Kusikiliza Qur-aan Badala Ya Muziki
Kusikiliza Qur-aan Badala Ya Muziki
SWALI:
ASALAAM ALEIKUM! Mimi Huwa Napenda Sana Kusikiliza Qur-aan Wakati Nataka Kulala Na Huwa Naisikiliza Mpaka Napata Usingizi Ilhali Inaendelea Kusomwa.
Sababu Kubwa Ni Kwamba Kulala Bila Kusikiliza Kitu Kama Vile Music Au Qur-aan Au Mawaidha Huwa Nachelewa Kupata Usingizi. Sasa Nimeamua Kusikiliza Qur-aan Ili Nisipate Kusikiliza Sikiliza Music Wakati Wa Kulala, JE HII INAFAA AU HAIFAI?. Allah Awaongoze Katika Kulijibu Swali Langu, Waadha Asalaam Aleikum.
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Wa ‘Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh
Kusikiliza Qur-aan ni jambo linalompasa kila Muislamu na ni katika ‘amali njema zenye faida na thawabu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾
Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A’raaf: 204]
Ama kusikiliza muziki ni katika maasi yaliyoharamishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hivyo basi ni dhambi kusikiliza muziki.
Kwa hiyo kuacha muziki na kuielekea Qur-aan ni jambo jema uliloamua kufanya.
Soma zaidi kwenye kiungo hapa chini kuhusu Uharamu Wa Muziki:
Hukmu Ya Muziki Katika Qur-aan Na Sunnah - Ewe Upendaye Nyimbo Na Muziki, Haujafika Wakati Wa Kuogopa Adhabu Kali Za Allaah?
Muziki Inayowekwa Katika Nashiyd Na Qaswiydah Inafaa? Anavutiwa Nazo Sana
Na Allaah Anajua zaidi