02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Hajj: Mlango Wa Mawaaqiyt (Vituo Vya Ihraam)
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْحَجِّ
Kitabu Cha Hajj
بَابُ اَلْمَوَاقِيتِ
02-Mlango Wa Mawaaqiyt (Vituo Vya Ihraam)
590.
عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَقَّتَ لِأَهْلِ اَلْمَدِينَةِ: ذَا الْحُلَيْفَةِ، وَلِأَهْلِ اَلشَّامِ: اَلْجُحْفَةَ، وَلِأَهْلِ نَجْدٍ: قَرْنَ اَلْمَنَازِلِ، وَلِأَهْلِ اَلْيَمَنِ: يَلَمْلَمَ، هُنَّ لَهُنَّ وَلِمَنْ أَتَى عَلَيْهِنَّ مِنْ غَيْرِهِنَّ مِمَّنْ أَرَادَ اَلْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ، وَمَنْ كَانَ دُونَ ذَلِكَ فَمِنْ حَيْثُ أَنْشَأَ، حَتَّى أَهْلُ مَكَّةَ مِنْ مَكَّةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichagua vituo vifuatavyo kwa ajili ya kuingia katika Ihraam:[1] (a) Dhal-Hulayfah[2] kwa watu wa Al-Madiynah. (b) Al-Juhfah kwa watu wa Syria. (c) Qarna Al-Manaazil kwa watu wa Najd. Na (d) Yalamlam kwa watu wa Yaman. Kwa hivyo vituo hivyo ni kwa kanda hizo na kwa watu wa maeneo mengine wanaokwenda huko kwa niyyah ya Hijjah na ‘Umrah. Mahala ambapo watu wa Makkah wanatakiwa kuingia katika Ihraam ni pale wanapotokea; hata wakazi wa Makkah huvalia Ihraam mumo humo Makkah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
591.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا: {أَنَّ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَقَّتَ لِأَهْلِ اَلْعِرَاقِ ذَاتَ عِرْقٍ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ
وَأَصْلُهُ عِنْدَ مُسْلِمٍ مِنْ حَدِيثِ جَابِرٍ إِلَّا أَنَّ رَاوِيَهُ شَكَّ فِي رَفْعِهِ
وَفِي اَلْبُخَارِيِّ: {أَنَّ عُمَرَ هُوَ اَلَّذِي وَقَّتَ ذَاتَ عِرْقٍ}
وَعِنْدَ أَحْمَدَ، وَأَبِي دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيِّ: عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَقَّتَ لِأَهْلِ اَلْمَشْرِقِ: اَلْعَقِيقَ}
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichagua Dhaata ‘Irq[3] iwe ndio pahala pa kuingia katika Ihraam watu wa Iraaq.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]
Asili yake ni Hadiyth ya Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) katika upokezi wa Muslim, lakini msimulizi wake ana shaka kama ni Marfuw’.
Na katika Swahiyh Al-Bukhaariy imeelezwa kuwa: “’Umar ndiye aliyeteua Dhaata ‘Irq.”
Ahmad, Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy wameipokea hii kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichagua Al-‘Aqiyqa[4] iwe kituo cha watu wa mashariki kuingia katika Ihraam zao.”
[1] Maana ya Ihraam kilugha: ni haraam, yaani ni jambo lililoharamishwa.
Kiistilahi: Ni kuweka niyyah ya kuingia katika ‘ibaadah ya Hajj au ‘Umrah; kwa maana mtu anapoazimia kutekeleza ‘Umrah au Hajj akaanza taratibu zake Miyqaat na kutamka Talbiyah, huwa ameshaingia katika Ihraam na kwa hivyo kuna baadhi ya vitendo huwa ni haraam kwake kuvitenda, hadi atakapomaliza taratibu zake na akaitengua na Ihraam .
Na pia wanaume hutakiwa wavae mavazi maalumu ya shuka mbili nyeupe zinazovaliwa na wanaohiji au wenye kutekeleza ‘Umrah wanaponuia. Wanaweza kuvaa mavazi hayo kabla ya kufika Miyqaat kuanza safari ya kuenda kutekeleza Hijjah au ‘Umrah au wanaweza kuyavalia katika Miyqaat.
[2] Dhal Hulayfah ni jina la mahali ambapo ni umbali wa kilomita 15 kutoka Al-Madiynah. Na “Najd” kiistilahi ni “Ardhi iliyonyanyuliwa juu”, na ni ardhi kati ya Tihama na Iraq. “Qarna Al-Manaazil” ni pahala mkabala na Twaaif ambapo sasa panaitwa “Saail”. “Yalamlam” ni jina la mlima ulioko umbali wa safari ya siku mbili kutoka Yaman. Hivi ndivyo vituo vilivyopangiwa Hujaji waingie katika hali zao za Ihraam. Watu wanaoishi nje ya mipaka hii, lazima waingie katika hali ya Ihraam katika vituo hivi, na watu wanaoishi ndani ya mipaka hii waingie katika hali za Ihraam kutokea majumbani kwao wanakoishi. Siyo lazima kwao kuenda hadi kwenye Miyqaat (vituo vilivyotajwa hapo juu) kuingia Ihraam.
[3] Ukweli ni kuwa Dhaat ‘Irq ilichaguliwa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwenyewe kuwa Miyqaat kwa ajili ya Hujaji watokao Iraaq, na uamuzi wa hili ulifanyika wakati wa Hajjatul-Wadaa’ (Hijjah ya mwisho au Hijjah ya kuaga aliyoifanya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kabla ya kufa kwake). Ameipokea Al-Bukhaariy kwamba: “’Umar ndiye aliyeichagua Dhaat ‘Itq”, ambapo ukweli ni kwamba ‘Umar aliitangaza tu.
[4] Al-‘Aqiyqa ni jina la mahala ambapo ni mkabala na Dhaat-‘Irq