09-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaah Za Sunnah
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلصَّلَاةِ
Kitabu Cha Swalaah
بَابُ صَلَاةِ اَلتَّطَوُّعِ
09-Mlango Wa Swalaah Za Sunnah
281.
عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ كَعْبٍ الْأَسْلَمِيِّ رِضَى اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {قَالَ لِي اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم سَلْ . فَقُلْتُ : أَسْأَلُكَ مُرَافَقَتَكَ فِي اَلْجَنَّةِ . فَقَالَ: أَوَغَيْرَ ذَلِكَ ؟ ، قُلْتُ: هُوَ ذَاكَ ، قَالَ: " فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ بِكَثْرَةِ اَلسُّجُودِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Rabiy’ah bin Ka’b Al-Aslamiyy[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniambia: “Omba.” Nikasema: “Ninakuomba niwe pamoja nawe Jannah.” Aksema: “Hakuna zaidi ya hilo?” Nikasema: “Hilo tu basi.” Akasema: “Basi nisaidie mimi juu ya nafsi yako[2] kwa kukithirisha kusujudu.” (Yaani Swalaah)[3] [Imetolewa na Muslim][4]
282.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : {حَفِظْتُ مِنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم عَشْرَ رَكَعَاتٍ : رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ اَلظُّهْرِ ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْمَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْعِشَاءِ فِي بَيْتِهِ ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ اَلصُّبْحِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُمَا: {وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْجُمْعَةِ فِي بَيْتِهِ}
وَلِمُسْلِمٍ: {كَانَ إِذَا طَلَعَ اَلْفَجْرُ لَا يُصَلِّي إِلَّا رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nimehifadhi kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Rakaa kumi (za Sunnah): Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri, na mbili baada yake; Rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na Rakaa mbili baada ya ‘Ishaa nyumbani kwake; na Rakaa mbili kabla ya Alfajiri.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika mapokezi yao (Al-Bukhaariy, Muslim) mengine: “Rakaa mbili baada ya Ijumaa nyumbani kwake.”
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Haswali baada ya kutoka jua ila Rakaa mbili khafifu.”
283.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا : أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم { كَانَ لَا يَدَعُ أَرْبَعًا قَبْلَ اَلظُّهْرِ وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ اَلْغَدَاةِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Hakuacha Rakaa nne kabla ya Swalaah ya Adhuhuri, na Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri.[5]” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
284.
وَعَنْهَا قَالَتْ: {لَمْ يَكُنْ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى شَيْءٍ مِنْ اَلنَّوَافِلِ أَشَدَّ تَعَاهُدًا مِنْهُ عَلَى رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِمُسْلِمٍ: {رَكْعَتَا اَلْفَجْرِ خَيْرٌ مِنْ اَلدُّنْيَا وَمَا فِيهَا}
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuwahi kukaza niyyah ya kuswali Rakaa mbili za Swalaah yoyote ya khiari kuliko Rakaa mbili kabla ya Alfajiri. [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Rakaa mbili za Alfajiri ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.”
285.
وَعَنْ أُمِّ حَبِيبَةَ أُمِّ اَلْمُؤْمِنِينَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : سَمِعْتَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {مَنْ صَلَّى اِثْنَتَا عَشْرَةَ رَكْعَةً فِي يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ بُنِيَ لَهُ بِهِنَّ بَيْتٌ فِي اَلْجَنَّةِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ . وَفِي رِوَايَةٍ " تَطَوُّعًا"
وَلِلتِّرْمِذِيِّ نَحْوُهُ ، وَزَادَ: {أَرْبَعًا قَبْلَ اَلظُّهْرِ وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْمَغْرِبِ ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْعِشَاءِ ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلَاةِ اَلْفَجْرِ}
وَلِلْخَمْسَةِ عَنْهَا: {مَنْ حَافَظَ عَلَى أَرْبَعٍ قَبْلَ اَلظُّهْرِ وَأَرْبَعٍ بَعْدَهَا حَرَّمَهُ اَللَّهُ عَلَى اَلنَّارِ}
Kutoka kwa Ummu Habiybah[6] Mama wa Waumini (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nimemsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Mwenye kuswali Rakaa kumi na mbili mchana na usiku atajengewa nyumba Jannah kwa sababu ya hizo Rakaa.” [Imetolewa na Muslim]
Katika mapokezi mengine: “…Za Sunnah….”
Na At-Tirmidhiy alisimulia hivyo hivyo ila akaongezea: “Rakaa nne kabla ya adhuhuri na mbili baada yake; na Rakaa mbili baada ya Magharibi, na Rakaa mbili baada ya ‘Ishaa, na Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri.”
Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) wamepokea toka kwake (Ummu Habiybah): “Mwenye kuhifadhi (kuswali) Rakaa nne kabla ya Adhuhuri na nne baada yake, Allaah (تعالى) Atamharamishia Moto.”
286.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {رَحِمَ اَللَّهُ اِمْرَأً صَلَّى أَرْبَعًا قَبْلَ اَلْعَصْرِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Anamrehemu mtu anayeswali Rakaa nne kabla ya Alasiri.[7]” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy naye aliipa daraja la Hasan. Na Ibn Khuzaymah aliipa daraja la Swahiyh]
287.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ الْمُزَنِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {صَلُّوا قَبْلَ اَلْمَغْرِبِ ، صَلُّوا قَبْلَ اَلْمَغْرِبِ" ثُمَّ قَالَ فِي اَلثَّالِثَةِ : " لِمَنْ شَاءَ" كَرَاهِيَةَ أَنْ يَتَّخِذَهَا اَلنَّاسُ سُنَّةً} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
وَفِي رِوَايَةِ اِبْنِ حِبَّانَ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَلَّى قَبْلَ اَلْمَغْرِبِ رَكْعَتَيْنِ}
وَلِمُسْلِمٍ عَنْ أَنَسٍ قَالَ: {كُنَّا نُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ بَعْدَ غُرُوبِ اَلشَّمْسِ ، فَكَانَ صلى الله عليه وسلم يَرَانَا ، فَلَمْ يَأْمُرْنَا وَلَمْ يَنْهَانَا}
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mughaffal Al-Muzaniyy[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalini kabla ya Magharibi, swalini kabla ya Magharibi.”[9] Na mara ya tatu amesema: “Kwa anayetaka.” Kwa kuchelea watu wasiifanye kuwa ni Sunnah.[10] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Ibn Hibbaan: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Rakaa mbili kabla ya Magharibi.”
Na Muslim kupitia kwa Anas (رضي الله عنه) amesema: “Tulikuwa tukiswali Rakaa mbili baada ya kuchwa jua, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akituona naye hakutuamrisha wala hakutukataza.”
288.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يُخَفِّفُ اَلرَّكْعَتَيْنِ اَللَّتَيْنِ قَبْلَ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ ، حَتَّى إِنِّي أَقُولُ : أَقَرَأَ بِأُمِّ اَلْكِتَابِ ؟} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akihafifisha Rakaa mbili kabla ya Alfajiri hadi mimi ninasema: Amesoma Ummul-Kitaab? (Al-Faatihah).” [Al-Bukhaariy, Muslim]
289.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ : {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَرَأَ فِي رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ: ( قُلْ يَا أَيُّهَا اَلْكَافِرُونَ ) و ( قُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ )} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisoma:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾
Sema: “Enyi makafiri!”[11]
Na:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
“Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee.”[12] katika Rakaa mbili za Alfajiri.” [Imetolewa na Muslim]
290.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا صَلَّى رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ اِضْطَجَعَ عَلَى شِقِّهِ اَلْأَيْمَنِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Pindi Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa mbili za Alfajiri analalia ubavu wake wa kulia.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
291.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ اَلرَّكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ ، فَلْيَضْطَجِعْ عَلَى جَنْبِهِ اَلْأَيْمَنِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakaposwali mmoja wenu Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri, basi alalie upande wake wa kuume.”[13] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy naye aliipa daraja la Swahiyh]
292.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { صَلَاةُ اَللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى ، فَإِذَا خَشِيَ أَحَدُكُمْ اَلصُّبْحِ صَلَّى رَكْعَةً وَاحِدَةً ، تُوتِرُ لَهُ مَا قَدْ صَلَّى} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِلْخَمْسَةِ وَصَحَّحَهُ اِبْنِ حِبَّانَ: {صَلَاةُ اَللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مَثْنَى مَثْنَى"} وَقَالَ النَّسَائِيُّ : "هَذَا خَطَأٌ"
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah za usiku ni Rakaa mbili mbili, na mmoja wenu akikhofia Swalaah ya Alfajiri, basi aswali Rakaa moja ambayo itakuwa ni Witr ya Rakaa alizoswali.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Imepokewa Hadiyth na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad), ambayo Ibn Hibbaan aliipa daraja la Swahiyh: “Swalaah za (Sunnah za) usiku na mchana ni Rakaa mbili mbili.”
An-Nasaaiy amesema: “Hili ni kosa.[14]”[15]
293.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { أَفْضَلُ اَلصَّلَاةِ بَعْدَ اَلْفَرِيضَةِ صَلَاةُ اَللَّيْلِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah bora zaidi baada ya Swalaah ya faradhi ni Swalaah ya usiku.” [Imetolewa na Muslim]
294.
وَعَنْ أَبِي أَيُّوبَ اَلْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {اَلْوِتْرُ حَقٌّ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ ، مَنْ أَحَبَّ أَنْ يُوتِرَ بِخَمْسٍ فَلْيَفْعَلْ ، وَمَنْ أَحَبَّ أَنْ يُوتِرَ بِثَلَاثٍ فَلْيَفْعَلْ ، وَمَنْ أَحَبَّ أَنْ يُوتِرَ بِوَاحِدَةٍ فَلْيَفْعَلْ} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ ، وَرَجَّحَ النَّسَائِيُّ وَقْفَهُ
Kutoka kwa Abuu Ayyuwb Al-Anaswaariy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Witr ni haki juu ya kila Muislamu.[16] Anayependa kuswali kwa Rakaa tano, na afanye hivyo, na anayetaka kuiswali kwa Witr ya Rakaa tatu na afanye hivyo, na anayetaka kuiswali kwa Rakaa moja na afanye hivyo.[17]” [Imetolewa na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan, na An-Nasaaiy aliipa daraja la Mawquwf]
295.
وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {لَيْسَ اَلْوِتْرُ بِحَتْمٍ كَهَيْئَةِ اَلْمَكْتُوبَةِ ، وَلَكِنْ سُنَّةٌ سَنَّهَا رَسُولُ اَللَّهِ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Swalaah ya Witr siyo lazima kama Swalaah ya faradhi, lakini ni Sunnah iliyowekwa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).” [Imetolewa na An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy naye aliipa daraja la Hasan, na Al-Haakim akaisahihisha]
296.
وَعَنْ جَابِرٍ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَامَ فِي شَهْرِ رَمَضَانَ، ثُمَّ اِنْتَظَرُوهُ مِنْ اَلْقَابِلَةِ فَلَمَّا يَخْرُجْ ، وَقَالَ: " إِنِّي خَشِيتُ أَنْ يُكْتَبَ عَلَيْكُمْ اَلْوِتْرُ} رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali katika mwezi wa Ramadhwaan kisha Maswahaba zake wakamngojea usiku wa pili, lakini hakutoka (nyumbani kwake) akasema: Niliogopa isije[18] Witr ikafaradhishwa kwenu[19].” [Imetolewa na Ibn Hibbaan]
297.
وَعَنْ خَارِجَةَ بْنِ حُذَافَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِنَّ اَللَّهَ أَمَدَّكُمْ بِصَلَاةٍ هِيَ خَيْرٌ لَكُمْ مِنْ حُمُرِ اَلنَّعَمِ " قُلْنَا : وَمَا هِيَ يَا رَسُولَ اَللَّهِ ؟ قَالَ: " اَلْوِتْرُ ، مَا بَيْنَ صَلَاةِ اَلْعِشَاءِ إِلَى طُلُوعِ اَلْفَجْرِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
وَرَوَى أَحْمَدُ: عَنْ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ ، عَنْ أَبِيهِ ، عَنْ جَدِّهِ نَحْوَهُ
Kutoka kwa Khaarijah bin Hudhaafah[20] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Amekupeni Swalaah ya ziada iliyo bora kwenu kuliko ngamia wekundu.” Tukasema: “Ni ipi Ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: “Ni Witr iliyo baina ya Swalaah ya ‘Ishaa na Alfajiri.[21]” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Al-Haakim]
Na Ahmad amepokea Hadiyth inayofanana na hiyo kutoka kwa ‘Amr[22] bin Shu’ayb[23] kwa usimulizi wa baba yake aliyeipokea kutoka kwa babu yake ‘Amr.
298.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { اَلْوِتْرُ حَقٌّ، فَمَنْ لَمْ يُوتِرْ فَلَيْسَ مِنَّا} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَد لَيِّنٍ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
وَلَهُ شَاهِدٌ ضَعِيفٌ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عِنْدَ أَحْمَدَ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah[24] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amepokea kutoka kwa baba yake kuwa, Rasuli wa Allaa (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Witr ni haki kwa hivyo asiyeiswali si miongoni mwetu.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad laini, na akaisahihisha Al-Haakim]
Na ina ushahidi dhaifu kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) uliopokewa na Ahmad.
299.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {مَا كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَزِيدُ فِي رَمَضَانَ وَلَا فِي غَيْرِهِ عَلَى إِحْدَى عَشْرَةَ رَكْعَةً، يُصَلِّي أَرْبَعًا، فَلَا تَسْأَلْ عَنْ حُسْنِهِنَّ وَطُولِهِنَّ، ثُمَّ يُصَلِّي أَرْبَعًا، فَلَا تَسْأَلْ عَنْ حُسْنِهِنَّ وَطُولِهِنَّ، ثُمَّ يُصَلِّي ثَلَاثًا. قَالَتْ عَائِشَةُ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ، أَتَنَامُ قَبْلَ أَنْ تُوتِرَ ؟ قَالَ: "يَا عَائِشَةُ، إِنَّ عَيْنَيَّ تَنَامَانِ وَلَا يَنَامُ قَلْبِي".} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُمَا عَنْهَا: {كَانَ يُصَلِّي مِنْ اَللَّيْلِ عَشْرَ رَكَعَاتٍ، وَيُوتِرُ بِسَجْدَةٍ، وَيَرْكَعُ رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ، فَتِلْكَ ثَلَاثُ عَشْرَةَ}
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuzidisha Rakaa kumi na moja za Sunnah katika mwezi wa Ramadhwaan wala katika miezi mingine, Aliswali Rakaa nne, usiulize uzuri wake wala urefu wake. Kisha Rakaa nne usiulize uzuri na urefu wake. Kisha akswali Rakaa tatu za Witr.” ‘Aaishah akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Utalala usingizi kabla ya kuswali Witr?” Akasema: “Ee ‘Aaishah macho yangu hulala, lakini moyo wangu haulali.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika mapokezi ya Al-Bukhaariy na Muslim: “Alikuwa akiswali usiku Rakaa kumi, na anamalizia Witr kwa kuswali Rakaa moja, na alikuwa akiswali Rakaa mbili za Alfajiri, kwa hiyo hizo ni Rakaa kumi na tatu.[25]”
300.
وَعَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي مِنْ اَللَّيْلِ ثَلَاثَ عَشْرَةَ رَكْعَةً، يُوتِرُ مِنْ ذَلِكَ بِخَمْسٍ، لَا يَجْلِسُ فِي شَيْءٍ إِلَّا فِي آخِرِهَا}
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa kumi na tatu usiku, akiswali Witr Rakaa tano kati ya hizo, na hakai popote isipokuwa katika Rakaa ya mwisho.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
301.
وَعَنْهَا قَالَتْ: {مِنْ كُلِّ اَللَّيْلِ قَدْ أَوْتَرَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَانْتَهَى وِتْرُهُ إِلَى اَلسَّحَرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِمَا
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Katika usiku mzima Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameswali Witr, na Witr yake iliishia wakati wa suhuwr.” (Saa ya mwisho kabla ya Alfajiri)[26] [Al-Bukhaariy, Muslim]
302.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ اَلْعَاصِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {يَا عَبْدَ اَللَّهِ! لَا تَكُنْ مِثْلَ فُلَانٍ، كَانَ يَقُومُ مِنْ اَللَّيْلِ، فَتَرَكَ قِيَامَ اَللَّيْلِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniambia: “Ee ‘Abdullaah! Usiwe kama fulani alikuwa akiswali usiku akaacha kuswali usiku.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
303.
وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { أَوْتِرُوا يَا أَهْلُ اَلْقُرْآنَ، فَإِنَّ اَللَّهَ وِتْرٌ يُحِبُّ اَلْوِتْرَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Enyi watu wa Qur-aan! Swalini Swalaah ya Witr kwa sababu Allaah ni Witr (Mmoja)[27] na Anapenda Witr.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Khuzayma]
304.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {اِجْعَلُوا آخِرَ صَلَاتِكُمْ بِاللَّيْلِ وِتْرًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Fanyeni mwisho wa Swalaah zenu usiku ni Witr.”[28] [Al-Bukhaariy, Muslim]
305.
وَعَنْ طَلْقٍ بْنِ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {لَا وِتْرَانِ فِي لَيْلَةٍ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالثَّلَاثَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Twalq bin ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.” [Imetolewa na Ahmad, na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd), na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
306.
وَعَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُوتِرُ بِـ "سَبِّحِ اِسْمَ رَبِّكَ اَلْأَعْلَى"، و: "قُلْ يَا أَيُّهَا اَلْكَافِرُونَ"، و: "قُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ. وَزَادَ: {وَلَا يُسَلِّمُ إِلَّا فِي آخِرِهِنَّ}
وَلِأَبِي دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيِّ نَحْوُهُ عَنْ عَائِشَةَ وَفِيهِ: {كُلَّ سُورَةٍ فِي رَكْعَةٍ، وَفِي اَلْأَخِيرَةِ: "قُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ"، وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ}
Kutoka kwa Ubayy bin Ka’b[29] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akiswali Witr anasoma Suwrah Al-A’laa[30] katika Rakaa ya kwanza, na Suwrah Al-Kaafiruwn katika Rakaa ya pili na Suwrah Al-Ikhlaasw katika Rakaa ya tatu.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy] Naye akaongeza: “Wala hatoi Salaam isipokuwa mwishoni.”
Na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy wamepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma kila Suwrah moja katika kila Rakaa, na katika Rakaa ya mwisho alikuwa akisoma Al-Ikhlaasw pamoja na Al-Mu’awwidhatayn.[31]”
307.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {أَوْتِرُوا قَبْلَ أَنْ تُصْبِحُوا} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَلِابْنِ حِبَّانَ: {مَنْ أَدْرَكَ اَلصُّبْحَ وَلَمْ يُوتِرْ فَلَا وِتْرَ لَهُ }
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalini Witr kabla ya Alfajiri.” [Imetolewa na Muslim]
Na Ibn Hibbaan amepokea: “Mwenye kudiriki Alfajiri na hakuiswali Witr, basi hana Witr.”[32]
308.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَنْ نَامَ عَنْ اَلْوِتْرِ أَوْ نَسِيَهُ فَلْيُصَلِّ إِذَا أَصْبَحَ أَوْ ذَكَرَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kulala akakosa Witr au akaisahau, basi na aiswali asubuhi[33] au hapo atakapokumbuka.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy]
309.
وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَنْ خَافَ أَنْ لَا يَقُومَ مِنْ آخِرِ اَللَّيْلِ فَلْيُوتِرْ أَوَّلَهُ، وَمَنْ طَمِعَ أَنْ يَقُومَ آخِرَهُ فَلْيُوتِرْ آخِرَ اَللَّيْلِ، فَإِنَّ صَلَاةَ آخِرِ اَللَّيْلِ مَشْهُودَةٌ، وَذَلِكَ أَفْضَلُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuchelea kuamka mwishoni mwa usiku, basi aswali Witr mwanzoni mwa usiku, na mwenye azma ya kuamka mwisho mwa usiku basi aiswali Witr mwishoni mwa usiku, kwani Swalaah iswaliwayo mwishoni mwa usiku hushuhudiwa (Na Malaika) nayo ni bora zaidi.” [Imetolewa na Muslim]
310.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِذَا طَلَعَ اَلْفَجْرُ فَقَدْ ذَهَبَ كُلُّ صَلَاةِ اَللَّيْلِ وَالْوَتْرُ، فَأَوْتِرُوا قَبْلَ طُلُوعِ اَلْفَجْرِ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Alfajiri ikichomoza Swalaah zote za usiku pamoja na Witr zimeondoka, basi swalini Witr kabla ya kuchomoza Alfajiri.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy]
311.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي اَلضُّحَى أَرْبَعًا، وَيَزِيدُ مَا شَاءَ اَللَّهُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَلَهُ عَنْهَا: {أَنَّهَا سُئِلَتْ: هَلْ كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي اَلضُّحَى ؟ قَالَتْ: لَا، إِلَّا أَنْ يَجِيءَ مِنْ مَغِيبِهِ}
وَلَهُ عَنْهَا: {مَا رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي سُبْحَةَ اَلضُّحَى قَطُّ، وَإِنِّي لَأُسَبِّحُهَا}
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Dhwuhaa Rakaa nne[34] na akizidisha kiasi apendacho Allaah.” [Imetolewa na Muslim]
Katika upokezi wake (Muslim) mwingine: “’Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) aliulizwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Dhwuhaa? Akasema: “Laa isipokuwa awe kutoka safarini.”
Na katika upokezi wake (Muslim) mwingine: ’Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Sikumuona kamwe Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali Dhwuhaa, lakini mimi ninaiswali.”[35]
312.
وَعَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {صَلَاةُ اَلْأَوَّابِينَ حِينَ تَرْمَضُ اَلْفِصَالُ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
Kutoka kwa Zayd bin Arqam (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimuliwa kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Al-Awwaabiyn (wanaotubia) huswaliwa wakati ndama wa ngamia wanapochomwa na jua.”[36] [Imetolewa na At-Tirmidhiy]
313.
وَعَنْ أَنَسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَنْ صَلَّى اَلضُّحَى ثِنْتَيْ عَشْرَةَ رَكْعَةً بَنَى اَللَّهُ لَهُ قَصْرًا فِي اَلْجَنَّةِ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَاسْتَغْرَبَهُ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuswali Rakaa kumi na mbili za Dhwuhaa, Allaah atamjengea nyumba Jannah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na aliipa daraja la Ghaarib (ngeni)]
314.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {دَخَلَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْتِي، فَصَلَّى اَلضُّحَى ثَمَانِيَ رَكَعَاتٍ} رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ فِي "صَحِيحِهِ"
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliingia nyumbani kwangu akaswali Rakaa nane za Dhwuhaa.” [Imetolewa na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]
[1] Jina la utani la Rabiy’ah bin Ka’b Al-Aslamiyy ni Abuu Firaas Al-Madaniy. Alikuwa Swahaba alitoka katika Maswahaba wa Suffa. Alikuwa mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na alikuwa akimhudumia na kuongozana naye katika safari na nyumbani. Alifariki mnamo mwaka wa 3 A.H.
[2] Hii inatufunza kuwa, iwapo mtu anataka kumkurubia sana Allaah (سبحانه وتعالى) na Nabiy wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ni lazima aswali Swalaah za khiari (Nawaafil) kwa wingi.
[3] Hadiyth hii ina ushahidi kwa watu wale wanaohesabu kwamba kusujudu ni bora kabisa kuliko vitendo vingine vya Swalaah.
[4] Maana ya Hadiyth hii ni kwamba: “Mimi ninaomba kwa Allaah ili Akupe wewe kile unachokitaka, na nitamuomba Yeye Akupe wewe, lakini kwa kuwa ni kitu kikubwa sana kuomba hicho, basi ni sharti uswali Swalaah nyingi sana za khiari ili du’aa zangu zipate kukubalika.”
[5] Hadiyth hii inatuarifu kuhusu Rakaa nne za Sunnah kabla ya Swalaah ya faradhi wakati wa Adhuhuri. Imetajwa kupitia katika rejea ya ‘Abdullaah bin ‘Umar kuwa kuna Rakaa mbili za kuswaliwa kabla ya Swalaah ya faradhi. Kama ufafanuzi kuhusu hali hii, inasemwa kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa nne kama tendo la kuonyesha unyenyekevu na kufunguliwa kwa milango ya Jannah, na Rakaa mbili za Sunnah Msikitini. Wengine wanasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa nne nyumbani, na kuhusu Rakaa mbili ambazo alikuwa akiziswali Msikitini, hazikuwa zingine ila ni ile Swalaah ya Tahiyyatul-Masjid (Maamkizi ya Msikiti). Wengine wanasema kwamba, zote mbili zilikuwa ni Sunnah za Swalaah ya Adhuhuri, na kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mara nyingine alikuwa akiziswali Rakaa nne na mara nyingine mbili tu. Zote mbili ni sawa, lakini nne ni bora zaidi kuliko mbili. Hakuna tofauti ya maoni juu ya Rakaa mbili za Swalaah ya Alfajiri, kwa kuwa zinahesabika kuwa ni Sunnah Muakkadah (Sunnah iliyosisitizwa iliyoswaliwa mara kwa mara na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)). Imeripotiwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa haziachi hizo hata akiwa safarini, na kwa hivyo ni Waajib kwa msafiri kutoiacha Swalaah ya Witr ya usiku na pia Sunnah ya Swalaah ya Alfajiri.
[6] Ummu Habiybah anaitwa Ramla bint Abuu Sufyaan ni dada wa Mu’aawiyah. Alisilimu zamani, akahamia Abyssinia, na mumewe ‘Ubaydullaah bin Jahsh alirtadi na akawa Mkristo akafia huko. Kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuoa mnamo mwaka wa 7A.H. wakati yeye Ramla yuko kule, kisha akaja Al-Madiynah pamoja na wahamiaji wa Abyssinia. Alifariki mnamo mwaka wa 42, au 44 au 50 A.H.
[7] Hadiyth hii inatuarifu kuwa, desturi ya Rakaa nne kuswaliwa kabla ya Swalaah ya Alasiri pia ilikuwepo. Endapo mtu yeyote ataziswali hizo, atapata thawabu, lakini asipozswali hana lawama.
[8] ‘Abdullaah bin Mughaffal alikuwa miongoni mwa Aswhaab Ash-Shajara (Waliofanya bay’ah yaaani kula kiapo kuutetea Uislamu dhidi ya Maquraysh kule Hudaybiyah). Aliishi Al-Madiynah na baadae Basra. Alikuwa ni mmoja wa wale watu kumi waliopelekwa na ‘Umar Basra kuwafundisha watu Dini. Alikufa mnamo mwaka wa 60 A.H
[9] Kuna tofauti ya maoni miongoni mwa Wanazuoni kuhusu ubora wa kuswali Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Magharibi. Wale wanaokubali kusihi kwake wanachukua ushahidi kutoka katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim). Na wale wanaokanusha wanalinganisha na Hadiyth ya Abuu Daawuwd kuwa, alipoulizwa ‘Abdullaah bin ‘Umar juu ya hizo Rakaa mbili za kabla ya Swalaah ya Magharibi alisema hakuwahi kumuona yeyote akiziswali Rakaa hizo wakati Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa bado yu hai. Ukweli ni kuwa, usahihi unathibitishwa, lakini zisihesabike kuwa ni Sunnah Muakkadah (Zilosisitizwa), kwa sababu Anas, msimuliaji wa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema kuwa: “Kila Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipotuona sisi tunaswali Rakaa hizo, hakutuamrisha sisi kuwa lazima tuwe tukiziswali, wala hakutuamrisha sisi tuache tusiziswali.” Kwa hivyo inaonekana kuwa mtu anaweza kuziswali iwapo tu bado upo muda kabla ya Swalaah ya Jamaa lakini si sawa kuichelewesha Swalaah ya faradhi kwa ajili yake.
[10] Hadiyth hii inatuambia sisi kuwa, kujuzu na usahihi wa Rakaa hizo mbili kabla ya Swalaah ya Magharibi umethibitishwa.
[11] Suwrah Al-Kaafiruwn (109)
[12] Suwrah Al-Ikhlaasw (113)
[13] Kuna tofauti ya maoni juu ya tatizo hili ambalo ni la kipekee. Wengine wanakuhesabu kule kulala chini kuwa ni Waajib (Lazima); wengine wanasema ni Sunnah (khiari), na wapo wanaosema hiyo ni Mustahab (iliyopendekezwa). Kwa mujibu wa maoni ya Imaam Nawawi, ni Sunnah ambayo inaingia akilini pia. Ama ripoti ya Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kutokuafiki, ni sababu ya kuhusiana na Msikiti. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alilala chini hivyo nyumbani kwake tu. Vitendo vyote viwili vya kuswalia hizo Rakaa mbili Msikitini na akalala chini mle, havijathibitishwa.
[14] An-Nasaaiy anasema kuwa yale maneno ya
صَلَاةُ اَللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى
(Swalaah za usiku ni Rakaa mbili, mbili)
ni sawa, lakini maneno ya
صَلَاةُ اَللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مَثْنَى مَثْنَى
(Swalaah za usiku na za mchana ni Rakaa mbili, mbili) siyo sawa. Yaani kule kuongezwa kwa neno “Wan-nahaar” kunahisabika kuwa ni kwingi mno na kwa hivyo ni makosa, kwa mujibu wa maoni ya Imaam An-Nasaaiy.
[15] Maoni ya Imaam An-Nasaaiy kuhusu usimulizi huo na kukiri kuwa sio sahihi haukubaliki na hauna uthibitisho kwa kuwa Bayhaqiy amekiri kuwa ni sahihi. Tena Imaam Muslim, kwa kunukuu usimulizi wa ‘Aliy bin ‘Abdullaah Bariqi, msimuliaji wa Ahaadiyth za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliidhinisha kwa hiyo akauthibitisha usahihi wake. Imaam Al-Bukhaariy ameripoti Hadiyth nane kuhusu kadhia hii, na zote zinaiunga mkono. Hata hivyo, bila kujali kuwa Rakaa hizo zitaswaliwa mchana au usiku, ni ubora kuziswali hizo Nawaafil (Swala za khiari, yaani Sunnah) kwa Swalaah za Rakaa mbili mbili, na inaruhusika pia kuziswali kwa Swalaah za Rakaa nne.
[16] Hadiyth hii inatuarifu kwamba kuswali Witr ni lazima. Wale Ahnaaf (Wafuasi wa Imaam Abuu Haniyfah yaani Wahanafi) wanafuata fikra hizo hizo. Maimaam waliobaki na Wanazuoni wengi wengine wanaihesabu Witr kuwa ni Sunnah. Kwa hivyo Hadiyth inayofuata, ambayo ni imara zaidi katika mlolongo wa wapokezi, nayo inaunga mkono.
[17] Kwa mujibu wa ripoti, namba ya Rakaa za Swalaah ya Witr ni kati ya moja na kumi na moja. Wanazuoni wengine hupendelea kuswali Rakaa tatu. Wengi wa Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), wafuasi wao, Imaam Shaafi’, Imaam Ahmad, na Imaam Maalik, wanatambua na wanapendelea Rakaa moja.
[18] Kwa mujibu wa Hadiyth hii, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Swalaah ya Taraawiyh katika Jamaa kwa mausiku matatu tu katika maisha yake yote, na kuiswali Swalaah hii kila siku katika mwezi wa Ramadhwaan, kulianzishwa baadaye na Khalifa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
[19] Hadiyth hii inaelezea Swalaah ya Taraawiyh ambayo wingi wa Rakaa zake ni kumi na moja, na Witr nayo wingi wa Rakaa zake ni kumi na moja pia. ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) aliripoti kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuswali zaidi ya Rakaa kumi na moja za Witr mnamo mwezi wa Ramadhwaan na katika miezi mingine. ‘Umar (رضي الله عنه) alimuamrisha ‘Ubay bin Ka’b (رضي الله عنه) kuswalisha Rakaa nane za Taraawiyh. Kwa hivyo inaweza kusemwa kuwa watu walikuwa wakiswali kwa uwingi Rakaa ishirini (20) pia mnamo zama za ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) (ilimradi hii pia ilithibitishwa na mlolongo wa wapokezi). Lakini hakuna Hadiyth Swahiyh inayojulikana chanzo inayothibitisha Rakaa ishirini za Taraawiyh.
[20] Khaarijah bin Hudhaafah ni Qurayshi na ni ‘Adawi ambaye alifananishwa na wapanda farasi elfu moja. ‘Amr bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuomba ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), ampelekee wapanda farasi elfu tatu, lakini yeye akampelekea watu watatu tu, nao ni Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam, Al-Miqdaad bin Al-Aswad, na Khaarijah. Alikuwa Qadhi kule Misri kwa ‘Amr bin Al-‘Aasw na akauliwa kule mnamo Ramadhwaan mwaka 40 A.H, na mmoja wa Khawaarij aliyemdhania kuwa yeye ndiye ‘Amr bin Al-‘Aasw. Hii ilikuwa wakati ule wale Makhawaarij walipokula njama ya kuwaua ‘Amr, ‘Aliy na Mu’aawiyah.
[21] Kwa mujibu wa Hadiyth hii, wakati wa ‘Ishaa ni kutokea wakati wa Swalaah ya ‘Ishaa mpaka wakati wa dalili za kwanza za Alfajiri. Wakati wake mzuri ni usiku zaidi; lakini iwapo mtu hatokuwa na hakika kuwa atawahi kuamka toka usingizini, basi ni ubora aiswali Witr mara baada ya kuiswali ‘Ishaa.
[22] ‘Amr huyu ndiye Abuu Ibraahiym ‘Amr bin Shu’ayb bin ‘Abdillaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw As-Sahmiy Al-Qurayshiy Al-Madaniy, aliyelowea Twaaif. An-Nasaaiy alimthibitisha kuwa ni wa kutegemewa. Alikufa mnamo mwaka 118 A.H.
[23] Shu’ayb alikuwa mmoja wa Taabi’iyn wa kutegemewa. Inasemekana kuwa babake Muhammad alikufa zama za utoto wake; kwa hivyo babu yake ‘Abdullaah bin ‘Amr yule Swahaba maarufu ndiye alimlea. Na imethibitika kuwa yeye aliisikia hasa hii Hadiyth kutoka kwake. Kwa hiyo hii siyo Munqatwi’ wala siyo Mursal, bali ni Mutwassil ambayo haiendi chini ya daraja la Hassan.
[24] ‘Abdullaah bin Buraydah ndiye Abuu Sahl, Qadhi wa Marw, ambaye alikuwa ni mmoja wa Taabi’iyn wa daraja la tatu wa kutegemewa sana na maarufu kabisa. Alifia Marw mnamo mwaka wa 115 A.H.
[25] Kuna tofauti ya maoni iwapo Swalaah ya Tahajjud (Swalaah ya usiku wa manane) ina Rakaa kumi na moja au kumi na tatu. Kumi na moja zimeafikiwa, lakini kumi na tatu zina mtafaruku. Ukweli ni kwamba, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wakati mwingine aliswali kumi na moja za Tahajjud kujumlisha na Witr na wakati mwingine kumi na tatu.
[26] Suwhur inajulikana pia ni kula daku.
[27] Inamaanisha Sifa za Allaah, yaani Yeye ni wa Kipekee, na “Hakuna chochote kinachofanana na Yeye”
[28] Kwa mujibu wa simulizi zingine, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa mbili za Sunnah (Naafil) baada ya Swalaah ya Witr kwa hivyo amesamehewa. Wengine wanasema kuwa mtu ni bora aswali Rakaa mbili za Swalaah ya Sunnah katika sehemu ya mwisho ya usiku, akiwa ameshaswali Swalaah ya Witr sehemu ya mwanzo ya usiku. Endapo ataswali Witr katika sehemu ya mwisho ya usiku, basi hana haja ya kuswali hiyo Swalaah ya Sunnah.
[29] Ubayy bin Ka’b ni Answaar, na ni Khazraj, alipewa jina la utani la Abu Al-Mundhir. Alikuwa ndiye Sayyid wa Wanazuoni wa Qur-aan na alikuwa mmoja wa waandishi wa Wahy. Na alikuwa pia mmoja wa watu walioikusanya Qur-aan na alitoa Fatwa (uamuzi wa kisheria) zama za uhai wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alishiriki katika vita vya ‘Aqabah, Badr na vita vilivyofuatia hivi. Mwaka wa kufa kwake kumetofautiana; wengine wakisema alikufa mnamo mwaka wa 19, au 20, au 22, au 30, au 32, au 33 A.H
[30] Suwrah Al-A’laa (87).
[31] Suwrah za Al-Mu’awwidhatayn ni: Al-Falaq (113) na An-Naas (114).
[32] Hadiyth hii inatuambia kuwa wakati wa Witr unakwisha kunapopambazuka; na Hadiyth hii inamaanisha kuwa Witr anayoiswali mtu huku wakati huo umepita basi inakuwa haikuswaliwa kwa mujibu wa Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Haimaanishi kuwa iwapo mtu hakuwahi kuswali Witr kabla ya Alfajiri basi asiiswali kabisa. Tukio moja linalowahusu Maswahaba linasimuliwa na Hadiyth isemayo kwamba, wakati fulani alilala na akachelewa kuamka. Akamtuma Mtumwa wake akaone kama Swalaah ya Jamaa imekwisha kuswaliwa; na Mtumwa akarejea na kumjibu kuwa imekwisha kuswaliwa. Baada ya kuambiwa hivi, aliswali hiyo Witr kwanza, kisha Sunnah na kisha akaiswali Swalaah ya faradhi ya Alfajiri. Kwa hivyo inaeleweka kwamba, mtu asipowahi kuswali Witr katika wakati wake, ni lazima aiswali kama kadhaa baadaye. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisisitiza kuwa Witr ni lazima iswaliwe katika wakati wake bila kukosa. Na aliagiza kuwa kwa wale waliokuwa na shaka ya kuwahi kuamka kuiswali, basi waiswali usiku (kabla hawajalala). Kwa hivyo akamuamrisha Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) aswali Witr usiku.
[33] Ieleweke kwamba, mtu akiikosa Swalaah kwa sababu ya kusahau au usingizi, hatotiwa hatiani na atapata thawabu na kama aliiswali Swalaah ile kwa wakati wake; lakini imekatazwa kwenda kulala wakati ambao unakaribia Swalaah fulani. Itokeapo kwamba hili linatokea kwa bahati mbaya na kwa hali ambayo yeye hawezi kuiepuka, basi hatolaumiwa.
[34] Ifahamike kwamba Ishraaq, Swalaatul-Awwaabiyn, na Dhwuhaa ni majina tofauti yanayomaanisha Swalaah zile zile za kabla ya Swalaah ya Adhuhuri. Wakati wa Swalaah hiyo ni mara baada ya kuchomoza jua na huendelea hadi robo moja ya mchana. Idadi ya chini kabisa ya Rakaa za Dhwuhaa ni Rakaa mbili, na idadi ya juu kabisa ni Rakaa kumi na mbili. Inayopendelewa ni Rakaa nne, ambayo inaungwa mkono na Hadiyth za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Ikumbukwe pia kuwa Swalaah hii ni Sunnah ya Manabiy waliotangulia kwa vile walikuwa wakiziswali hizo katika zama zao. Kwa hivyo Swalaah hii ni Sunnah na Mustahabb (inayopendekezwa). Ama ‘Umar (رضي الله عنه) kuiita Swalaah hii ni Bid’ah (uzushi), inamaanisha tu kuwa ikiwa mtu atazowea kuiswali hiyo kila siku zote, yaweza kuhesabika ni Bid’ah kwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuiswali siku zote.
[35] Ingawa Hadiyth hii na hizo mbili zilizoitangulia zinaonekana kupingana, zinaonyesha tu kuwa Swalaah ya Dhwuhaa ni Swalaah ya khiari kama inavyothibitishwa na Wanazuoni wa Hadiyth.
[36] Hadiyth hii inaonyesha kuwa wakati mzuri kuliko wote wa Swalaah ya Dhwuhaa ni kabla tu ya saa sita mchana.