08-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Sajdatus-Sahw Na Nyingine
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلصَّلَاةِ
Kitabu Cha Swalaah
بَابُ سُجُودِ اَلسَّهْوِ وَغَيْرِهِ
08-Mlango Wa Sajdatus-Sahw[1] Na Nyingine
263.
عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ بُحَيْنَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَلَّى بِهِمُ الظُّهْرَ ، فَقَامَ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ اَلْأُولَيَيْنِ ، وَلَمْ يَجْلِسْ ، فَقَامَ اَلنَّاسُ مَعَهُ ، حَتَّى إِذَا قَضَى اَلصَّلَاةَ ، وَانْتَظَرَ اَلنَّاسُ تَسْلِيمَهُ ، كَبَّرَ وَهُوَ جَالِسٌ . وَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ ، قَبْلَ أَنْ يُسَلِّمَ ، ثُمَّ سَلَّمَ} أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ ، وَهَذَا لَفْظُ اَلْبُخَارِيِّ
وَفِي رِوَايَةٍ لمُسْلِمٍ :{يُكَبِّرُ فِي كُلِّ سَجْدَةٍ وَهُوَ جَالِسٌ وَسَجَدَ اَلنَّاسُ مَعَهُ ، مَكَانَ مَا نَسِىَ مِنَ الْجُلُوسِ}
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buhaynah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaswalisha Adhuhuri, akasimama mwisho wa Rakaa mbili za mwanzo na hakuketi chini.[2] Watu walimfuata wakasimama pamoja naye. Swalaah ilipomalizika, watu wakangojea atoe salaam. Akapiga Takbiyra hali akiwa ameketi. Huku akiwa amekaa, akasujudu Sajdah mbili kabla hajatoa salaam,[3], kisha akatoa salaam.” [Imetolewa na As-Sab’ah (Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad), na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipiga Takbiyra kwa kila Sajdah alipiga akiwa amekaa. Kisha alisujudu na Maamuma wote walisujudu pamoja naye kwa kufidia kule kuketi alikosahau.”
264.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ :{صَلَّى اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِحْدَى صَلَاتِي اَلْعَشِيِّ رَكْعَتَيْنِ ، ثُمَّ سَلَّمَ ، ثُمَّ قَامَ إِلَى خَشَبَةٍ فِي مُقَدَّمِ اَلْمَسْجِدِ ، فَوَضَعَ يَدَهُ عَلَيْهَا ، وَفِي اَلْقَوْمِ أَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ ، فَهَابَا أَنْ يُكَلِّمَاهُ ، وَخَرَجَ سَرَعَانُ اَلنَّاسِ ، فَقَالُوا : أَقُصِرَتْ . الصَّلَاةُ ، وَرَجُلٌ يَدْعُوهُ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ذَا اَلْيَدَيْنِ ، فَقَالَ : يَا رَسُولَ اَللَّهِ ، أَنَسِيتَ أَمْ قُصِرَتْ ؟ فَقَالَ : " لَمْ أَنْسَ وَلَمْ تُقْصَرْ " فَقَالَ : بَلَى ، قَدْ نَسِيتُ ، فَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ سَلَّمَ ، ثُمَّ كَبَّرَ ، فَسَجَدَ مِثْلَ سُجُودِهِ ، أَوْ أَطْوَلَ ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ فَكَبَّرَ ، ثُمَّ وَضَعَ رَأْسَهُ ، فَكَبَّرَ ، فَسَجَدَ مِثْلَ سُجُودِهِ ، أَوْ أَطْوَلَ . ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ وَكَبَّرَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ :{صَلَاةُ اَلْعَصْرِ}
وَلِأَبِي دَاوُدَ ، فَقَالَ :{أَصَدَقَ ذُو اَلْيَدَيْنِ ؟ " فَأَوْمَئُوا : أَيْ نَعَمْ}
وَهِيَ فِي " اَلصَّحِيحَيْنِ " لَكِنْ بِلَفْظِ : فَقَالُوا وَهِيَ فِي رِوَايَةٍ لَهُ :{وَلَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَقَّنَهُ اَللَّهُ تَعَالَى ذَلِكَ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Rakaa mbili za Swalaah mojawapo kati ya mbili za Al-‘Ashiyy (yaani Adhuhuri au Alasiri), kisha akatoa salaam. Akasimama karibu na kipande kimoja cha ubao kilichokuwa mbele ya Msikiti akaweka mkono wake juu yake. Abuu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) walikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo pale, wakaogopa kumsemesha lolote Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Wenye haraka wakatoka na wakasema Swalaah imefupishwa. Miongoni mwa watu hao alikuwepo mtu ambaye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimwita Dhul-Yadayn[4] (mtu mwenye mikono mirefu), akauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Umesahau au Swalaah imefupishwa? Akasema: “Sijasahau[5] wala haijafupishwa.” Akasema: “Bali umesahau.”[6], Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaswali Rakaa mbili zilizobakia, kisha akatoa salaam. Akapiga Takbiyra, akasujudu kama anavyosujudu Sajdah yake kawaida au ndefu zaidi. Kisha akainua kichwa chake na akatamka Takbiyra[7], akasujudu, akapiga Takbiyra, akasujudu kama Sajdah yake ya kawaida au ndefu zaidi. Akainua kichwa chake na akapiga Takbiyra.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Swalaah ya Alasiri.”
Na katika upokezi wa Abuu Daawuwd: “Je Dhul-Yadayn amesema kweli? Nao wakasema “Ndio” kwa kuashiria.
Na hiyo imo katika Swahiyhayn lakini kwa neno فَقالوا(wakasema). Na katika mapokezi yake (Abuu Daawuwd) mengine: “Hakusujudu hadi Allaah (تعالى) alipompa uhakika wa hilo.”
265.
وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَلَّى بِهِمْ ، فَسَهَا فَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ ، ثُمَّ تَشَهَّدَ ، ثُمَّ سَلَّمَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ ، وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaswalisha wao, akasahau kitu. Akasujudu Sajdah mbili, akasoma, kisha akatoa Tashahhud na salaam.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy aliipa daraja la Hasan, na Al-Haakim akaipa daraja la Swahiyh]
266.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ ، فَلَمْ يَدْرِ كَمْ صَلَّى أَثْلَاثًا أَوْ أَرْبَعًا ؟ فَلْيَطْرَحِ الشَّكَّ وَلْيَبْنِ عَلَى مَا اسْتَيْقَنَ ، ثُمَّ يَسْجُدُ سَجْدَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ يُسَلِّمَ ، فَإِنْ كَانَ صَلَّى خَمْساً شَفَعْنَ لَهُ صَلَاتَهُ ، وَإِنْ كَانَ صَلَّى تَمَامًا كَانَتَا تَرْغِيمًا لِلشَّيْطَانِ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akitia shaka katika Swalaah yake, hajui Rakaa ngapi ameswali, ni tatu au nne, basi aache mashaka na ajengee idadi aliyo na yakini nayo[8]. Kisha asujudu Sajdah mbili kabla hajatoa salaam. Ikiwa aliswali Rakaa tano, basi Swalaah yake itamuombea[9], na ikiwa aliswali Rakaa nne kamili zitakuwa zimemtahayarisha shaytwaan.” [Imetolewa na Muslim]
267.
وَعَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ:{صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا سَلَّمَ قِيلَ لَهُ : يَا رَسُولَ اَللَّهِ ، أَحَدَثَ فِي اَلصَّلَاةِ شَيْءٌ ؟ قَالَ : " وَمَا ذَلِكَ ؟ " . قَالُوا : صَلَّيْتَ كَذَا ، قَالَ : فَثَنَى رِجْلَيْهِ وَاسْتَقْبَلَ اَلْقِبْلَةَ ، فَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ ، ثُمَّ سَلَّمَ ، ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَيْنَا بِوَجْهِهِ فَقَالَ: " إِنَّهُ لَوْ حَدَثَ فِي اَلصَّلَاةِ شَيْءٌ أَنْبَأْتُكُمْ بِهِ ، وَلَكِنْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُم، أَنْسَى كَمَا تَنْسَوْنَ ، فَإِذَا نَسِيتُ فَذَكِّرُونِي ، وَإِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ فَلْيَتَحَرَّ اَلصَّوَابَ ، فلْيُتِمَّ عَلَيْهِ ، ثُمَّ لِيَسْجُدْ سَجْدَتَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ:{ فَلْيُتِمَّ ، ثُمَّ يُسَلِّمْ ، ثُمَّ يَسْجُدْ}
وَلِمُسْلِمٍ :{أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم سَجَدَ سَجْدَتَيْ اَلسَّهْوِ بَعْدَ اَلسَّلَامِ وَالْكَلَامِ}
وَلِأَحْمَدَ ، وَأَبِي دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيِّ ; مِنْ حَدِيثِ عَبْدِ بْنِ جَعْفَرٍ مَرْفُوعاً:{مَنْ شَكَّ فِي صَلَاتِهِ ، فَلْيَسْجُدْ سَجْدَتَيْنِ بَعْدَمَا يُسَلِّمُ} وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha, na alipotoa salaam aliulizwa: Ee Rasuli wa Allaah! Kuna jambo jipya limetokea katika Swalaah? Akasema: “Kitu gani?” Wakasema: “Umeswali Rakaa kadhaa.” Hapo akakunja miguu yake akaeleka Qiblah na akasujudu Sajdah mbili, akatoa salaam. Akaelekea watu akasema: “Endapo kitu kipya kingeletwa katika Swalaah, ningekujulisheni, lakini mimi ni mwana Aadam kama nyinyi,[10] ninasahau kama nyinyi mnavyosahau. Kwa hivyo nikisahau mnikumbushe. Na ikiwa yeyote kati yenu ana mashaka katika Swalaah yake, basi afuate lililo sawa na aikamilishe, kisha alete Sajdah mbili.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika mapokezi ya Al-Bukhaariy: “Akamilishe (Swalaah yake) kisha atoe salaam, kisha asujudu.”
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisujudu Sajdah mbili za Sahw baada ya kutoa salaam na kuongea.”
Na katika mapokezi ya Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kutokana Hadiyth Marfuw’ ya ‘Abdullaah bin Ja’far[11] ilisema: “Mwenye kutia shaka katika Swalaah yake, basi asujudu sijda mbili baada ya salaam.” [Akaisahihisha Ibn Khuzaymah]
268.
وَعَنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ {إِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ ، فَقَامَ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ ، فَاسْتَتَمَّ قَائِمًا ، فَلْيَمْضِ ، وَلْيَسْجُدْ سَجْدَتَيْنِ ، وَإِنْ لَمْ يَسْتَتِمْ قَائِمًا فَلْيَجْلِسْ وَلَا سَهْوَ عَلَيْهِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَابْنُ مَاجَهْ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ ، وَاللَّفْظُ لَهُ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ
Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Endapo mmoja wenu atapata mashaka akasimama katika Rakaa mbili, akikumbuka wakati ameshasimama basi aendelee[12] na asirejee kwenye kukaa, na asujudu katika Sajdah mbili. Lakini endapo hakuwahi kusimama wima kabisa basi akae na hana Sajdah mbili za kusahau.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na Ad-Daaraqutwniy na tamshi ni lake, kwa Isnaad dhaifu]
269.
وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ :{لَيْسَ عَلَى مَنْ خَلَفَ اَلْإِمَامَ سَهْوٌ فَإِنْ سَهَا اَلْإِمَامُ فَعَلَيْهِ وَعَلَى مَنْ خَلْفَهُ"} رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ وَالْبَيْهَقِيُّ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ
Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Sijdatus-sahw kwa anayeswali[13] nyuma ya Imaam, Imaam akisahau, ni juu yake na juu ya Imaam na wanaomfuata kuileta.” [Imetolewa na Al-Bazzaar na Al-Bayhaqiyy kwa Isnaad dhaifu]
270.
وَعَنْ ثَوْبَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {لِكُلِّ سَهْوٍ سَجْدَتَانِ بَعْدَمَا يُسَلِّمُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَابْنُ مَاجَهْ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ
Kutoka kwa Thawbaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila sahau ni Sajdah mbili baada ya salaam.[14]” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na Ibn Maajah kwa Isnaad dhaifu]
271.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {سَجَدْنَا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي : ( إِذَا اَلسَّمَاءُ اِنْشَقَّتْ ) ، و : ( اِقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ )} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulisujudu pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akisoma Suwrah:[15]
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾[16],
na
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ[17]
.” [Imetolewa na Muslim]
272.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {( ص ) لَيْسَتْ مِنْ عَزَائِمِ اَلسُّجُودِ ، وَقَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَسْجُدُ فِيهَا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutokwa kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Kusujudu wakati inaposomwa Suwrah Swaad[18] si katika ‘azaaaim (zilizoamrishwa kusujudu)[19], lakini nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisujudu katika Suwrah hiyo.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
273.
وَعَنْهُ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم سَجَدَ بِالنَّجْمِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) tena amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisujudu kwa kusoma Suwrah An-Najm.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
274.
وَعَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {قَرَأْتُ عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم اَلنَّجْمَ ، فَلَمْ يَسْجُدْ فِيهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Zayd bin Thaabit[20] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilisoma mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Suwrah An-Najm[21], na hakusujudu ndani yake.[22]” [Al-Bukhaariy, Muslim]
275.
وَعَنْ خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {فُضِّلَتْ سُورَةُ اَلْحَجِّ بِسَجْدَتَيْنِ} . رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ فِي " اَلْمَرَاسِيلِ "
وَرَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ مَوْصُولًا مِنْ حَدِيثِ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ ، وَزَادَ: {فَمَنْ لَمْ يَسْجُدْهُمَا ، فَلَا يَقْرَأْهَا} وَسَنَدُهُ ضَعِيفٌ
Kutoka kwa Khaalid bin Ma’daan[23] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Suwrah Al-Hajj[24] imefadhilishwa kwa kuwa na Sajdah mbili.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd katika Al-Maraasiyl]
Na waliipokea Ahmad na At-Tirmidhiy katika Hadiyth Mawsuwl kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir, akaongezea: “Asiyesujudu Sajdah hizo mbili (za Suwrah Al-Hajj), basi asiisome.” [Isnaad yake ni dhaifu]
276.
وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {يَا أَيُّهَا اَلنَّاسُ إِنَّا نَمُرُّ بِالسُّجُودِ فَمَنْ سَجَدَ فَقَدْ أَصَابَ ، وَمَنْ لَمْ يَسْجُدْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ} . رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ . وَفِيهِ: {إِنَّ اَللَّهَ تَعَالَى لَمْ يَفْرِضْ اَلسُّجُودَ إِلَّا أَنْ نَشَاءَ} . وَهُوَ فِي " اَلْمُوَطَّأِ
Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Enyi watu, katika visomo vyetu tunapita Aayah za kusujudu. Hivyo, anayesujudu amefanya sawa na asiyesujudu hana dhambi.[25]” [Imetolewa na Al-Bukhaariy] na ndani yake kuna: “Allaah (تعالى) Hakufaradhisha kusujudu, ila tukipenda.” [Ipo katika kitabu Al-Muwatwa’ cha Imaam Maalik]
277.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ عَلَيْنَا اَلْقُرْآنَ ، فَإِذَا مَرَّ بِالسَّجْدَةِ ، كَبَّرَ ، وَسَجَدَ ، وَسَجَدْنَا مَعَهُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ فِيهِ لِيِنٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitusomea Qur-aan, na kila alipofika mahali pa kusujudu alipiga Takbiyra na akasujudu, nasi tukasujudu pamoja naye.[26]” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad laini]
278.
وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا جَاءَهُ أَمْرٌ يَسُرُّهُ خَرَّ سَاجِداً لِلَّهِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ
Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa likimjia jambo lililomfurahisha anaporomoka, akisujudu.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy]
279.
وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {سَجَدَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَطَالَ اَلسُّجُودَ ، ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ وَقَالَ: " إِنَّ جِبْرِيلَ آتَانِي ، فَبَشَّرَنِي ، فَسَجَدْت لِلَّهِ شُكْرًا"} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf[27] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisujudu na akarefusha Sajdah, kisha akainua kichwa chake akasema: “Jibriyl amekuja na akanibashiria habari nzuri, kwa hiyo nimesujudu kumshukuru Allaah.” [Imetolewa na Ahmad, na akaisahihisha Al-Haakim]
280.
وَعَنْ اَلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ عَلِيًّا إِلَى اَلْيَمَنِ فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ قَالَ : فَكَتَبَ عَلِيٌّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ بِإِسْلَامِهِمْ ، فَلَمَّا قَرَأَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم اَلْكِتَابَ خَرَّ سَاجِدًا} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ وَأَصْلُهُ فِي اَلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma ‘Aliy kwenda Yaman. Msimuliaji akaitaja Hadiyth.[28] Alisema: “’Aliy akaandika barua kuhusu kusilimu kwao. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasoma barua hiyo akasujudu kumshukuru[29] Allaah (تعالى) kwa ajili ya hilo.” [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy na chanzo chake kimo katika Al-Bukhaariy]
[1] Sijdatus-sahw (Sajdah ya kusahau) huwa ni waajib iwapo mtu anayeswali anaongeza au anapunguza tendo fulani ndani ya Swalaah kwa makosa.
[2] Yapasa tuelewe kwamba tafsiri ya maneno ya kiarabu “Sahw” na “Nisyaan” ni “Kusahau”. Lakini “Sahw” inamaanisha kutenda mambo zaidi, na “Nisyaan” kwa kawaida inamaanisha sehemu ndogo ya taarifa. Lakini maneno yote haya mawili yanahesabika kuwa ni visawe, yaani moja ni sawasawa na jingine. Miongoni mwa ‘Ulamaa, hakuna hata mmoja anayelitumia neno “Nisyaan” kwa ajili ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Kwa hivyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamwe hakuwahi kuugua maradhi ya kuchanganyikiwa katika mambo yahusuyo kulingania Risala ya Uislamu. Angewezaje kuugua maradhi kama hayo wakati Allaah, Anasema katika Suwrah Al-A’laa:
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾
Tutakusomesha (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi hutoisahau
[Al-A’laa: 6].
‘Ulamaa waadilifu wanasema kuwa, matumizi ya neno ‘Sahw’ kwa ajili ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) inaruhusiwa kwa kuwa zipo rejea nyingi kutoka katika Hadiyth nyingi kuhusu kadhia hii. Maimaamu wote wane wanaafiki kwamba, mazingira yanayohusu kusahau (Sahw) kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yamethibitishwa. Hakuna ubaya katika hili; bali kuna niyyah njema (inamaanisha, usahau wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).
[3] Hadiyth hii inatufunza kuwa, mtu anaweza kufidia katika kuacha Tashahhud ya kwanza kwa kuleta Sijdatus-Sahw. Wengine wanasema iletwe kabla ya Salaam, na wengine wanasema iletwe baada ya Salaam. Hali zote hizi mbili zina ushahidi kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambaye hakuweka kanuni thabiti kuhusu hili. Katika kitabu cha Niyl Al-Awtwaar kuwa endapo kumeondoshwa jambo ndani ya Swalaah basi Sajdah iletwe baada ya Salaam. Wanazuoni wengine wanasema kuwa, ushahidi wa Sajdah kabla ya Salaam ni sahihi na sawa zaidi.
[4] Huyu Dhul-Yadayn ndiye Al-Khirbaq bin ‘Amr As-Sulaymiy wa kabila la Baniy Sulaym. Alifariki zama za Ukhalifa wa Mu’aawiyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Inasemekana pia kuwa alifia kule Dhi Khashab zama za Ukhalifa wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alikuwa na mikono mirefu mno; ndiyo maana akaitwa kiutani Dhul-Yadayn
[5] Kwa mujibu wa ufahamu wangu, sijaugua usahaulifu wala haikuja amri la Shariy’ah kwa Swalaah kufupishwa.
[6] Usahaulifu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa ndani ya Swalaah, juu ya ukweli kwamba alikuwa kazama sana katika tafakuri wakati akiomba Du’aa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) inaweza kueleweka kikweli kuwa ilikuwa tendo la haki na lilikuwa kwa niyyah njema. Kwanza tendo lile lilikuwa la kuuelimisha Ummah kimatendo juu ya mambo yanayohusu kusahau (Sahw) na ni yapi maagizo yake na jinsi ya kuyarekebisha pindi mtu yeyote atakabiliwa na hali kama ile. Pili, alitaka kuufundisha Ummah kwamba, juu ya heshima zake, hadhi, na nafasi ya juu sana ya kuwa zaidi kuliko viumbe wote, na yeye ni mwana Aadam, na amerithi hisia zote za kibinadamu kwa mfano kula, kunywa, kulala, kuamka, kutembea tembea, kwenda haja, kupata magonjwa na kuponywa, n.k. sifa zote zilizotajwa hapo juu zimedhihirishwa kwa nafsi yake. Yeye mwenyewe alilitaja jambo hili la busara na kama hilo litakalotajwa katika Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).
[7] Hadiyth hii inaweka wazi kwamba, pindi mtu akifikiri ana hakika amekamilisha Swalaah yake, anatoa Salaam, anaanza hata kuzungumza, na kisha ghafla anatambua kosa lake kwa kukumbuka yeye mwenyewe au mtu mwingine anamkumbusha kosa lake, Swalaah yake inabakia kuwa sahihi ilimradi tu aikamilishe mara moja.
[8] Hii ina maana mbili: Kwanza, kukiweko mashaka, mtu achukue namba ndogo zaidi. Kwa mfano, akiwa hana hakika ameshaziswali Rakaa tatu au nne, basi achukulie kuwa ni Rakaa tatu, kwani hii ni karibu zaidi na ukweli. Pili afanye lile ambalo ana hakika zaidi kuwa ndiyo sawa.
[9] Inamaanisha kuwa iwapo mtu kaziswali Rakaa tano, zitakuwa sita kwa kujumlisha na Sijdatus-Sahw. Inaonekana kutoka katika Hadiyth hii kuwa mtu sharti awe akichukulia namba ya Rakaa ya chini zaidi, kwani hiyo ndiyo huwa karibu zaidi na ukweli.
[10] Kwa mujibu wa rejea hii, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitumia maneno ya:
" إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُم "
((Mimi ni mwanadamu kama nyinyi).”
Hii huenda itawashangaza sana watu wasiomchukulia yeye kama mwana Aadam, na wanadai kuwa kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan:
إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ
“Hakika mimi ni mtu kama nyinyi;” [Fusw-Swilat: 6],
Unawania kuwanyamazisha tu washirikina wengi, ambapo ukweli ni kwamba watu wanaohusika hapa ni Waumini na wala sio washirikina.
[11] ‘Abdullaah bin Ja’far ndiye Abuu Ja’far ‘Abdullaah bin Ja’far bin Abiy Twaalib, na mama yake ni Asmaa’ bint ‘Umays. Huyu ni Mwislamu wa mwanzo kuzaliwa kule Abyssinia, na baba yake alitoka Al-Madiynah mnamo mwaka wa 7 A.H. alikuwa mcheshi sana, mwenye taqwa, na mkarimu sana. Alikuwa mkarimu kuliko wote miongoni mwa Waislamu. Alifariki Al-Madiynah mnamo mwaka 80 A.H. akiwa na umri wa miaka 80.
[12] Endapo mtu amesahau kusoma Tashahhud ya kati na akasimama wima kabisa, lazima aendelee na Swalaah yake. Lakini akiwa hakuwahi kusimama wima kikamilifu, achunguze kama yuko karibu na kusimama au karibu na kukaa. Akiwa karibu zaidi na kusimama, lazima asimame na alete Sijdatus-Sahw. Akiwa karibu na kukaa basi lazima akae chini kabisa, asome Tashahhud, na hana haja ya kuleta zile Sajdah mbili za Sahw.
[13] Hadiyth hii inatufunza kwamba, kuleta Sijdatus-Sahw huwa ni lazima kwa Muqtadi (mtu anayeswalishwa yaani Maamuma) pale tu ambapo Imaam kasahau, na wala siyo ikiwa yeye mtu mwenyewe kasahau.
[14] Hadiyth hii haina maana ya kuwa endapo mtu kafanya makosa mawili au manne, basi lazima alete Sijdatus-Sahw mbili kwa kila kosa. Inamaanisha tu kwamba, bila kujali aina na wingi wa makosa ambayo mtu kayafanya, Sajdah mbili tu zinatosheleza kufidia makosa yote. (Baadhi ya Wanazuoni wanaona kuwa Hadiyth hii inakubalika. Tazama Subulus-Salaam, (1/418-419), namba (319) na Irwaa’ Al-Ghaliyl, (2/47- 48) namba (339).
[15] Kama Sijdatut-Tilaawa (Sajdah ya kusoma baada ya Aayah maalumu za Qur-aan) itahesabika kama Mashruw’ (ya kuamrishwa), Sunnah (ya khiayri), au Waajib (ya kuwajibika), Wanazuoni wengi wanahesabu ile ni Sunnah, lakini Imaam Abuu Haniyfah amesema kuwa ni Waajib. Pia kuna kutofautiana maoni mtu sharti awe na wudhuu au hata akiwa hana wudhuu, anaweza kuleta Sajdah hii.
[16] Al-Inshiqaaq (84: 21)
[18] Swaad (38: 88)
[19] Kwa mujibu wa Imaam wengine, Sajdah hii ni lazima kama Sajdah zingine. Hadiyth hii inaashiria tu kwamba hii haikuamriwa kuwa iwe ni tendo la ‘Ibaadah; lakini Sajdah hii inatekelezwa mpaka sasa ikiwa kama ukumbusho wa mwenendo wa Nabiy Daawuwd (عليه السلام) .
[20] Zayd bin Thaabit ni Answaar na Najjaar, alipewa jina la utani la Abuu Sa’iyd au Abuu Khaarijah. Alikuwa muandishi mzuri wa Qur-aan, na alijua sana elimu ya Mirathi. Alipigana kwanza katika vita vya Al-Khandaq. Alikusanya Qur-aan zama za Ukhalifa wa Abuu Bakr, na aliinakili katika Ukhalifa wa ‘Uthmaan. Alijifunza maandishi ya Kiyahudi kwa nusu mwezi. Kwa amri ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na alikuwa akimuandikia na kumsomea maandishi hayo. Alifia Al-Madiynah mnamo mwaka wa 45 A.H. Imesemekana pia kuwa alikufa katika mwaka mwingine.
[21] An-Najm (53: 62).
[22] Hii ndiyo maana Wanazuoni wameihesabu Sijdatut-Tilaawah inayofanywa wakati wa kusoma Aayah maalumu za Qur-aan kuwa ni Sunnah, kwa sababu Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuitekeleza hii mara zote. Wakati mwingine alisujudu, na wakati mwingine hakuisujudu kabisa.
[23] Khaalid bin Ma’daan ndiye Abuu ‘Abdillaah Al-Kalaa’i kutoka Hims, Syria. Alikuwa miongoni mwa kizazi cha Taabi’iy (watu waliokuja baada ya Maswahaba) maarufu na wenye elimu na ujuzi sana. Alisema kuwa aliwahi kukutana na Maswahaba sabini wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alifariki mwaka 103 au 104 au 108 A.H
[24] Al-Hajj (22: 18 , 77).
[25] Hadiyth hii ni ushahidi wa wazi kuwa Sijdatut-Tilaawah siyo tendo la lazima. ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisema hivyo alipokuwa akiwahutubia Maswahaba waliokusanyika kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na hakuna hata mmoja kati yao aliyenena neno juu yake, hiyo ilithibitisha kuwa wote walibaki kimya kuhusu jambo hili.
[26] Hii inatufahamisha kuwa kusujudu ni waajib wa msomaji na hata msikilizaji, kwa sharti kwamba watu wawe ndani ya Swalaah. Na vivyo hivyo huwa kwa Sijdatut-Tilaawah (Sajdah ndani ya kisomo) na Sajdah Ash-Shukr.
[27] ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رضي الله عنه) ndiye aitwaye Abuu Muhammad Az-Zuhriy Al-Qarayshiy. Alisilimu mapema, akahamia Abyssinia mara mbili. Alishiriki katika vita vya Badr na vita vingine vikubwa. Huyu ni mmoja katika wale watu kumi walioahidiwa Jannah, na ni mmoja wa watu sita ambao ‘Umar (رضي الله عنه) aliwateua kuwa Makhalifa baada yake. Alitoa dinari elfu nne, kisha elfu arubaini, na kisha farasi mia tano na ngamia mia tano waliobebeshwa kama Swadaqah wakati Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akingali hai. Aliacha wasia wa bustani la thamani ya elfu mia nne kwa “Akina Mama wa Waumini.” Alikufa mnamo mwaka wa 34 A.H. na akazikwa Al-Baqi’.
[28] Imeripotiwa kuwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikwenda Yemen na watu wake mia tatu. Akawaita Wayemeni kusilimu. Jibu la Wayemeni lilikuwa kuwashambulia akina ‘Aliy kwa mishale, ‘Aliy alijibu mashambulizi yale, na wanaharakati wake maarufu 20 wakauliwa. Kukazuka mfarakano katika kambi ya ‘Aliy, na wengine wakakimbia kutoka uwanja wa vita. Wakaitwa kusilimu mara ya pili, nao wakakubali. ‘Aliy alikutana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kule Makkah wakati wa Hijjah, mwaka ule ule, baada ya kurejea salama toka katika ujumbe huo.