipa daraja la Hasan At-Tirmidhiy]
231.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَلَا وَإِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَقْرَأَ اَلْقُرْآنَ رَاكِعًا أَوْ سَاجِدًا ، فَأَمَّا اَلرُّكُوعُ فَعَظِّمُوا فِيهِ اَلرَّبَّ ، وَأَمَّا اَلسُّجُودُ فَاجْتَهِدُوا فِي اَلدُّعَاءِ ، فَقَمِنٌ أَنْ يُسْتَجَابَ لَكُمْ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jueni nimekatazwa kusoma Qur-aan[32] nikiwa nimerukuu au nimesujudu, ama katika kurukuu Muadhimisheni humo Rabb, na wakati wa kusujudu jitahidini kuomba du’aa, kwani hakika mtajibiwa.” [Imetolewa na Muslim]
232.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: فِي رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ : "سُبْحَانَكَ اَللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ ، اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasema wakati wa kurukuu na kusujudu:
“Subhaanaka-Allaahumma Rabbanaa wa bi-Hamdika, Allaahummagh-firliy”
(Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, Rabb wetu, na kuhimidiwa ni Kwako, ee Allaah nighufirie).” [Al-Bukhaariy, Muslim]
233.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا قَامَ إِلَى اَلصَّلَاةِ يُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْكَعُ ، ثُمَّ يَقُولُ : "سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ" حِينَ يَرْفَعُ صُلْبَهُ مِنْ اَلرُّكُوعِ ، ثُمَّ يَقُولُ وَهُوَ قَائِمٌ : "رَبَّنَا وَلَكَ اَلْحَمْدُ" ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَهْوِي سَاجِدًا ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَسْجُدُ ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ ، ثُمَّ يَفْعَلُ ذَلِكَ فِي اَلصَّلَاةِ كُلِّهَا ، وَيُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ مِنْ اِثْنَتَيْنِ بَعْدَ اَلْجُلُوسِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anaposimama kuswali, alikuwa anapiga Takbiyra[33] ilhali amesimama wima, kisha anatamka Takbiyra wakati akirukuu, kisha anasema:
“Sami’a-Allaahu liman Hamidah.”
(Allaah Amemsikia mwenye kumhimidi).
Wakati anainua mgongo wake kutoka katika rukuu akishasimama wima (I’tidaal) anasema:
“Rabbanaa wa-Lakal Hamd.”
(Rabb wetu kuhimidiwa ni kwako).
Kisha anapiga Takbiyra anapoinama kwa ajili ya kusujudu, kisha anapiga takbiyra anapoinua kichwa, kisha anapiga takbiyra anaposujudu mara ya pili, kisha anapiga takbiyra anapoinua kichwa mara nyingine. Na alifanya hivyo hivyo katika Swalaah yote. Na alipiga takbiyra aliposimama toka katika kikao, baada ya Rakaa mbili.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
234.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ :{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنْ اَلرُّكُوعِ قَالَ : " اَللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ مِلْءَ اَلسَّمَوَاتِ وَمِلْءَ اَلْأَرْضِ ، وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ ، أَهْلَ اَلثَّنَاءِ وَالْمَجْدِ ، أَحَقُّ مَا قَالَ اَلْعَبْدُ وَكُلُّنَا لَكَ عَبْدٌ اَللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا اَلْجَدِّ مِنْكَ اَلْجَدُّ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anapoinua kichwa chake baada ya rukuu alikuwa anasema:
“Allaahumma Rabbanaa Lakal-Hamd, mil-as-samawaati wal-ardhwi, wa mil-a maa Shii-ta min shay-in ba’du, ahlath-thanaai wal-Majdi, ahaqqu maa qaalal-‘abdu, wa kullunaa Laka ‘abdu, Allaahumma laa maani’a limaa A’twayta, wa laa mu’twiya limaa Mana’ta, wa laa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu.”
(Ee Allaah! Rabb wetu, Himdi ni Zako, ujazo wa mbingu na ardhi, na ujazo wa chochote Ulichotaka (kuumba) baadaye. Ee Mwenye Sifa na Utukufu, Mwenye kustahiki kuliko vyote kwa kila alilolisema mja Wako, Ee Allaah hakuna mwenye kuzuia Ulichotoa, au kutoa Ulichozuia, wala mali[34] haziwezi kumnufaisha tajiri Kwako).[35]” [Imetolewa na Muslim]
235.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أُمِرْتُ أَنْ أَسْجُدَ عَلَى سَبْعَةِ أَعْظُمٍ : عَلَى اَلْجَبْهَةِ وَأَشَارَ بِيَدِهِ إِلَى أَنْفِهِ وَالْيَدَيْنِ ، وَالرُّكْبَتَيْنِ ، وَأَطْرَافِ اَلْقَدَمَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nimeamrishwa kusujudu juu ya mifupa saba: paji la uso, akaashiria kwa mikono yake miwili juu ya pua yake[36], magoti mawili na vidole vya miguu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
236.
وَعَنْ اِبْنِ بُحَيْنَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {كَانَ إِذَا صَلَّى فَرَّجَ بَيْنَ يَدَيْهِ ، حَتَّى يَبْدُوَ بَيَاضُ إِبِطَيْهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn Buhaynah[37] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisujudu anaposwali, hupanua mikono yake hadi weupe wa kwapa zake ukaonekana.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
237.
وَعَنْ اَلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا سَجَدْتَ فَضَعْ كَفَّيْكَ ، وَارْفَعْ مِرْفَقَيْكَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Al-Baraai bin ‘Aazib[38] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Unaposujudu, weka viganja vya mikono yako juu ya ardhi na unyanyue viwiko vyako.” [Imetolewa na Muslim]
238.
وَعَنْ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {كَانَ إِذَا رَكَعَ فَرَّجَ بَيْنَ أَصَابِعِهِ، وَإِذَا سَجَدَ ضَمَّ أَصَابِعَهُ} رَوَاهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Waail bin Hujr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alipokuwa akirukuu anapanua vidole vyake, anaposujudu alivikusanya.” [Imetolewa na Al-Haakim]
239.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : {رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي مُتَرَبِّعًا} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali akiwa amekaa huku kakunja miguu.[39]” [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]
240.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ بَيْنَ اَلسَّجْدَتَيْنِ : {اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي ، وَاهْدِنِي، وَعَافِنِي، وَارْزُقْنِي} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ إِلَّا النَّسَائِيُّ ، وَاللَّفْظُ لِأَبِي دَاوُدَ ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasoma baina ya Sijda mbili:
“Allaahummagh-fir-liy Warhamniy, Wahdiniy, Wa’aafiniy, Warzuqniy.”
(Ee Allaah! Nighufirie, Nirehemu, Nihidi, Nijaalie ‘Aafiyah (siha, amani nk.) na Niruzuku).” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, na tamshi hili ni la Abuu Daawuwd, na aliisahihisha Al-Haakim
241.
وَعَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ {رَأَى اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي ، فَإِذَا كَانَ فِي وِتْرٍ مِنْ صَلَاتِهِ لَمْ يَنْهَضْ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَاعِدًا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Maalik bin Al-Huwayrith (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali, na alipokuwa katika Rakaa za Swalaah ya Witr, hakusimama wima hadi alipokaa chini sawasawa.”[40] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
242.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ قَنَتَ شَهْرًا بَعْدَ اَلرُّكُوعِ ، يَدْعُو عَلَى أَحْيَاءٍ مِنْ أَحْيَاءِ اَلْعَرَبِ ، ثُمَّ تَرَكَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِأَحْمَدَ وَاَلدَّارَقُطْنِيِّ نَحْوُهُ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ ، وَزَادَ :{فَأَمَّا فِي اَلصُّبْحِ فَلَمْ يَزَلْ يَقْنُتُ حَتَّى فَارَقَ اَلدُّنْيَا}
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisoma Qunuwt mwezi mmoja, baada ya kurukuu, akilaani makabila fulani ya Waarabu[41], kisha akaiacha.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Katika Riwaayah ya Ahmad na Ad-Daaraqutwniyy kuna Hadiyth kama hiyo kwa njia nyingine, na kuna ziada hii: “Ama katika Alfajiri aliendelea kusoma Qunuwt mpaka alipoaga dunia.”
243.
وَعَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم{ كَانَ لَا يَقْنُتُ إِلَّا إِذَا دَعَا لِقَوْمٍ ، أَوْ دَعَا عَلَى قَوْمٍ} صَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakutekeleza Qunuwt isipokuwa alipokuwa akiomba du’aa dhidi ya watu[42] baada ya kuinuka kutoka katika rukuu isipokuwa alipowaombea watu, au kuwalaani watu.” [Aliisahihisha Ibn Khuzaymah]
244.
وَعَنْ سَعْدِ بْنِ طَارِقِ الْأَشْجَعِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ :{قُلْتُ لِأَبِي : يَا أَبَتِ ! إِنَّكَ قَدْ صَلَّيْتُ خَلْفَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبِي بَكْرٍ ، وَعُمَرُ ، وَعُثْمَانُ ، وَعَلَيَّ ، أَفَكَانُوا يَقْنُتُونَ فِي اَلْفَجْرِ ؟ قَالَ : أَيْ بُنَيَّ ، مُحْدَثٌ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ ، إِلَّا أَبَا دَاوُدَ
Kutoka kwa Sa’d[43] bin Twaariq[44] Al-Ashja’iyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nilimuuliza baba yangu: Ee baba yangu! Wewe umeswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan na ‘Aliy, Je walikuwa wakifanya Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri? Akasema: Ee mwanangu! Huo ni uzushi.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa Abuu Daawuwd]
245.
وَعَنْ اَلْحَسَنِ بْنِ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ; قَالَ :{عَلَّمَنِي رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَلِمَاتٍ أَقُولُهُنَّ فِي قُنُوتِ اَلْوِتْرِ : "اَللَّهُمَّ اِهْدِنِي فِيمَنْ هَدَيْتَ ، وَعَافِنِي فِيمَنْ عَافَيْتَ ، وَتَوَلَّنِي فِيمَنْ تَوَلَّيْتَ ، وَبَارِكْ لِي فِيمَا أَعْطَيْتَ ، وَقِنِي شَرَّ مَا قَضَيْتَ ، فَإِنَّكَ تَقْضِي وَلَا يُقْضَى عَلَيْكَ ، إِنَّهُ لَا يَذِلُّ مَنْ وَالَيْتَ ، تَبَارَكْتَ رَبَّنَا وَتَعَالَيْتَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ . وَزَادَ اَلطَّبَرَانِيُّ وَالْبَيْهَقِيُّ :{وَلَا يَعِزُّ مَنْ عَادَيْتَ} زَادَ النَّسَائِيُّ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ فِي آخِرِهِ :{وَصَلَّى اَللَّهُ عَلَى اَلنَّبِيِّ}
وَلِلْبَيْهَقِيِّ عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا :{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا دُعَاءً نَدْعُو بِهِ فِي اَلْقُنُوتِ مِنْ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ} وَفِي سَنَدِهِ ضَعْفٌ
Kutoka kwa Al-Hasan bin ‘Aliy[45] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alinifundisha maneno ya kusema katika Qunuwt ya Swalaah ya Witr:
“Allaahumma-hdniy fiyman Hadayta, wa-‘Aafiniy fiyman ‘Aafayta, wa-Tawallaniy fiyman Tawallayta, wa-Baarik liy fiymaa A’twayta, wa-Qiniy sharra maa Qadhwayta, fa-Innaka Taqdhwiy walaa yuqdhwaa ‘Alayka, innahu laa yadhillu man Waalayta, Tabaarakta Rabbanaa wa-Ta’aalayta.”
(Ee Allaah! Nihidi pamoja na Uliowahidi, na Unipe ’aafiyah pamoja na Uliowapa ’aafiyah, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya wapenzi Wako, na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi, Umebarikika Ee Rabb wetu na Umetukuka) [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad)]
Atw-Twabaraaniyy na Al-Bayhaqiyy wakaongeza:
“Wa laa ya’izzu man ‘aadayta.”
(Wala hana ’izzah (hadhi) Unayemfanya adui).
Katika Riwaayah iliyopokewa na An-Nasaaiy aliongezea:
“Wa Swalla Allaahu ‘alan-Nabiyy.”
(na Allaah Amaswalie Nabiy).[46]
Na Bayhaqiyy amepokea kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anatufundisha du’aa tunaiomba katika Qunuwt ya Swalaah ya asubuhi.” Katika Isnaad yake kuna udhaifu.
246.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا سَجَدَ أَحَدُكُمْ فَلَا يَبْرُكْ كَمَا يَبْرُكُ اَلْبَعِيرُ، وَلْيَضَعْ يَدَيْهِ قَبْلَ رُكْبَتَيْهِ} أَخْرَجَهُ اَلثَّلَاثَةُ
وَهُوَ أَقْوَى مِنْ حَدِيثِ وَائِلٍ :{رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا سَجَدَ وَضَعَ رُكْبَتَيْهِ قَبْلَ يَدَيْهِ} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ
فَإِنْ لِلْأَوَّلِ شَاهِدًا مِنْ حَدِيثِ :اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا صَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ ، وَذَكَرَهُ اَلْبُخَارِيُّ مُعَلَّقًا مَوْقُوفًا
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu anaposujudu, asipige magoti kama afanyavyo ngamia, bali aweke viganja vyake chini kabla ya kuweka magoti yake.” [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd)]
Nayo ina nguvu (kwa usahihi) zaidi[47] kuliko Hadiyth ya Waail bin Hujr: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiweka magoti yake chini kabla ya kuweka viganja vyake akisujudu.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]
Hadiyth ya kwanza inashuhudiwa na Hadiyth ya Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) (inayofuata chini), ambayo Ibn Khuzaymah amesema ni Swahiyh, Al-Bukhaariy aliitaja kuwa ni Mu’allaq Mawquwf.
247.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَعَدَ لِلتَّشَهُّدِ وَضَعَ يَدَهُ اَلْيُسْرَى عَلَى رُكْبَتِهِ اَلْيُسْرَى ، وَالْيُمْنَى عَلَى اَلْيُمْنَى ، وَعَقَدَ ثَلَاثَةً وَخَمْسِينَ ، وَأَشَارَ بِإِصْبَعِهِ اَلسَّبَّابَةِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ :{وَقَبَضَ أَصَابِعَهُ كُلَّهَا ، وَأَشَارَ بِاَلَّتِي تَلِي اَلْإِبْهَامَ}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa anakaa kwa ajili ya Tashahhud aliweka kiganja chake cha kushoto juu ya goti lake la kushoto, na cha kuume juu ya goti lake la kuume, na akakunja vidole vyake[48] na akaashiria kwa kidole chake cha kulia cha Shahaadah.” [Imetolewa na Muslim]
Na katika mapokezi yake mengine tamshi la Muslim ilisema: “Na alikunja vidole vyake vyote vya mkono wa kuume, na akaashiria kwa kidole chake cha Shahaadah.”
248.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {اِلْتَفَتَ إِلَيْنَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : "إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَقُلْ : اَلتَّحِيَّاتُ لِلَّهِ ، وَالصَّلَوَاتُ ، وَالطَّيِّبَاتُ ، اَلسَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا اَلنَّبِيُّ وَرَحْمَةَ اَللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ ، اَلسَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اَللَّهِ اَلصَّالِحِينَ ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ، ثُمَّ لِيَتَخَيَّرْ مِنْ اَلدُّعَاءِ أَعْجَبُهُ إِلَيْهِ ، فَيَدْعُو} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ .
وَلِلنَّسَائِيِّ :{كُنَّا نَقُولُ قَبْلِ أَنْ يُفْرَضَ عَلَيْنَا اَلتَّشَهُّدُ}
وَلِأَحْمَدَ :{أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَلَّمَهُ اَلتَّشَهُّد ، وَأَمَرَهُ أَنْ يُعَلِّمَهُ اَلنَّاسَ}
وَلِمُسْلِمٍ : عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ يُعَلِّمُنَا اَلتَّشَهُّدَ: " اَلتَّحِيَّاتُ اَلْمُبَارَكَاتُ اَلصَّلَوَاتُ لِلَّهِ ...} إِلَى آخِرِهِ
Kutoka kwa Abdullaah bin Mas- ‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Alitugeukia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mmoja wenu anaposwali aseme:
“At-tahiyyaatu liLLaah, wasw-Swalawaatu, watw-Twayyibaatu. As-salaamu ‘alayka ayyuhan-Nabiy wa-RahmatuLLaahi wa Barakaatuh, As-salaamu ‘alaynaa wa ‘alaa ‘ibaadi-LLaahi-sw-Swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illaa Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu.”
(Maamkizi mema ni ya Allaah, na Swalaah na maneno mema yote. Amani iwe juu yako Ee Nabiy[49] na Rahmah za Allaah na Baraka Zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja Swalihina wa Allaah, Ninashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake).
Kisha achague dua yoyote[50] aipendayo aisome.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Katika mapokezi ya An-Nassaiy: “Tulikuwa tukisema kabla ya kufaradhishwa (At-Tashahhud).[51]”
Na katika mapokezi ya Ahmad: “Kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimfundisha At-Tashahhud na akamuamrisha kuwafundisha watu.”
Na katika Muslim kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufundisha At-Tashahhud:
“At-Tahiyyaatu, Al-Mubaarakatu, Asw-Swalawaatu, Atw-Twayyibaatu liLLaah…”
(Maamkizi mema, maneno yenye baraka na mazuri yote, Swalaah ni kwa ajili ya Allaah).
Mpaka mwisho wake.
249.
وَعَنْ فَضَالَةَ بْنِ عُبَيْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {سَمِعَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم رِجْلاً يَدْعُو فِي صَلَاتِهِ ، لَمْ يَحْمَدِ اَللَّهَ ، وَلَمْ يُصَلِّ عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : " عَجِلَ هَذَا " ثُمَّ دَعَاهُ ، فَقَالَ : " إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ رَبِّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ، ثُمَّ يُصَلِّي عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ يَدْعُو بِمَا شَاءَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَالثَّلَاثَةُ ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd[52] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimsikia mtu akiomba du’aa ndani ya Swalaah na hakumhimidi Allaah wala hakumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akasema: “Huyu ameharakisha.” Kisha akamuita yule mtu na akasema: “Mmoja wenu anaposwali, aanze kwa kumhimidi Rabb wake na kumsifu, kisha amswalie Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kisha aombe anachotaka.” [Imetolewa na Ahmad na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na waliisahihisha At-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
250.
وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ اَلْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {قَالَ بَشِيرُ بْنُ سَعْدٍ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! أَمَرَنَا اَللَّهُ أَنْ نُصَلِّيَ عَلَيْكَ ، فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ ؟ فَسَكَتَ ، ثُمَّ قَالَ: " قُولُوا : اَللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ ، وَبَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ فِي اَلْعَالَمِينَ إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ . وَالسَّلَامُ كَمَا عَلَّمْتُكُمْ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَزَادَ اِبْنُ خُزَيْمَةَ فِيهِ :{فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ ، إِذَا نَحْنُ صَلَّيْنَا عَلَيْكَ فِي صَلَاتِنَا}
Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd Al-Answaariyy[53] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Bashiyr bin Sa’d[54] amesema Ee Rasuli wa Allaah! Allaah Ametuamrisha tukuswalie, sasa tukuswalie namna gani? (Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akanyamaza, kisha akasema: Semeni[55]:
“Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiym, wa Baarik ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa Ibraahiym fil ‘Aalamiyna Innaka Hamiydun Majiyd.”
(Ee Allaah! Mswalie Muhammad na ahli wa Muhammad, kama ulivyomswalia Ibraahiym na Umbariki Muhammad na ahli wa Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym Ulimwenguni kote, hakika Wewe ni Mwenye Kuhimidiwa, Mtukufu)[56]
na kusalimiana ni kama mnavyojua.” [Imetolewa na Muslim]
Na akaongezea Ibn Khuzaymah: “Namna gani tukuswalie wakati tushakuswalia katika Swalaah zetu.”
251.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِذَا تَشَهَّدَ أَحَدُكُمْ فَلْيَسْتَعِذْ بِاَللَّهِ مِنْ أَرْبَعٍ ، يَقُولُ : اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ ، وَمِنْ عَذَابِ اَلْقَبْرِ ، وَمِنْ فِتْنَةِ اَلْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ ، وَمِنْ شَرِّ فِتْنَةِ اَلْمَسِيحِ اَلدَّجَّالِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ :{إِذَا فَرَغَ أَحَدُكُمْ مِنْ اَلتَّشَهُّدِ اَلْأَخِيرِ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu anapomaliza Tashahhud, aombe isti’aadhah (kinga) kwa Allaah dhidi ya mambo manne aseme:
“Allaahumma inniy a’uwdhubika min ‘adhaabi Jahannama, wamin ‘adhaabil qabri, wamin fitnatil-mahyaa wal-mamaati, wamin sharri fitnatil-masiyhid-dajjaal.”
(Ee Allaah, naomba kinga Kwako dhidi ya adhabu ya Jahannam na adhabu ya kaburi[57], na dhidi ya mitihani ya uhai na mauti, na dhidi ya mitihani ya Masiyh Ad-Dajjaal[58]).[59] [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Akimaliza mmoja wenu Tahiyyaat ya mwisho.”
252.
وَعَنْ أَبِي بَكْرٍ اَلصِّدِّيقِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ قَالَ لِرَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ عَلِّمْنِي دُعَاءً أَدْعُو بِهِ فِي صَلَاتِي . قَالَ قُلْ : "اَللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا ، وَلَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ ، فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ ، وَارْحَمْنِي ، إِنَّكَ أَنْتَ اَلْغَفُورُ اَلرَّحِيمُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amepokea[60] kuwa alimuambia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Nifundishe du’aa ya kuomba katika Swalaah yangu. Akasema: Sema:
“Allaahumma inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman kathiyran, walaa yaghfirudh-dhunuwba illaa Anta, faghfir-liy maghfiratan min ‘Indika, war-hamniy, Innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym.”
(Ee Allaah, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, wala hapana wa kughufiria dhambi isipokuwa Wewe, kwa hivyo naomba unighufirie maghfirah Yako na unirehemu, Hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu).[61] [Al-Bukhaariy, Muslim]
253.
وَعَنْ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَكَانَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ : " اَلسَّلَام عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اَللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ " وَعَنْ شِمَالِهِ : " اَلسَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اَللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ صَحِيحٍ
Kutoka kwa Waail bin Hujr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimeswali pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitoa Salaam kulia kwake[62] akisema:
“Assalaam ‘alaykum wa-RahmatuLLaahi wa-Barakaatuh.”
(Amani iwe juu yenu na Rahmah za Allaah na Baraka Zake)
na kushoto akisema:
“Assalaam ‘alaykum wa-RahmatuLLaahi wa-Barakaatuh.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
254.
وَعَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم { كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةِ مَكْتُوبَةٍ : " لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ اَلْمُلْكُ ، وَلَهُ اَلْحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، اَللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا اَلْجَدِّ مِنْكَ اَلْجَدُّ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alikuwa akisema mwisho wa kila Swalaah ya faradhi:
“Laa ilaaha illaa Allaah Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulk wa-Lahul-Hamd wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, Allaahumma laa maani’a limaa A’twayta, wa laa mu’twiya limaa Mana’ta, wa laa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu.”
(Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake Hana mshirika, Ufalme ni Wake, Kuhimidiwa ni Kwake, Naye ni Mweza wa kila kitu. Ee Allaah, hakuna wa kuzuia Ulilotoa, wala wa kulitoa Ulilozuia, wala mwenye utajiri hatanufaishwa chochote Kwako na utajiri wake)[63]. [Al-Bukhaariy, Muslim]
255.
وَعَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {إِنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَتَعَوَّذُ بِهِنَّ دُبُرَ اَلصَّلَاةِ : " اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ اَلْبُخْلِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ اَلْجُبْنِ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلَى أَرْذَلِ اَلْعُمُرِ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ اَلدُّنْيَا ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ اَلْقَبْرِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Sa’d bin Abii Waqqaasw[64] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akijikinga (kwa Allaah) baada ya kila Swalaah:
“Allaahumma inniy a’uwdhubika minal-bukhli, wa a’uwdhubika minal-jubni, wa a’uwdhubika min an uradda ilaa ardhalil-‘umuri, wa a’uwdhubika min fitnatid-dunyaa wa adhaabil-qabri.”
(Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ubakhili, na najikinga Kwako kutokana na uoga, na najikinga Kwako kurudishwa katika umri wa kudhalilika [uzee][65], na najikinga Kwako fitnah za dunia na adhabu za kaburi). [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
256.
وَعَنْ ثَوْبَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا اِنْصَرَفَ مِنْ صَلَاتِهِ اِسْتَغْفَرَ اَللَّهَ ثَلَاثًا ، وَقَالَ : " اَللَّهُمَّ أَنْتَ اَلسَّلَامُ وَمِنْكَ اَلسَّلَامُ . تَبَارَكْتَ يَا ذَا اَلْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Thawbaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa alipomaliza Swalaah yake, anaomba maghfirah kwa Allaah mara tatu[66], na anasema:
“Allaahumma Antas-Salaam, wa Minkas-Salaam, Tabaarakta yaa Dhal Jalaali wal Ikraam.”
(Ee Allaah, Wewe Ndiye Amani, na Amani hutoka Kwako, Umebarikika ee Mwenye Ujalali na Utukufu).[67] [Imetolewa na Muslim]
257.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : {مَنْ سَبَّحَ اَللَّهَ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ ، وَحَمِدَ اَللَّهِ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ ، وَكَبَّرَ اَللَّهُ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ ، فَتِلْكَ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ ، وَقَالَ تَمَامَ اَلْمِائَةِ : لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ اَلْمُلْكُ ، وَلَهُ اَلْحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، غُفِرَتْ لَهُ خَطَايَاهُ ، وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ اَلْبَحْرِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَفِي رِوَايَةٍ أُخْرَى: أَنَّ اَلتَّكْبِيرَ أَرْبَعٌ وَثَلَاثُونَ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakaye Sabbih (Subhaana Allaah) kila baada ya Swalaah mara thelathini na tatu[68], akaleta tahmiyd (AlhamduliLLaah) mara thelathini na tatu akaleta takbiyra (Allaahu Akbar) mara thelathini na tatu, akamalizia itimie mia kwa:
“Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr.”
(Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu), ataghufuriwa makosa yake japokuwa ni mfano wa povu la bahari.” [Imetolewa na Muslim]
Na katika mapokezi mengine: “Takbiyra ni mara thelathini na nne.”
258.
وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{قَالَ لَهُ : " أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ : لَا تَدَعَنَّ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ أَنْ تَقُولُ : اَللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيُّ بِسَنَدٍ قَوِيٍّ
Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia: “Nakuusia ee Mu’aadh! Usiache abadani baada ya kila Swalaah kusema:
“Allaahumma a’inniy ‘alaa Dhikrika wa Shukrika, wa husni ‘ibaadatika.”
(Ee Allaah! Nisaidie kukudhukuru, na kukushukuru, na kukuabudu kwa uzuri upasao). [Imetolewa na Amad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kwa Isnaad yenye nguvu (Qawiyy)]
259.
وَعَنْ أَبِي أُمَامَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{مَنْ قَرَأَ آيَةَ اَلْكُرْسِيِّ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ لَمْ يَمْنَعْهُ مِنْ دُخُولِ اَلْجَنَّةِ إِلَّا اَلْمَوْتُ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
وَزَادَ فِيهِ اَلطَّبَرَانِيُّ :{وَقُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ}
Kutoka kwa Abuu Umaamah[69] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma Aayatul kursiyy[70] mwisho wa kila Swalaah ya faradhi, hakuna kitakachomzuia kuingia Jannah isipokuwa[71] mauti.”[72] [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
At-Twabaraaniyy aliongezea: “Na Qul-Huwa-Allaahu Ahad.”[73]
260.
وَعَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ صَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Maalik bin Al-Huwayrith (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”[74] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
261.
وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَالَ لِيَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " صَلِّ قَائِمًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَقَاعِدًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَعَلَى جَنْبٍ وَإِلَّا فَأَوْمِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swali huku umesimama, na ukiwa huwezi swali kwa kukaa, na ukiwa huwezi, swali kwa ubavu, laa sivyo swali kwa ishara.”[75] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
262.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {قَالَ لِمَرِيضٍ صَلَّى عَلَى وِسَادَةٍ ، فَرَمَى بِهَا وَقَالَ : " صَلِّ عَلَى اَلْأَرْضِ إِنْ اِسْتَطَعْتَ ، وَإِلَّا فَأَوْمِئْ إِيمَاءً ، وَاجْعَلْ سُجُودَكَ أَخْفَضَ مِنْ رُكُوعِكَ} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ بِسَنَدٍ قَوِيٍّ وَلَكِنْ صَحَّحَ أَبُو حَاتِمٍ وَقْفَهُ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia mgonjwa aliyekuwa anaswali juu ya mto (tandiko) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliutupa, akasema: “Swali juu ya ardhi ukiweza, vinginevyo swali kwa ishara na uzifanye Sijdah zako ziwe chini zaidi kuliko rukuu zako.” [Imetolewa na Al-Bayhaq kwa Isnaad yenye nguvu, lakini Abuu Haatim aliisahihisha iliyo Mawquwf]
[1] Ni wazi kwamba kuisoma Qur-aan ni lazima. Kuna Hadiyth inayosema:
((ثُمَّ اِقْرَأ بِأمِّ الْقُرْآن))
((Kisha soma kwa Mama wa Qur-aan))
Ni wazi kuwa inamaanisha Suwrah Al-Faatihah.
[2] Wale watu ambao hawarukuu vizuri, hawasujudu vizuri, na hawakai vizuri, n.k katika Swalaah zao, waizingatie Hadiyth hii. Vitendo vinavyofanywa ovyo-ovyo, na harakaharaka siyo sahihi. Hivi vitendo vya ovyo-ovyo huharibu Swalaah zao. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema Swalaah kama hiyo ni “Swalaah ya mnafiki” na wanaotenda hivyo ni “Wezi wa aina mbaya kabisa.”
[3] Huyu Rifaa’ah alipewa jina la utani la Abuu Mu’aadh na alikuwa Az-Zurqi Al-Answaar Al-Madaniy, Swahaba mkubwa ambaye alishiriki katika Al-‘Aqabah pamoja na babake ambaye alikuwa Answaar wa kwanza kusilimu. Rifaa’ah alishiriki katika vita vya Badr na vita vyote vilivyofuata; na pia alikuwa pamoja na ‘Aliy katika vita vya Al-Jamal na Siffiyn. Alikufa mwanzoni mwa Ukhalifa wa Mu’aawiyah mnamo mwaka 41 A.H.
[4] Ummul-Qur-aan ni jina lingine la Suwrah Al-Faatihah. Hadiyth hii ya kusoma Al-Faatihah na Suwrah au Aayah zingine za Qur-aan ni muhimu. Kwa mujibu wa ‘Ulamaa wengine, baada ya kuisoma Al-Faatihah ni muhimu kusoma zaidi, na wengine wanasema inapendeza. Ukitaka kujua zaidi soma vitabu vya Hadiyth.
[5] Abuu Humayd anaitwa ‘Amr au Mundhir bin Sa’d bin Al-Mundir au Maalik Al-Answaar Al-Khazraj Al-Madaniy. Ametoka katika kizazi cha Saa’idah ambaye ndiye baba wa Al-Khazraj. Alishiriki katika Uhud na vita vilivyofuatia, na akafariki ima mwishoni mwa Ukhalifa wa Mu’aawiyah au mwanzoni mwa utawala wa Yaziyd mnamo mwaka 61 A.H.
[6] Ummah wote wa kiislamu unatakiwa uswali kama alivyokuwa akiswali mwenyewe Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alikuwa akiswali kwa amani na utulivu wa akili na ukamilifu. Kuswali kwa papara, harakaharaka kunakatazwa.
[7] Katika Hadiyth hii, “Raf’u yadayni” (kunyanyua mikono) imetajwa kuwa ifike hadi mabegani. Usimulizi wa Waail bin Hujr, umetaja hadi masikioni.
[8] Katika mwisho wa Hadiyth hii, inatajwa kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma du’aa hii wakati wa kuswali Tahajjud iswaliwayo katikati ya usiku. Mtunzi, katika kitabu chake cha Talkhiys, ameripoti kutoka kwa Imaam Shaafi’iy na Ibn Khuzaymah kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliisoma du’aa hiyo katika Swalaah zote za faradhi. Katika usimulizi wa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) anasema uwezekano wa kusoma du’aa hii katika Swalaah zote mbili upo.
[9] Katika maneno haya matukufu, Muislamu anaagizwa aombe maghfirah kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya dhambi zake, anazozijua na asizozijua, hata awe mtiifu sana kuliko wote.
[10] Suwrah Al-Faatihah:
[11] “’Uqbat ash-shaywaan” (mkao wa shaytwaan) ni kuweka matako ardhini na kunyanyua magoti na mguu uliyoko chini ya goti na viganja vikiwa ardhini pande zote mbili. “Iftiraash As-Sab’i” (kutandaza mikono kama mnyama mwitu) ni kukalia sehemu za nyuma za mguu wa chini na sehemu ya nyuma ya paja na kisha kuinamia mbele huku ukinyoosha viganja mbele yako juu ya ardhi.
[12] Simulizi hii ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) ni dhahiri kabisa kuthibitisha kwa kila mwanzo wa Swalaah, wakati wa kurukuu, kuinuka baada ya kurukuu, kunyanyua mikono mpaka kwenye masikio ni Sunnah. Hayo maneno:
كانَ يَرْفَعُ
“alikuwa akinyanyua…”
Yanaonyesha udumishaji. Inathibitisha unyanyuaji wa mikono haukuwahi kufutwa wala kuachwa. Ahaadiyth zote zinazopinga “kunyanyua mikono” ni dhaifu au mawdhwu’ (zimetungwa). Miongoni mwa Hadiyth dhaifu, udhaifu wa zingine umeafikiwa na wengi, na zingine zina kukhitilafiana. Katika zote hizo, usimulizi wa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd huhesabika kuwa bora zaidi. Imaam Al-Bukhaariy alinukuu maoni ya kishariy’ah ya mwalimu wake ‘Ali bin Al-Madiniy kwa msingi wa simulizi za ‘Abdullaa bin ‘Umar ni lazima kwa kila Muislamu kunyanyua mikono. Ikhtilaaf kuhusu kadhia hii ni pana mno kujadaliwa hapa.
[13] Waail bin Hujr au Abuu Hunayda au Abuu Hinda, alikuwa Swahaba mkubwa, na babake alikuwa mmoja wa wafalme wa Hadhramaut. Alimzuru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambaye alitandika shali (nguo ya juu) yake ili akalie, na akamuombea Baraka yeye na wanawe, na kisha akamteua awe mkuu wa Aqyal ya Hadhramaut. Alilowea mji wa Kufa, na akafariki wakati wa Ukhalifa wa Mu’aawiyah.
[14] Hadiyth hii inaweka wazi mambo mawili: Kwanza kuikunja mikono ndani ya Swalaah ni Sunnah, na kutokuikunja ni kuipinga Sunnah. Watu wengine wameipokea Hadiyth hii kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) lakini siyo sahihi. Pili, mkono ikunjwe juu ya kifua, siyo chini ya kitovu, kama wanavyofanya watu wengine. Usimulizi wanaotegemeza ubishani wao pia siyo sahihi.
[15] ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit alikuwa mmoja wa viongozi wa ki-Answaar katika ‘Aqabah (Maktaba) wa kwanza na wa pili wa Aqaba. Pia alihudhuria katika vita vya Badr na vita vilivyofuata. ‘Umar alimpeleka Shaam awe Kadhi na mwalimu. Kwa hivyo alilowea Hims na baadaye alikwenda Palestina na akafia Ramlah au Bayt Al-Maqdis mnamo mwaka 34 A.H. akiwa na miaka 72.
[16] Hadiyth iliyotajwa hapo juu ni ushahidi tosha kuwa bila kusoma Suwrah Al-Faatihah Swalaah haiswihi. Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na wafuasi wa Maswahaba na wengi wa ‘Ulamaa waliiamini desturi hii. Katika Hadiyth ijulikanayo kama (مسء الصلاة) - maneno yenyewe ni:
إِقْراْ بِاُمِّ الْكِتاب
(Soma kwa Ummul-Kitaab)
Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha kuswali kwa kusoma Al-Faatihah katika kila Rakaa. Imaam na Maqtadi (Maamuma) wote sharti waisome Al-Faatihah. Hakuna mtu yoyote aliyeepushiwa kusoma, na yatakiwa isomwe katika kila Swalaah, kimyakimya (Sirran) au kwa sauti (Jahran), ni lazima kuisoma Al-Faatihah. Muslim amesimulia Hadiyth aliyoipokea Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), aliulizwa juu ya kuisoma Al-Faatihah, endapo Swalaah inaswaliwa nyuma ya Imaam. Abuu Hurayrah alijibu kuwa: ni lazima isomwe kwa siri kwa sauti ya chini. At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy wameripoti Hadiyth kutoka kwa ‘Ubaadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwahi kuwauliza: “Je mnasoma chochote mkiwa nyuma ya Imaam?” Maswahaba wakajibu: ‘Ndiyo,” Ndipo Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia: Someni Al-Faatihah na siyo nyingine yoyote, kwa kuwa bila kuisoma Suwrah hiyo Swalaah haiswihi. Kuna Hadiyth nyingine nyingi tu ambazo zinathibitisha kuwa kuisoma Al-Faatihah ni lazima hata ukiwa nyuma ya Imaam pia. Ama kuhusu Hadiyth inayosema kuwa kusoma kwa Imaam kunatosheleza kwa Maamuma pia, ni dhaifu. Miongoni mwa wale wanaoamini maoni haya (kuisoma Al-Faatihah), kwengine wanaona kuwa Al-Faatihah isomwe katikati ya mapumziko ya visomo vya Imaam, na wengine wanasema kuwa isomwe baada ya kumaliza Imaam kusoma Al-Faatihah.
[17] Inamaanisha kuwa walikuwa hawaisomi kwa sauti, bali waliisoma kimyakimya kama ilivyosema Hadiyth iliyofuatia.
[18] Mtu anaweza kufanya yoyote kati ya hizo njia, ni sahihi.
[19]Nu’aym huyu ndiye Abuu ‘Abdillaah Nu’aym ‘Abdillaah Al-Mujmir, ambaye ni mtumwa aliyeachwa huru na ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alikuwa akifukiza manukato katika Msikiti wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kila siku ya Ijumaa saa sita mchana, kwa hivyo alipewa jina la utani la Al-Mujmir. Alikuwa Taabi’i na Abuu Haatim, Ibn Ma’iyn, Ibn Sa’d na An-Nasaaiy walimthibitisha kuwa ni wa kutegemewa.
[20] Baada ya kuisoma Suwrah Al-Faatihah ni Sunnah kusema “Aamiyn”. Ikiwa ni Imaam au Maamuma, kila mtu ni wajibu kusema “Aamiyn” ambayo maana yake ni: “Ee Allaah Ikubali du’aa hii au kisomo hiki.”
[21] “Aamiyn” inajuzu kwa sauti au kimyakimya. Kuna kutofautiana maoni juu ya kadhia hii. Hanafiyah wanaisoma kimyakimya. Shaafi’i na Ahlul-Hadiyth huisoma kwa sauti kubwa. Sauti kubwa (Jahr) maana yake, ni sauti ya mtu wa pili kuweza kuisikia. Kusoma “Aamiyn” kwa sauti kubwa kumethibitishwa na Ahaadiyth nyingi zingine. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma kwa sauti na alikuwa akiirefusha. At-Tirmidhiy aliipa Hadiyth hii kuwa ni Hasan, na Ad-Daaraqutwniy aliipa daraja la Swahiyh. Maulana Abdul-Hayy Lucknowi alisema kuwa, kwa mujibu wa kutopendela upande wowote, kuisoma Aamiyn kwa sauti kubwa ni sahihi zaidi. Ama kuhusu kuisoma Aamiyn kimya kimya, Imaam At-Tirmidhiy amesimulia Hadiyth ambayo kwayo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliisoma Aamiyn na akatumia sauti ya chini. Kwa hivyo baadhi ya Wahanafi wanahoji matumizi ya Hadiyth hii, ingawa At-Tirmidhiy mwenyewe ameikanusha Hadiyth hii kwa nukta nne za maoni. Hata hivyo, kila mtu ana uhuru na anawajibika kwa desturi na matendo yake mwenyewe.
[22] ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa ndiye aliyepewa jina la utani la Abuu Mu’aawiyah, na jina la babake ilikuwa ‘Alqamah bin Al-Haarith Al-Aslamiy. Yeye na babake wote walikuwa Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alihudhuria Al-Hudaybiyyah, Khaybar, na vita vilivyofuata. Aliishi katika mji wa Kufa nchini ‘Iraaq na alifariki huko katika mwaka 87H. Alipofuka macho na alikuwa Swahaba wa mwisho kufariki katika mji wa Kufa huko ‘Iraaq.
[23] Watu wengine hutumia Hadiyth hii kudai kuwa kusioma Suwrah Al-Faatihah ndani ya Swalaah siyo lazima kwa sababu Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakusema kuwa alilazimika kujifunza Al-Faatihah. Hii na ikumbukwe kwamba kuna kuwahurumia walemavu katika Shariy’ah. Makatazo na amri huwa hazibadili Shariy’ah za kuhurumia kama hizo. Iwapo mtu anasema kuwa hawezi kutawadha kwa sababu asizoweza kuzizuia, basi huambiwa ajitwahirishe kwa kutayammam (kwa mchanga); na hii haimaanishi kuwa kuchukua wudhuu siyo lazima.
[24] Hii imeafikiwa na wengi kuwa kuisoma Al-Faatihah kwa Swalaah za Adhuhuri na Alasiri huwa kwa sauti ya chini au kimyakimya.
[25] Inaelekea kutoka katika Hadiyth hii kuwa, hakuisoma Suwrah yoyote baada ya Al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho. Lakini Hadiyth ya Abuu Sa’iyd katika Swahiyh Muslim inaripoti kwamba, walikisia urefu wa Rakaa ya mwisho ni kama Aayah 15 wakati wa Aayah za Al-Faathah ni Aayah 7 tu. Kwa hivyo, yaelekea kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alizisoma Aayah zingine na wakati mwingine hakuzisoma. Yaani, kusoma katika Rakaa za mwisho ni Sunnah.
[26] Suwrah As-Sajdah (32: 1-30) ambayo ina Aayah thelathini (30).
[27] Sulaymaan bin Yasaar alikuwa ni mmoja wa ‘Ulamaa saba wa Fiqh na miongoni mwa Taabi’iyn maarufu. Alikuwa ni wa kutegemewa, mwenye taqwa, msomi, na alihifadhi Hadiyth nyingi. Alipewa jina la utani la Abuu Ayyuwb, na alikuwa mtumwa alieachwa huru na Maymuwnah, (Mama wa Waumini). Alifariki mnamo mwaka wa 107A.H. akiwa na umri wa miaka 73.
[28] Kutoka Suwrah ya Al-Hujuraat mpaka mwisho, Suwrah zote zinaitwa “Mufasw-swal” (zilizopambanuliwa), kwa sababu ya nafasi ndefu kati ya BismiLLaahi mbili. Na kutoka Suwrah ya Al-Hujuraat hadi Al-Buruwj zinaitwa “Twiwaal Mufasw-swal” (ndefu zilizopambanuliwa) na kutoka Al-Buruwj mpaka Al-Bayyinah mpaka mwisho zinaitwa “Awsaatw Mufasw-swal” (zenye urefu wa wastani). Na kutoka Al-Bayyinah mpaka mwisho zinaitwa “Qiswaar Mufasw-swal” (Fupi zilizopambanuliwa). Kuisoma Twiwaal katika Swalaah za Alfajiri, Awsaatw katika Swalaah za ‘Ishaa, na Qiswaar katika Swalaah ya Magharibi ni Sunnah. Mara nyingine hutokea kinyume chake kama inavyoelezewa katika Hadiyth ifuatayo.
[29] Hadiyth zingine zinaripoti kwamba, Suwrah Al-A’raaf, Asw-Swaffaat, na Ad-Dukhaan pia zilizomwa kwenye Swalaah ya Magharibi. Inamaanisha kuwa Suwrah ndefu pia zimewahi kusomwa katika Swalaah ya Magharibi; na Mu’awwidhatayn (Suwrah Al-Falaq na An-Naas) zilizosomwa katika Swalaah ya Alfajiri. Lakini kawaida ilikuwa ni kusoma kama ilivyoelezwa hapo juu.
[30] Katika Suwrah hizi yametajwa mambo ya kuumbwa kwa Aadam, maajabu ya uumbaji, na Siku ya Mkusanyiko, na Siku ya kufufuliwa itatokea siku ya Ijumaa. Kwa sababu hii, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akizisoma Suwrah hizi mnamo siku ya Ijumaa, ili watu waweze kufikiri kuwa kitu chaweza kutokea leo na wamuogope Allaah (سبحانه وتعالى).
[31] Inamaanisha kuwa, Suwrah hizi zisomwe kila siku ya Ijumaa katika Swalaah ya Alfajiri, Suwrah zozote maalumu ambazo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akizisoma katika Swalaah yoyote maalumu kwa mpangilio maalumu na kila mara, ni vizuri kuzisoma hizo kwa namna ile ile kwa kila Swalaah kwa kuwa hiyo ndiyo Sunnah. Kuzisoma Suwrah nyingine pia inaruhusiwa.
[32] Katika Rukuu na Sijdah, kusoma Qur-aan ni haraam na inachukiza. Kuna sehemu nyingi za Qur-aan, na kila sehemu ina namna yake, na kwa kila sehemu imeelezwa du’aa na maombi maalumu. Katika Rukuu yatakiwa kusomwa:
سُبْـحانَ رَبِّـيَ الْعَظـيم
na katika Sijdah isomwe:
سُبْـحانَ رَبِّـيَ الأَعْلـى
Katika Sijdah inaruhusiwa kuomba du’aa.
[33] Takbiyra ya kwanza inaitwa Takbiyraatul-Ihraam (ya kukataza kufanya lolote liwalo isipokuwa Swalaah tu), au huitwa Takbiyratul-Iftitaah (ya kufungulia), au Takbiyratul-Uwlaa (ya mwanzo), na Takbiyra zingine zote zinaitwa Takbiyratul-Intiqaal, maana yake ni ya kuhamia ndani ya Swalaah kwa mfano kutoka katika kisimamo hadi kwenda Rukuu, na kutoka Rukuu kwenda Sijdah, n.k. Ile Takbiyra ya mwanzo (Takbiyratul-Ihraam) imeshurutishwa kuwajibika, na Takbiyra zinazobakia ni za Sunnah, na kwa mujibu wa wengine ni waajib (lazima).
[34] Neno hilo جد linatumika katika lugha ya Kiarabu kwa maana mbili; Kwanza babu na mababu, na pili utukufu na hadhi. Maana zote mbili ni sahihi katika muktadha huu kwa sababu mali au utajiri, utukufu wa kuzaliwa na taadhima, vyote havina thamani mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى). ‘Amali njema pekee ndiyo dira ya kuepukia adhabu. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia binti yake Faatwimah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kutenda ‘amali njema ili kujiokoa yeye mwenyewe kutokana na adhabu ya Allaah (سبحانه وتعالى), na wala asimtegemee babake (Yeye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wala unasaba wake. Kuokoka kunategemea ‘amali njema tu, sasa iwapo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamuambia hivyo binti wa kumzaa yeye mwenyewe namna hii, basi nani mwingine tena anaweza kujivunia hadhi ya kuzaliwa?
[35] Du’aa hii ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni ushahidi tosha wa kukanusha dhana ya wale wanaosimama wima moja kwa moja baada ya kurukuu, na kuchukulia kwamba ucheleweshaji wa kutamka Tasbiyh tatu (yaani kusema سبحان الله) utaifanya Sijdah ya kulipia ni lazima. Inapokuwa imethibitishwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) basi tena hakuna nafasi ya maoni ya mtu mwingine binafsi.
[36] Hadiyth hii inaweka wazi kuwa paji la uso na pua, vyote vinahesabika kuwa ni kiungo kimoja. Ukihesabu paji la uso mbali na pua, utapata viungo vinane.
[37] Huyu Ibn Buhaynah ni Abuu Muhammad ‘Abdillaah bin Maalik bin Al-Qishb Al-Azdi, na hilo Buhaynah ni jina la mamake. Alisilimu zamani na akawa mtawa, mwenye taqwa, na alikuwa akifunga (Swawm) siku zote. Alifariki chini ya bonde la Rim, maili tatu kutoka Al-Madiynah, mnamo mwaka wa 54 au 58 A.H.
[38] Huyu Al-Baraa ndiye Abuu ‘Ammaara Al-Baraa bin ‘Aazib bin Al-Haarith bin ‘Adiy Al-Answaariy Al-Aws, ambaye alikuwa Swahaba na pia mwana wa Swahaba. Aliachwa kwenye vita vya Badr kwa sababu ya umri wake ulikuwa mdogo, na kushiriki kwake mara ya kwanza kulikuwa katika vita vya Uhud au Al-Khandaaq. Aliteka Ar-Ray na alishiriki katika vita vya Al-Jamaal, Siffiyn, na Naharwaan pamoja na ‘Aliy. Alifia Kufa mnamo mwaka wa 72 A.H.
[39] Hii ilikuwa kwa ajili ya kutojiweza kwa sababu alianguka kutoka juu ya farasi wake, na akateguka kiunganishi cha mguu wake.
[40] Inamaanisha katika Rakaa ya kwanza na ya tatu. Na hii inaitwa Jalsatul-Istiraahah (mkao wa kupumzika). Kwa mujibu wa usimulizi, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akikaa katika mkao huu kwa muda mrefu kiasi kwamba watu walifikiri ni kwa ajili ya kusahau kwake. Haikuwa kwa sababu ya umri wake, kwani yeye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamwe hakurahisisha wajibu wake wowote kwa ajili ya udhaifu utokanao na uzee.
[41] Makabila haya yalikuwa ya رعل (Ri’il), ذكوان (Dhakwaan) na عصية (‘Uswayyah). Haya yalifanya bay’ah (mkataba) na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini yakavunja ahadi yao na yakawaua Wahubiri sabiini wa Kiislamu baada ya kuwategea kwa kuwaalika. Tukio hili linajulikana kama Bi’r Ma’uwnah.
[42] Inaelekea kuwa kuna ikhtilaaf miongoni mwa Hadiyth hizi. Ya kwanza inasema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) daima alikuwa akisoma Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri kisha akaacha. Hadiyth nyengine inasema kuwa aliisoma Qunuwt kila alipokuwa akiomba ustawi wa kijamii wa taifa au kuwalaani watu fulani kwa ufisadi wao. Hadiyth ya tatu inasema kuwa, kusoma Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri ni uzushi. Lakini iliyo sahihi ni kwamba haikuwa ni waajib zama hizo kuisoma Qunuwt kama wafanyavyo baadhi ya watu sasa kuidumisha Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri, bali lililo sahihi ni kuwa Qunuwt inasomwa pale inapotokea shida fulani kwa Waislamu, kisha inapomalizika huachwa kutekelezwa Qunuwt kama ilivyotajwa katika Hadiyth namba (242) ya Al-Bukhaariy na Muslim.
[43] Sa’d huyu ndiye Abuu Maalik Sa’d bin Twaariq bin Ashyaam bin Mas-‘uwd Al-Ashja’iy Al-Kuwfi. Alikuwa miongoni mwa Taabi’iyn waliotegemewa. Alifariki mnamo mwaka 140 A.H.
[44] Twaariq ni Swahaba aliyesimulia Hadiyth chache. Hadiyth kumi nne tu ndizo zilizosimuliwa kutoka kwake, na zote zilisimuliwa na mwanae huyo aliyetajwa hapo juu, Sa’d. Alistakir kule Kufa.
[45] Al-Hasan ni mjukuu kipenzi wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na ni mmoja wa vijana wa Jannah. Alizaliwa mnamo mwezi wa Ramadhwaan mwaka wa 3 A.H; na aliapishwa kuwa Khalifa baada ya kuuliwa baba yeke ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), lakini alimkabidhi Mu’aawiyah Ukhalifa mnamo mwezi wa Jumaadal-Uwlaa mwaka 41 baada ya miezi saba tu kwa kuchukia kumwaga damu ya Waislamu. Alikufa mnamo mwaka 49 A.H., na akazikwa Al-Baqiy’.
[46] Ifahamike kuwa baadhi ya watu husoma Qunuwt mikono yao ikiwa wazi kabla ya kurukuu. Lakini sahihi yake ni kusoma kwanza Qunuwt huku mikono imeinuliwa juu baada ya kusimama wima kutoka katika Rukuu. Watu wengine husoma Qunuwt kila wanaposwali Witr, wakati wengine husoma Qunuwt katika wiki mbili za mwisho za mwezi wa Ramadhwaan tu. Watu wengine huhesabu Qunuwt kama ni Waajib (lazima), na wengine huihesabu kuwa ni Sunnah. Ukweli ni kwamba hiyo ni Sunnah.
[47]Kitabu cha Fathul-‘Uluwm kinasema kuwa, Hadiyth zote mbili ni imara, na zinatumika sawasawa. Hata hivyo tendo la Muhaddithiyn (‘Ulmaa Wasimulizi wa Hadiyth) na Hanaabilah (wafuasi wa Hanbali) imeegemezwa kwenye Hadiyth ya Abuu Hurayrah. Msimamo wa Shafi’iyya, Hanafiyya na Malikiyya ummegemezea katika rejea ya Waail.
[48] Sharti ikunjwe kwa njia ambayo mtu aweke kidole gumba chake chini (kifunikwe na) kidole chake cha Shahaadah huku akiwa kavifumba vidole vitatu vilivyobaki. Kisha ainue kidole chake cha Shahaadah wakati akisoma sehemu ya Tahiyyaat inayosema:
أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله
“Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah”
Na wakati anapokishusha asome hivyo hivyo.
[49] Mwanzoni, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufundisha tumswalie yeye, kwa sababu haki yake kwa Ummah wake ni zaidi kuliko mtu yoyote awaye, zaidi kuliko Muumini mwenyewe.
[50] Hadiyth hii inaelezea kuwa, du’aa yoyote ndani ya Swalaah ni kufuata mwendo wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), hii pia inaweka wazi kuwa hakuna jambo lolote makhsusi ambalo mja anaweza kuomba ndani ya Swalaah. Mtu anaweza kuomba chochote akitakacho, iwe cha hapahapa duniani au cha Aakhirah.
[51] Yale maneno ambayo watu walikuwa wakiyasoma kabla ya kufaradhishwa At-Tashahhud hayajatajwa na msimulizi. Lakini kwa mujibu wa Hadiyth zingine, walikuwa wakisema hivi:
السَّلاَمُ عَلَى جِبْرِيلَ، السَّلاَمُ عَلَى مِيكَائِيلَ ...
Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwazuia kusema hivyo, ndipo akawafundisha At-Tashahhud.
[52] Fadhwaalah bin ‘Ubayd bin Naafidh bin Qays alipewa jina la utani la Abuu Muhammad Al-Answaar Al-Aws. Mwanzo alipigana vita vya Uhud na vita vingine vilivyofuata. Alichukua Bay’atur-Ridhwaan. Alilowea Damascus, Shaam na akawa Kadhi wake akiwa aliteuliwa na Mu’aawiyah wakati alipokuwa akienda kwenye vita vya As-Siffiyn. Alifariki mnamo mwaka wa 56 A.H.
[53] Abuu Mas-‘uwd ndiye ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’alabah Al-Answaar Al-Badri, alikuwa ni mmoja wa Maswahaba maarufu. Alishiriki ‘Aqabah ya pili wakati angali kijana. Alilowea Kufa na akafia huko au Al-Madiynah baada ya miaka ya arubaini ya Hijrah.
[54] Bashiyr Ibn Sa’d huyu ndiye Abuu An-Nu’maan Bashiyr bin Sa’d bin Tha’alabah bin Al-Jullaas au Al-Khallaas Al-Answaar Al-Khazraj. Alipigana vita vya Badr, na alihudhuria Bay’atul-‘Aqabah. Pia alishiriki katika vita vya Uhud, Al-Khandaq, na vita vingine vilivyofuata. Aliuwawa kule ‘Ayn At-Tamr mnamo mwaka wa 13 A.H.
[55] Maneno ya kumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yametajwa namna tofauti katika Hadiyth mbalimbali. Kwenye Hadiyth moja huweko neno au maneno zaidi kuliko kwenye Hadiyth nyingine.
[56] Hii inaweka wazi kuwa hiyo kumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yatakiwa isomwe baada ya kusoma At-Tashahhud ndani ya Swalaah, na kuomba du’aa sharti iwe katika Tashahhud ya mwisho tu. Tuna arifiwa zaidi kwamba, kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalaah ndani ya Swalaah ni Waajib (lazima).
[57] Hadiyth hii inatuarifu kwamba, mtu akishafariki hukumbana na adhabu kaburini, halikadhalika inatuarifu kuwa Muumin wa kweli huwa hana khofu yoyote kaburini. Hii inatibitishwa na Hadiyth nyingi tu.
[58] Al-Masiyh Ad-Dajjaal atakuwa ni kafiri atakayezuka kabla ya Siku ya Qiyaamah ili kuijaribu Iymaan za Waumini. Waumini wakweli watabakia wameishikilia Iymaan yao kwa dhati kabisa juu ya madhila makubwa, ambapo watu wenye Iymaan dhaifu na yenye kuyumba, na makafiri na wanafiki, watafuata amri zake huyo Masiyh Ad-Dajjaal. Huyo ataitwa Masiyh na Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) pia anaitwa Masiyh. Ingawa matamshi ya haya majina mawili ni sawa, lakini maana zake hapo ni tofauti. Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) anaitwa Masiyh kwa sababu aliwaponya wagonjwa kwa kuwagusa. Maana ya Masiyh ni kugusa. Lakini Ad-Dajjaal ataitwa Masiyh kwa sababu jicho lake moja limeguswa au limeharibiwa na kwa hivyo limegeuka umbo.
[59] Katika Ahaadiyth zingine maneno yafuatayo yameongezwa:
مِنَ المْغْـرَم وَالْمأْثَمِ
“Minal maghrami wal ma-athami” (dhidi ya madeni na mwenye dhambi). Imeripotiwa katika Al-Bukhaariy kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa kwamba kwa nini alikuwa anaomba hifadhi dhidi ya kuwa na madeni kwa namna hiyo? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema kwamba: “Mtu mwenye deni siyo tu huwa anaongopa, bali pia huwa anavunja ahadi zake. Maafa ya maisha yapo kwenye mwisho wa maisha (huku mtu ukiwa huna Iymaan), na maafa ya kifo yapo katika ukali wa maswali aulizwayo mtu kaburini.”
[60] Huyu ndiye ‘Abdullaah bin ‘Uthmaan Abuu Quhaafah bin ‘Aamir bin At-Taymiy, ambaye ndiye Khalifa wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na mwenzi wake aliyekuwa naye pamoja pangoni, na ndiye mzuri kuliko watu wote wa Ummah huu baki ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mweyewe. Alikuwa mweupe na nywele za singa, mzuri na mwembamba. Anajulikana sana, na hahitaji kujulishwa. Alikufa mnamo Jumaada Al-Aakhir mwaka wa 13 A.H.
[61] Hadiyth hii inafahamisha kuwa, mwana Aadam anapaswa awe muombaji wa maghfirah hata kama amepata daraja la juu kabisa la taqwa, ukweli na ikhlasi.
[62] Kuna simulizi kutoka kwa Maswahaba kumi na tano wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuhusu Tasliym (kumalizia kwa Salaam). Baadhi ya hizo ni Swahiyh, zingine ni Hasan, na zingine ni dhaifu. Hakuna hata moja ya hizo zilikuwa na maneno ya
وَبَرَكاتُه
“wa Barakaatuh.”
Kuna usimulizi mmoja tu kati ya hizi unaohesabika kuwa ni wa kuaminika na unakubalika.
[63] Maneno ya
ذَا اَلْجَدِّ مِنْكَ اَلْجَدُّ
Ina maana: “Endapo Kuridhia Kwako Allaah, hakupo, basi ukuu wote, ufakhari, na mali za kidunia zote, huwa hazina maana, yaani vitu vyovyote vya kidunia utakavyokuwa navyo (mali, vizazi, hadhi na uwezo), haisaidii katika uokovu. Uokovu utapatikana kutokana na Rahmah na Baraka Zako Wewe tu.”
[64] Sa’d bin Abiy Waqqaasw ndiye aliyepewa jina la utani la Abuu Is-haaq bin Maalik, na alikuwa ni Zuhri na Quraysh. Alikuwa ni Muislamu wa tano au wa saba, na ni mmoja wa wale watu kumi ambao waliahidiwa kuingia Jannah. Yeye ni mtu wa kwanza kupiga silaha katika njia ya Allaah, na alishiriki katika vita vyote muhimu. Alikomboa ‘Iraaq kwa ajili ya Uislamu, na du’aa zake zilitakabaliwa. Alikuwa mfupi, mnene, na mwenye nywele nyingi. Alifia Al-‘Aqiyq ambayo iko maili kumi kutoka Al-Madiynah, na alibebwa juu ya mabega ya watu hadi Al-Madiynah, na akazikwa Al-Baqi’y mnamo mwaka 55 H.
[65] Maana ya
أَرْذَلِ اَلْعُمُرِ
Ni pale uzee unamfikia mtu anapokuwa uwezo wa ndani ya mwili wake au nje yake, na akili, unadhoofika ima wote au baadhi yake.
[66] Kuonyesha kutubu na kuomba maghfirah kwa Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya kumaliza Swalaah, ni dalili ya kuwa Swalaah ya mtu anayoswali haina hadhi ya kuiwakilisha mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى), khasa kwa vile mja huwa amekwisha kutenda makosa, ukhalifu na dosari katika Swalaah yake.
[67] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alionyesha kutubu na aliomba maghfirah kwa Allaa (سبحانه وتعالى) kama njia ya kutoa shukrani kwa Allaah (سبحانه وتعالى), pamoja na kuwafundisha watu maadili mema. Basi na Muumini wa kawaida naye hufanya vivyo hivyo kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na utovu wa khushuw’ (unyenyekevu) kwa kumjia fikra na mawazo yanayomtoa nje ya Swalaah na kumweka mbali wakati anaswali.
[68] Adkhaar hizi zinawakilisha mambo yote mazuri ya dunia hii na Aakhirah. Inaelekea kuwa mtu sharti atamke Adhkaar baada ya kila Swalaah ya fardhi na Swalaah ya Sunnah. Lakini baadhi ya Wanachuoni wamependekeza kusoma Adkhaar hizi katika Swalaah za fardhi tu. Kwa hivyo umuhimu wa du’aa baada ya Swalaah za fardhi umethibitishiwa, lakini Ahaadiyth hazithibitishi kuwepo kwa kusoma Adhkaar hizi au du’aa zozote zile kwa pamoja (kwa jamaa) wala kwa kuinua mikono juu. Bali kila mtu anatakiwa asome Adhkaar hizi na du’aa zake binafi peke yake na bila ya kuinua mikono.
[69] Abuu Umaamah ndiye Iyaas bin Tha’labah Al-Balawiyy na Swahibu wa Banu Haarithah wa wa Answaar. Yeye ni Swahaba, na alisimulia Hadiyth nyingi. Hakushiriki katika vita vya Badr kwa kuwa alikuwa akimuuguza Mama yake.
[70] Aayatul-Kursiyy ni ya katika Suwrah Al-Baqarah (2: 255).
[71] Hii inamanisha kuwa ataingia Jannah mara atakapofariki. Yaani, kinachomzuia kuingia Jannah ni kuweko kwake duniani.
[72] Umuhimu wa Aayatul-Kursiyy ni kutokana na Aayah hii kuweko Majina ‘Adhimu kabisa na Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) na pia yanaelezea Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ambayo Yeye Anapenda zaidi Apwekeshwe. Suwrah Ikhlaasw pia ina Majina na Sifa kama hizo.
[73] Suwrah Ikhlaasw ni Suwrah namba (112).
[74] Hadiyth hii Swahiyh na ‘adhimu inatuambia kuwa kauli zote na matendo yote ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni maelezo ya kutulengea, kutuongoza na kutuamrisha kutekeleza Swalaah kama ilivyoamrishwa katika Qur-aan na Sunnah. Juu ya hivyo, ni dalili kwamba Muislamu anapaswa lazima afuate Sunnah za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika ‘ibaadah zake zote katika kila kitendo na kauli. Hivyo basi matendo yote aliyoyatenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kauli zote alizotamka katika Swalaah ni waajib kwetu isipokuwa zile ambazo zimethibitishwa vinginevyo kwa dalili ya wazi kabisa.
[75] Endapo mtu yoyote, kwa sababu zisizokuwa za maradhi, hawezi kusimama wima, anaruhusiwa yeye kuswali huku amekaa, kama ambavyo mtu hufanya akiwa katika safari ya treni, ilimradi awe akikamilisha vizuri vitendo vya kurukuu na kusujudu. Akiwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu ya maradhi, lazima afanye hivyo kwa kuashiria na kuinama. Akiwa anataka kusujudu mathalani, ni lazima ainamishe kichwa chake mbali zaidi kuliko kuinamisha kwa ajili ya kurukuu. Hii imeripotiwa katika Hadiyth iliyosimuliwa na Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).