05-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Hajj: Mlango Wa Sifa Za Hijjah Na Kuingia Makkah

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْحَجِّ

Kitabu Cha Hajj

 

بَابُ صِفَةِ اَلْحَجِّ وَدُخُولِ مَكَّةَ

05-Mlango Wa Sifa Za Hijjah Na Kuingia Makkah

 

 

 

 

607.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏حَجَّ، فَخَرَجْنَا مَعَهُ، حَتَّى أَتَيْنَا ذَا الْحُلَيْفَةِ، فَوَلَدَتْ أَسْمَاءُ بِنْتُ عُمَيْسٍ، فَقَالَ: " اِغْتَسِلِي وَاسْتَثْفِرِي بِثَوْبٍ، وَأَحْرِمِي " وَصَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏فِي اَلْمَسْجِدِ، ثُمَّ رَكِبَ اَلْقَصْوَاءَ‏ حَتَّى إِذَا اِسْتَوَتْ بِهِ عَلَى اَلْبَيْدَاءِ أَهَلَّ بِالتَّوْحِيدِ: " لَبَّيْكَ اَللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ اَلْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ ".‏

حَتَّى إِذَا أَتَيْنَا اَلْبَيْتَ اِسْتَلَمَ اَلرُّكْنَ، فَرَمَلَ ثَلَاثًا وَمَشَى أَرْبَعًا، ثُمَّ أَتَى مَقَامَ إِبْرَاهِيمَ فَصَلَّى، ثُمَّ رَجَعَ إِلَى اَلرُّكْنِ فَاسْتَلَمَهُ.‏

ثُمَّ خَرَجَ مِنَ اَلْبَابِ إِلَى اَلصَّفَا، فَلَمَّا دَنَا مِنَ اَلصَّفَا قَرَأَ: " إِنَّ اَلصَّفَا وَاَلْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اَللَّهِ " " أَبْدَأُ بِمَا بَدَأَ اَللَّهُ بِهِ " فَرَقِيَ اَلصَّفَا، حَتَّى رَأَى اَلْبَيْتَ، فَاسْتَقْبَلَ اَلْقِبْلَةَ ‏ فَوَحَّدَ اَللَّهَ وَكَبَّرَهُ وَقَالَ: " لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ اَلْمُلْكُ، وَلَهُ اَلْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ  وَحْدَهُ  أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ، وَهَزَمَ اَلْأَحْزَابَ وَحْدَهُ ".‏ ثُمَّ دَعَا بَيْنَ ذَلِكَ ‏ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ نَزَلَ إِلَى اَلْمَرْوَةِ، حَتَّى ‏ اِنْصَبَّتْ قَدَمَاهُ فِي بَطْنِ اَلْوَادِي  سَعَى حَتَّى إِذَا صَعَدَتَا ‏ مَشَى إِلَى اَلْمَرْوَةِ ‏ فَفَعَلَ عَلَى اَلْمَرْوَةِ، كَمَا فَعَلَ عَلَى اَلصَّفَا … ‏ فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ.‏ وَفِيهِ:

فَلَمَّا كَانَ يَوْمَ اَلتَّرْوِيَةِ تَوَجَّهُوا إِلَى مِنَى، وَرَكِبَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَصَلَّى بِهَا اَلظُّهْرَ، وَالْعَصْرَ، وَالْمَغْرِبَ، وَالْعِشَاءَ، وَالْفَجْرَ، ثُمَّ مَكَثَ قَلِيلاً حَتَّى طَلَعَتْ اَلشَّمْسُ، فَأَجَازَ حَتَّى أَتَى عَرَفَةَ، فَوَجَدَ اَلْقُبَّةَ قَدْ ضُرِبَتْ لَهُ بِنَمِرَةَ  فَنَزَلَ بِهَا.‏

حَتَّى إِذَا زَاغَتْ اَلشَّمْسُ أَمَرَ بِالْقَصْوَاءِ، فَرُحِلَتْ لَهُ، فَأَتَى بَطْنَ اَلْوَادِي، فَخَطَبَ اَلنَّاسَ.‏

ثُمَّ أَذَّنَ ثُمَّ أَقَامَ، فَصَلَّى اَلظُّهْرَ، ثُمَّ أَقَامَ فَصَلَّى اَلْعَصْرَ، وَلَمْ يُصَلِّ بَيْنَهُمَا شَيْئًا.‏

ثُمَّ رَكِبَ حَتَّى أَتَى اَلْمَوْقِفَ فَجَعَلَ بَطْنَ نَاقَتِهِ اَلْقَصْوَاءِ إِلَى الصَّخَرَاتِ، وَجَعَلَ حَبْلَ اَلْمُشَاةِ ‏ بَيْنَ يَدَيْهِ وَاسْتَقْبَلَ اَلْقِبْلَةَ، فَلَمْ يَزَلْ وَاقِفاً حَتَّى غَرَبَتِ اَلشَّمْسُ، وَذَهَبَتْ اَلصُّفْرَةُ قَلِيلاً، حَتَّى غَابَ اَلْقُرْصُ، وَدَفَعَ، وَقَدْ شَنَقَ لِلْقَصْوَاءِ اَلزِّمَامَ حَتَّى إِنَّ رَأْسَهَا لَيُصِيبُ مَوْرِكَ رَحْلِهِ، وَيَقُولُ بِيَدِهِ اَلْيُمْنَى: " أَيُّهَا اَلنَّاسُ، اَلسَّكِينَةَ، اَلسَّكِينَةَ "، كُلَّمَا أَتَى حَبْلاً ‏ أَرْخَى لَهَا قَلِيلاً حَتَّى تَصْعَدَ.‏

حَتَّى أَتَى اَلْمُزْدَلِفَةَ، فَصَلَّى بِهَا اَلْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ، بِأَذَانٍ وَاحِدٍ وَإِقَامَتَيْنِ، وَلَمْ يُسَبِّحْ ‏ بَيْنَهُمَا شَيْئًا، ثُمَّ اِضْطَجَعَ حَتَّى طَلَعَ اَلْفَجْرُ، فَصَلَّى ‏ اَلْفَجْرَ، حِينَ ‏ تَبَيَّنَ لَهُ اَلصُّبْحُ بِأَذَانٍ وَإِقَامَةٍ ثُمَّ رَكِبَ حَتَّى أَتَى اَلْمَشْعَرَ اَلْحَرَامَ، فَاسْتَقْبَلَ اَلْقِبْلَةَ، فَدَعَاهُ، وَكَبَّرَهُ، وَهَلَّلَهُ ‏ فَلَمْ يَزَلْ وَاقِفًا حَتَّى أَسْفَرَ جِدًّا.‏

فَدَفَعَ قَبْلَ أَنْ تَطْلُعَ اَلشَّمْسُ، حَتَّى أَتَى بَطْنَ مُحَسِّرَ فَحَرَّكَ قَلِيلاً، ثُمَّ سَلَكَ اَلطَّرِيقَ اَلْوُسْطَى اَلَّتِي تَخْرُجُ عَلَى اَلْجَمْرَةِ اَلْكُبْرَى، حَتَّى أَتَى اَلْجَمْرَةَ اَلَّتِي عِنْدَ اَلشَّجَرَةِ، فَرَمَاهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ، يُكَبِّرُ مَعَ كُلِّ حَصَاةٍ مِنْهَا، مِثْلَ حَصَى اَلْخَذْفِ، رَمَى مِنْ بَطْنِ اَلْوَادِي، ثُمَّ اِنْصَرَفَ إِلَى اَلْمَنْحَرِ، فَنَحَرَ، ثُمَّ رَكِبَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏فَأَفَاضَ إِلَى اَلْبَيْتِ، فَصَلَّى بِمَكَّةَ اَلظُّهْرَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ مُطَوَّلاً

Kutoka kwa Jaabir Bin ‘Abdullaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihiji na tulikwenda pamoja naye. Tulipofika Dhul-Hulayfah, Asmaa bint ‘Umays alijifungua mtoto. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Wewe oga, kisha uzingirishe nguo sehemu zako za siri, na uvae Ihraam.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaswali Msikitini na kisha akampanda Al-Qasw-waa,[1] na aliposimama wima na yeye Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa mgongoni kwake, kule Al-Baydaa,[2] akapaza sauti yake akitangaza Tawhiyd akasema:

لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ ، لَبَّيْكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ ، إِنَّ الْحَمْدَ ، وَالنِّعْمَةَ ، لَكَ وَالْمُلْكَ ، لاَ شَرِيكَ لَكَ

Labbayka-Allaahumma Labbayk. Labbayka laa shariyka Laka Labbayk. Innal-Hamda Wan-Ni'imata Laka wal-Mulk laa shariyka Lak.

"Nimekuitikia Ee Allaah nimekuitika, nimekuitika Huna mshirika nimekuitika, hakika Himdi na Neema na Ufalme ni Vyako Huna mshirika."

Mpaka tukafika katika Al-Ka’bah,[3] akagusa kona,[4] akakimbia mara tatu kuizunguka Nyumba,[5] akatembea mara nne kuizunguka Nyumba. Kisha akaja Maqaam  Ibraahiym na kuswali pale. Kisha akarejea kwenye kona akaigusa tena. Kisha akatoka nje mlangoni akakaribia Asw-Swafaa, akasoma:

إِنَّ اَلصَّفَا وَاَلْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اَللَّهِ

 

 “Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwaa ni katika alama za Allaah.” [Al-Baqarah (2: 158)] Akasema: “Nnaanza kile Alichoanza nacho Allaah”. Kwa hivyo akapanda Swafaa mpaka akaiona Ka’bah, kisha akageukia Qiblah akatangaza Tawhiyd ya Allaah na Akamkabbir akasema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ اَلْمُلْكُ، وَلَهُ اَلْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ  وَحْدَهُ  أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ، وَهَزَمَ اَلْأَحْزَابَ وَحْدَهُ

 

Laa Ilaaha Illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku Walahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr.  Laa Ilaaha Illa-Allaahu Wahdahu, Anjaza wa'dahu wa-Naswara 'Abdahu wa-hazamal-ahzaaba Wahdahu

“Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ni Wake Ufalme na Himdi ni Zake, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.  Hapana mwabudiwa wa haki Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi peke Yake.”

 Kisha akaomba du’aa baina yake peke yake kama hivyo mara tatu. Kisha akashuka hadi Al-Marwah. Alipoteremka hadi miguu yake ikakanyaga bonde alikimbia, hadi akapanda, alitembea hadi Al-Marwah. Kama alivyofanya Asw-Swafaa na msimuliaji akataja Hadiyth hivi: “Ilipofika Yawm At-Tarwiyah[6] wakaelekea Minaa,[7] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikwenda akaswali Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, ‘Ishaa na Alfajiri. Kisha akakaa kidogo, hadi jua likachomoza, akaenda hadi ‘Arafah akakuta ameshajengewa hema Namirah.[8]

Akashuka, jua lilipopinduka, aliamurisha Al-Qasw-waa aletwe, na alipowekewa matandiko, alikwenda chini bondeni kuhutubia watu. Kisha kukaadhiniwa na kukimiwa, akaswali Swalaah ya Adhuhuri, kisha ikakimiwa na akaswali Alasiri, bila kuswali Swalaah nyingine yoyote baina yake.

Kisha akampanda ngamia wake, akaja mahala pa kisimamo, akauelekeza tumbo la ngamia wake Al-Qasw-waa kwenye mawe,[9] na akatengeneza njia ya wanaoenda kwa miguu. mbele yake. Alielekea Qiblah, akabaki hivyo mpaka jua likazama mwanga wa manjano ukatoweka kidogo, umbo  mviringo la jua lilikuwa limekwisha potea. Alianza kuenda haraka na kuvuta kwa nguvu hatamu ya Al-Qasw-waa huku akiashiria kwa mkono wake wa kuume kwa watu na kusema: “Nyamazeni kimya, nyamazeni kimya” Na kila alipopita pahala palipoinuka juu, alilegeza hatamu ili ngamia aweze kupanda.

Alipofika Al-Muzdalifah aliswali Magharibi na ‘Ishaa kwa Adhana moja tu na Iqaama mbili,[10] hakuleta tasbiyh baina yake.[11] Kisha akalala mpaka alfajiri akaswali Alfajiri kwa Adhana moja na Iqaama moja. Kisha akampanda ngamia wake hadi akafika Al-Mash’aral-Haraam.[12] Akaelekea Qiblah, akamuomba Allaah, akamtukuza na kumpwekesha, na akabakia kusimama hadi kukang’aa sana.

Kisha akaondoka haraka haraka, kabla ya jua halijachomoza, hadi akafika katika bonde la Muhassir.[13] Akaharakisha kidogo kisha akafuata barabara ya katikati[14] ambayo ilikuwa ikitokezea katika Jamrah[15] kubwa, akafika hadi Jamrah jirani na mti. Akatupa vijiwe saba huku akipiga Takbiyr kwa kila kijiwe anachokitupa. Na kila kijiwe kilikuwa kidogo kama kokwa ya tende. Akavitupa bondeni, kisha akaenda mahala pa kuchinja akachinja. Baada ya hivyo, Rasuli wa Allaah akampanda ngamia wake na kuondoka haraka haraka hadi kwenye Al-Ka’bah,[16] na akaswali Adhuhuri Makkah.” [Imetolewa na Muslim kupitia Hadiyth ndefu]

 

 

 

608.

وَعَنْ خُزَيْمَةَ بْنِ ثَابِتٍ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏كَانَ إِذَا فَرَغَ مِنْ تَلْبِيَتِهِ فِي حَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ سَأَلَ اَللَّهَ رِضْوَانَهُ وَالْجَنَّةَ وَاسْتَعَاذَ‏ بِرَحْمَتِهِ مِنَ اَلنَّارِ} رَوَاهُ اَلشَّافِعِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Khuzaymah bin Thaabit (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kila alipomaliza Talbiyah yake, katika Hijjah au katika ‘Umrah, alikuwa akimuomba Allaah Radhi Zake na Jannah, na aliomba kujilinda na moto kwa Rahmah Yake.”[17] [Imetolewa na Ash-Shaafi’iyy kwa Isnaad dhaifu ya wapokezi]

 

 

 

609.

وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{نَحَرْتُ هَاهُنَا، وَمِنًى كُلُّهَا مَنْحَرٌ، فَانْحَرُوا فِي رِحَالِكُمْ، وَوَقَفْتُ هَاهُنَا وَعَرَفَةُ كُلُّهَا مَوْقِفٌ، وَوَقَفْتُ هَاهُنَا وَجَمْعٌ كُلُّهَا مَوْقِفٌ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nimechinja hapa, na Minnaa yote ni machinjio, kwa hiyo chinja hapo unapoishi. Nimesimama hapa, na ‘Arafah yote ni mahala pa kusimama. Nimesimama hapa na Jam’ (Al-Muzdalifah) yote ni mahala pa kusimama.”[18] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

610.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏لَمَّا جَاءَ إِلَى مَكَّةَ دَخَلَهَا مِنْ أَعْلَاهَا، وَخَرَجَ مِنْ أَسْفَلِهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuja Makkah, aliingilia juu na akatokea chini.”[19] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

611.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّهُ كَانَ لَا يَقْدُمُ مَكَّةَ إِلَّا بَاتَ بِذِي طُوَى حَتَّى يُصْبِحَ وَيَغْتَسِلَ، وَيَذْكُرُ ذَلِكَ عِنْدَ اَلنَّبِيِّ‏ صلى الله عليه وسلم} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Yeye (Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)) Alikuwa haji Makkah bila kulala pale Dhiy Twuwaa[20] hadi alfajiri, na kisha alioga. Alikuwa akisema hivyo ndivyo alivyofanya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

612.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّهُ كَانَ يُقَبِّلُ اَلْحَجَرَ اَلْأَسْوَدَ وَيَسْجُدُ عَلَيْهِ} رَوَاهُ اَلْحَاكِمُ مَرْفُوعًا، وَالْبَيْهَقِيُّ مَوْقُوفًا

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Alikuwa akilibusu Hajar Al-Aswad (Jiwe Jeusi) na akisujudu juu yake.”[21] [Imetolewa na Al-Haakim kama ni Marfuw’, na Al-Bayhaqiyy kama Mawquwf]

 

 

 

613.

وَعَنْهُ قَالَ: أَمَرَهُمْ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏{أَنْ يَرْمُلُوا ثَلَاثَةَ أَشْوَاطٍ وَيَمْشُوا أَرْبَعًا، مَا بَيْنَ اَلرُّكْنَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema tena: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaamrisha wakimbie mizunguko mitatu,[22] na watembee mizunguko minne,[23] kati ya nguzo mbili.”[24] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

614.

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا طَافَ الطَّوَافَ الأَوَّلَ خَبَّ ثَلاَثًا وَمَشَى أَرْبَعًا"

 وَفي رِواية: رَاَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا طَافَ فِي الْحَجِّ وَالْعُمْرَةِ أَوَّلَ مَا يَقْدَمُ فَإِنَّهُ يَسْعَى ثَلاَثَةَ أَطْوَافٍ بِالْبَيْتِ ثُمَّ يَمْشِي أَرْبَعَةً   متفق عليه

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Yeye alipokuwa akitufu Nyumba (Al-Ka’bah), alikuwa akikimbia mizunguko mitatu na akitembea mizunguko mine.”

Na katika Riwaayah nyingine inasema: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufu katika Hijjah au ‘Umrah mara alipowasili. Alikuwa akikimbia mizunguko mitatu na akawa anatembea mizunguko mine kuzunguka Nyumba.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

615.

وَعَنْهُ قَالَ: {لَمْ أَرَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يَسْتَلِمُ مِنْ اَلْبَيْتِ غَيْرَ اَلرُّكْنَيْنِ اَلْيَمَانِيَيْنِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Sikuwahi kumuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akigusa kitu chochote katika Nyumba (Al-Ka’bah) ile isipokuwa zile nguzo za Yamani.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

616.

وَعَنْ عُمَرَ‏ رضى الله عنه {أَنَّهُ قَبَّلَ اَلْحَجَرَ اَلْأَسْوَدَ فَقَالَ: إِنِّي أَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ لَا تَضُرُّ وَلَا تَنْفَعُ، وَلَوْلَا أَنِّي رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يُقَبِّلُكَ مَا قَبَّلْتُكَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Alibusu jiwe jeusi akasema: “Ninajua wewe ni jiwe hudhuru wala hunufaishi. Nisingemuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akikubusu, nisingekubusu.”[25] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

617.

وَعَنْ أَبِي اَلطُّفَيْلِ رضى الله عنه قَالَ: {رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يَطُوفُ بِالْبَيْتِ وَيَسْتَلِمُ اَلرُّكْنَ بِمِحْجَنٍ مَعَهُ، وَيُقْبِّلُ اَلْمِحْجَنَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Atw-Twufayl[26] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akizunguka Nyumba (Al-Ka’bah) huku anagusa kona kwa Mihjan[27] ambayo alikuwa nayo na kuibusu Mihjan.”[28] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

618.

وَعَنْ يَعْلَى بْنَ أُمَيَّةَ رضى الله عنه قَالَ: {طَافَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏مُضْطَبِعًا بِبُرْدٍ أَخْضَرَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Ya’laa bin Umayyah[29] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufu akiwa amevaa joho la Kiyemeni rangi ya kijani chini ya kwapa yake ya kuume na ncha yake ikiwa juu ya bega lake la kushoto.”[30] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

619.

وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ يُهِلُّ مِنَّا اَلْمُهِلُّ فَلَا يُنْكِرُ عَلَيْهِ، وَيُكَبِّرُ مِنَّا اَلْمُكَبِّرُ فَلَا يُنْكِرُ عَلَيْهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Miongoni mwetu wapo waliopaza sauti katika Talbiyah bila kukatazwa, na miongoni mwetu wapo waliopiga Takbiyra bila kukatazwa.”[31] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

620.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {بَعَثَنِي رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏فِي اَلثَّقَلِ، أَوْ قَالَ فِي اَلضَّعَفَةِ مِنْ جَمْعٍ‏ بِلَيْلٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alinituma (kuenda Minnaa) pamoja na wanawake na watoto, au amesema niende na watu dhaifu wa familia yake[32] kutoka Jam’ wakati wa usiku.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

621.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {اِسْتَأْذَنَتْ سَوْدَةُ رَسُولَ اَللَّهِ‏ صلى الله عليه وسلم ‏لَيْلَةَ اَلْمُزْدَلِفَةِ: أَنْ تَدْفَعَ قَبْلَهُ، وَكَانَتْ ثَبِطَةً ‏تَعْنِي: ثَقِيلَةً‏ فَأَذِنَ لَهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِمَا

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Sawdah[33] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) aliomba ruhusa kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ili atangulie usiku wa Muzdalifah, alikuwa mnene, kwa hivyo akaruhusiwa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

622.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ لَنَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{لَا تَرْمُوا اَلْجَمْرَةَ حَتَّى تَطْلُعَ اَلشَّمْسُ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَفِيهِ اِنْقِطَاعٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Alituambia kuwa: “Msitupe vijiwe pale Jamrah hadi jua lichomoze.”[34] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na kuna kukatika]

 

 

 

623.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {أَرْسَلَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏بِأُمِّ سَلَمَةَ لَيْلَةَ اَلنَّحْرِ، فَرَمَتِ اَلْجَمْرَةَ قَبْلَ اَلْفَجْرِ، ثُمَّ مَضَتْ فَأَفَاضَتْ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَإِسْنَادُهُ عَلَى شَرْطِ مُسْلِمٍ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtanguliza Umm Salamah usiku kabla ya siku ya kuchinja, na akatupa vijiwe kule Jamrah kabla ya alfajiri. Kisha akaharakisha kuenda Makkah na akatufu.”[35] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na wapokezi wake wanakidhi masharti ya Muslim]

 

 

 

624.

وَعَنْ عُرْوَةَ بْنِ مُضَرِّسٍ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{مَنْ شَهِدَ صَلَاتَنَا هَذِهِ ‏يَعْنِي: بِالْمُزْدَلِفَةِ‏ فَوَقَفَ مَعَنَا حَتَّى نَدْفَعَ، وَقَدْ وَقَفَ بِعَرَفَةَ قَبْلَ ذَلِكَ لَيْلاً أَوْ نَهَارًا، فَقَدْ تَمَّ حَجُّهُ وَقَضَى تَفَثَهُ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa ‘Urwah bun Mudhwarris[36] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuhudhuria Swalaah yetu hapa Muzdalifah na anasimama nasi hadi tuondoke kuenda Minnaa, na akisimama ‘Arafah kabla mchana au usiku, basi Hijjah yake imekamilika,[37] na ametekeleza Tafathah (taratibu)[38] zake.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Khuzaymah]

 

 

 

625.

وَعَنْ عُمَرَ‏ رضى الله عنه قَالَ: {إِنَّ اَلْمُشْرِكِينَ كَانُوا لَا يُفِيضُونَ حَتَّى تَطْلُعَ اَلشَّمْسُ، وَيَقُولُونَ: أَشْرِقْ ثَبِيرُ‏ وَأَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏خَالَفَهُمْ، ثُمَّ أَفَاضَ قَبْلَ أَنْ تَطْلُعَ اَلشَّمْسُ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Washirikina walikuwa hawarejei kutoka Muzdalifah hadi jua lichomoze na wanasema: Liache jua liangaze juu ya Thabiyr.[39] Kwa hivyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitofautiana na hao washirikina kwa kurejea upesi kutoka Muzdalifah kabla jua kuchomoza.”[40] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

626.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ وَأُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمْ قَالَا: {لَمْ يَزَلِ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏يُلَبِّي حَتَّى رَمَى جَمْرَةَ اَلْعَقَبَةِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas na Usaamah bin Zayd[41] (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمْ) wamesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliendelea kupaza sauti yake katika Talbiyah hadi alipotupa vijiwe[42] katika Jamratal-‘Aqabah.”[43] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

627.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّهُ جَعَلَ اَلْبَيْتَ عَنْ يَسَارِهِ، وَمِنًى عَنْ يَمِينِهِ، وَرَمَى اَلْجَمْرَةَ بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ‏ وَقَالَ: هَذَا مَقَامُ اَلَّذِي أُنْزِلَتْ عَلَيْهِ سُورَةُ اَلْبَقَرَةِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nyumba ikiwa kushoto na Minnaa kuume kwake, alitupa vijiwe saba katika Jamrah amesema: “Hiki ni kisimamo ambacho imeteremkia Suwrah Al-Baqarah.”[44] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

628.

وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه قَالَ: {رَمَى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏اَلْجَمْرَةَ يَوْمَ اَلنَّحْرِ ضُحًى، وَأَمَّا بَعْدَ ذَلِكَ فَإِذَا زَادَتْ اَلشَّمْسُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitupa vijiwe katika Siku ya Kuchinja mchana kabla ya adhuhuri, na baada ya hapo akatupa wakati jua limepinduka.”[45] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

629.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّهُ كَانَ يَرْمِي اَلْجَمْرَةَ اَلدُّنْيَا، بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ، يُكَبِّرُ عَلَى أَثَرِ كُلِّ حَصَاةٍ، ثُمَّ يَتَقَدَّمُ، ثُمَّ يُسْهِلُ، فَيَقُومُ فَيَسْتَقْبِلُ اَلْقِبْلَةَ، فَيَقُومُ طَوِيلاً، وَيَدْعُو وَيَرْفَعُ يَدَيْهِ، ثُمَّ يَرْمِي اَلْوُسْطَى، ثُمَّ يَأْخُذُ ذَاتَ اَلشِّمَالِ فَيُسْهِلُ، وَيَقُومُ مُسْتَقْبِلَ اَلْقِبْلَةِ، ثُمَّ يَدْعُو فَيَرْفَعُ يَدَيْهِ وَيَقُومُ طَوِيلاً، ثُمَّ يَرْمِي جَمْرَةَ ذَاتِ اَلْعَقَبَةِ مِنْ بَطْنِ اَلْوَادِي وَلَا يَقِفُ عِنْدَهَا، ثُمَّ يَنْصَرِفُ، فَيَقُولُ: هَكَذَا رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يَفْعَلُهُ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Alikuwa akitupa vijiwe saba katika Jamrah ya karibu,[46] akipiga Takbiyra kila anapotupa. Kisha alikuwa anasogea mbele, anakuenda mpaka ndani ya bonde.[47] Na baada ya kusimama akiwa kaelekea Qiblah akiomba du’aa na kuinua mikono yake akasimama kwa muda mrefu, akitupa vijiwe katika Jamrah ya kati. Kisha aligeukia kushoto na kuenda ndani zaidi kwenye bonde na baada ya kusimama akielekea Qiblah akaomba du’aa na kusimama kwa muda mrefu, akatupa vijiwe katika Jamrah Al-‘Aqabah kutoka bondeni chini, lakini hakusimama karibu yake. Kisha aliondoka na kusema: “Hivi ndivyo nilivyomuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akifanya.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

630.

وَعَنْــهُ ،‏ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: " اَللَّهُمَّ ارْحَمِ اَلْمُحَلِّقِينَ " قَالُوا: وَالْمُقَصِّرِينَ يَا رَسُولَ اَللَّهِ.‏ قَالَ فِي اَلثَّالِثَةِ: " وَالْمُقَصِّرِينَ "} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema:

اَللَّهُمَّ ارْحَمِ اَلْمُحَلِّقِينَ

Allaahumma Irham Al-Muhalliqiyna

(Ee Allaah warehemu ambao wamenyoa)

 

Watu wakapendekeza kuwa Na wale waliopunguza nywele zao[48] Ee Rasuli wa Allaah! Kisha akasema katika mara ya tatu:

وَالْمُقَصِّرِينَ

 “Na waliopunguza.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

631.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوِ بْنِ اَلْعَاصِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏وَقَفَ فِي حَجَّةِ اَلْوَدَاعِ، فَجَعَلُوا يَسْأَلُونَهُ، فَقَالَ رَجُلٌ: لَمْ أَشْعُرْ، فَحَلَقْتُ قَبْلَ أَنْ أَذْبَحَ.‏ قَالَ: " اِذْبَحْ وَلَا حَرَجَ " فَجَاءَ آخَرُ، فَقَالَ: لَمْ أَشْعُرْ، فَنَحَرْتُ قَبْلَ أَنْ أَرْمِيَ، قَالَ: " اِرْمِ وَلَا حَرَجَ " فَمَا سُئِلَ يَوْمَئِذٍ عَنْ شَيْءٍ قُدِّمَ وَلَا أُخِّرَ إِلَّا قَالَ: " اِفْعَلْ وَلَا حَرَجَ "} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bun Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisimama katika Hijja ya kuaga, wakawa watu wanamuuliza. Mtu mmoja akasema: “Sikujua, nimenyoa nywele kabla sijachinja.” Akasema: “Chinja tu kwani hakuna tatizo.” Mwingine akasema: “Sikujua nimechinja mnyama kabla sijatupa vijiwe.” Akasema: “Vitupe tu, kwani hakuna tatizo.” Hakuulizwa kitu chochote ambacho kilifanywa kabla au baada ya wakati wake maalumu siku ile bila kusema: “Fanya tu, kwani hakuna tatizo.”[49] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

632.

وَعَنْ اَلْمِسْوَرِ بْنِ مَخْرَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏نَحَرَ قَبْلَ أَنْ يَحْلِقَ، وَأَمَرَ أَصْحَابَهُ بِذَلِكَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Al-Miswar bin Makhramah[50] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichinja kabla ya kunyoa, na akaamuru Swahaba zake kufanya vivyo hivyo.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

633.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{إِذَا رَمَيْتُمْ وَحَلَقْتُمْ فَقَدَ حَلَّ لَكُمْ اَلطِّيبُ وَكُلُّ شَيْءٍ إِلَّا اَلنِّسَاءَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkishatupa vijiwe na kunyoa, manukato ni halali na kila kitu kingine imeruhusiwa isipokuwa wanawake.”[51] [Imetolewa na Ahmad, na Abuu Daawuwd kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

634.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {لَيْسَ عَلَى اَلنِّسَاءِ حَلْقٌ، وَإِنَّمَا يُقَصِّرْنَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kunyoa si wajibu kwa wanawake,[52] lakini wanapunguza (nywele zao).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

 

 

635.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّ اَلْعَبَّاسَ بْنَ عَبْدِ اَلْمُطَّلِبِ رضى الله عنه ‏ اِسْتَأْذَنَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏أَنْ يَبِيتَ بِمَكَّةَ لَيَالِيَ مِنًى، مِنْ أَجْلِ سِقَايَتِهِ، فَأَذِنَ لَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “’Abbaas bin ‘Abdul-Mutwalib aliomba ruhusa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) abakie Makkah katika usiku ambao alitakiwa awe Minaa, kwa sababu ya wadhifa wake wa kugawia watu maji, naye akamruhusu.”[53] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

636.

وَعَنْ عَاصِمِ بْنِ عَدِيٍّ‏ رضى الله عنه {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏أَرْخَصَ لِرُعَاة اَلْإِبِلِ فِي اَلْبَيْتُوتَةِ عَنْ مِنًى، يَرْمُونَ يَوْمَ اَلنَّحْرِ، ثُمَّ يَرْمُونَ اَلْغَدِ لِيَوْمَيْنِ، ثُمَّ يَرْمُونَ يَوْمَ اَلنَّفْرِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa ‘Aaswim bin ‘Adiyy[54] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaruhusu wachungaji wa ngamia wasibakie usiku kucha Minaa na kutupa vijiwe katika Siku ya Kuchinja kisha watupe siku ya pili yake na siku ya tatu yake pamoja, kisha watupe katika siku ya watu kutawanyika kutoka Minaa.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]

 

 

 

637.

وَعَنْ أَبِي بِكْرَةَ رضى الله عنه قَالَ:{خَطَبَنَا رَسُولُ اَللَّهِ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَوْمَ اَلنَّحْرِ.‏.‏.‏} اَلْحَدِيثَ.‏ مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alituhutubia Siku ya Kuchinja.” Msimuliaji alisimulia sehemu ya Hadiyth iliyosalia. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

638.

وَعَنْ سَرَّاءَ بِنْتِ نَبْهَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {خَطَبَنَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يَوْمَ اَلرُّءُوسِ فَقَالَ: " أَلَيْسَ هَذَا أَوْسَطَ أَيَّامِ اَلتَّشْرِيقِ ؟ "} اَلْحَدِيثَ رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ

Kutoka kwa Sarraa bint Nabhaan[55] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitupa mawaidha baada ya siku ya kuchinja[56] akasema: “Hii si siku ya katikati ya Siku za Tashriyq?” Msimulizi ameipokea sehemu ya Hadiyth iliyobakia [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad nzuri]

 

 

 

639.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ لَهَا: {طَوَافُكِ بِالْبَيْتِ وَبَيْنَ اَلصَّفَا وَاَلْمَرْوَةِ يَكْفِيكَ لِحَجِّكِ وَعُمْرَتِكِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia: “Kuizunguka Nyumba (kutufu) na kukimbia kati ya Asw-Swafaa na Al-Marwaa kunatosheleza kwa Hijjah na ‘Umrah yako.”[57] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

640.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ‏{لَمْ يَرْمُلْ فِي اَلسَّبْعِ اَلَّذِي أَفَاضَ فِيهِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ.

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Hakukimbia katika kuzunguka Nyumba mara saba[58] aliporudi Makkah.” [Imetolewa na Al-Khamsah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

641.

وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه {أَنَّ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم ‏صَلَّى اَلظُّهْرَ وَالْعَصْرَ وَالْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ، ثُمَّ رَقَدَ رَقْدَةً بِالْمُحَصَّبِ، ثُمَّ رَكِبَ إِلَى اَلْبَيْتِ فَطَافَ بِهِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Adhuhuri na Alasiri, Maghribi na ‘Ishaa, kisha akalala Al-Muhasw-swab.[59] Kisha akapanda ngamia wake hadi kwenye Al-Ka’bah na akafanya Twawaaf.”[60] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

642.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا: {أَنَّهَا لَمْ تَكُنْ تَفْعَلُ ذَلِكَ ‏أَيْ: اَلنُّزُولَ بِالْأَبْطَحِ‏ وَتَقُولُ: إِنَّمَا نَزَلَهُ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏لِأَنَّهُ كَانَ مَنْزِلاً أَسْمَحَ لِخُرُوجِهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Alikuwa hafanyi hivyo, yaani kushuka Al-Abtwah, amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alishukia pale kwa sababu palikuwa ni mahala rahisi zaidi kuondokea yeye.”[61] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

643.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {أُمِرَ اَلنَّاسُ أَنْ يَكُونَ آخِرَ عَهْدِهِمْ بِالْبَيْتِ، إِلَّا أَنَّهُ خَفَّفَ عَنِ الْحَائِضِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Watu waliamrishwa wasiondoke bila kupita katika Nyumba (Al-Ka’bah) ili kutufu Twawaaf Al-Wadaa’i, isipokuwa imesamehewa kwa mwenye hedhi.”[62] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

644.

وَعَنِ اِبْنِ اَلزُّبَيْرِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{صَلَاةٌ فِي مَسْجِدِي هَذَا أَفْضَلُ مِنْ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ إِلَّا اَلْمَسْجِدَ اَلْحَرَامَ ، وَصَلَاةٌ فِي اَلْمَسْجِدِ اَلْحَرَامِ أَفْضَلُ مِنْ صَلَاةٍ فِي مَسْجِدِي بِمِائَةِ صَلَاةٍ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Ibn Az-Zubayr[63] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah moja katika Msikiti wangu huu ni bora zaidi mara elfu kuliko Swalaah ya popote pengine isipokuwa Swalaah ya Al-Masjid Al-Haraam (Msikiti Mtukufu wa Makkah). Na Swalaah moja katika Msikiti Mtukufu wa Makkah ni bora zaidi kuliko Swalaah katika Msikiti wangu huu kwa Swalaah mia moja.”[64] [Imetolewa na Ahmad, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

[1] Al-Qasw-waa ni jina la ngamia jike wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

[2] Al-Baydaa maana yake ni msitu au tambarare, na pia kulikuwa na kijiji kilichoitwa Baydaa. Kama ilivyotajwa hapo nyuma, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alianza kusoma Talbiyah tokea Msikitini. Hii hapa inasema alianza kusoma kule Baydaa. Ukweli ni kwamba usemi wa kwanza ndio sahihi. Kwa kuwa msimuliaji alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisoma Talbiyah kule Baydaa, alidhani kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alianza kuisoma Talbiyah pale Baydaa, ambapo ukweli ni huo kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikwishaanza kuisoma tokea kabla hata ya kufika Baydaa.

[3] Nyumba hapa ina maana ya “Ka’bah”

[4] Katika lugha ya kiarabu, Rukn maana yake ni Al-Hajar Al-Aswad (Jiwe Jeusi), na Istalaam maana yake ni kulibusu au kuligusa.

[5] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofika Makkah pamoja na Maswahaba wake kutekeleza “Umratul-Qada”, Maqurayshi wakaanza kuwashutumu Waislamu kuwa wamekonda na wamedhoofu kuwa vile aina fulani ya homa iliwakumba walipokuwa Al-Madiynah. Baada ya kusikia shutuma hizi, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaamrisha Maswahaba wake watembee vifua mbele wakiwa wamejaa heshima na majivuno, kama wanavyofanya wapiganaji mieleka, kuwaonyesha Maqurayshi kuwa wao siyo dhaifu. Tokea siku ile mpaka leo hii, hilo tendo la kutembea kwa namna hii katika mizunguko mitatu ya kwanza ya Twawaaf (Kuizunguka Ka’bah) limekuwa tendo la Sunnah.

[6] Yawm At-Tarwiyah ni siku ya nane ya mwezi wa Dhul-Hijjah.

[7] Maana au tafsiri ya neno la Kiarabu “Minaa” ni “kukata au kuangusha”. Kwa sababu mahala pale ndipo zilipokuwa zikimwagwa damu za wanyama wa kafara, paliitwa “Minaa”.

[8] Namirah ni jina la mahala karibu na ‘Arafah, penye Msikiti wenye jina hilo.

[9] Kwa kiarabu, Asw-Swakharah maana yake ni “Mawe”.  

[10] Hadiyth hii inaashiria wazi kuwa, kila Swalaah mbili zinaposwaliwa pamoja (kisafari), huhitajika Adhana moja tu, lakini itahitaji kutamka Iqaama mbili tofauti tofauti, moja kwa kila Swalaah moja.

[11] Hadiyth hii pia inatufahamisha kuwa, kila Swalaah mbili zinaposwaliwa moja baada ya nyingine, hairuhusiwi kuswali Swalaah zozote za Sunnah kati yazo.

[12] Al-Mash’aral-Haraam ni eneo la wazi kati ya vilima viwili vya Muzdalifah.

[13] Bonde la Muhassir liko kati ya Al-Muzdalifah na Minaa

[14] Mahujaji huagizwa walivuke lile bonde kwa kasi na mapema sana, bila kujali amepanda kipando au anatembea kwa miguu. Kuna sababu mbili za hili: (a) Wale watu wa tembo waliteketezwa kwa nguvu za Ilaah mahali hapa, kwa hivyo mtu sharti apite pahala hapo kwa haraka na huku akilia machozi. (b) Wakati walipokuwa wakifanya Hijjah, wale washirikina waliokuwa wakiabudu asiyekuwa Allaah, wengi walikuwa wakikaa hapa, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitaka kutofautiana nao kwa hilo.

[15] Jamrah maana yake ni “Rundo la mawe”. Yapo majamrah matatu, na ni lazima yote yatupiwe vijiwe. Jamrah lililotajwa hapa ni Jamratul-‘Aqabah.  

[16] Khuzaymah bin Thaabit ndiye Ibn Al-Fakiha Al-Khatami Al-Answaariy Al-Aws. Alipewa jina la utani la Abuu ‘Imrata. Alishuhudia Badri na vita vingine vilivyofuata. Ndiye aliyeshika bendera ya Khatama wakati wa kutekwa Makkah, na alishiriki katika vita vya Siffiyn pamoja na ‘Aliy na akauliwa huko.

[17] Hii ina maana mbili: (a) Ya kwanza ni kwamba, baada ya kutamka Labbayk kila mara, sharti mtu umuombe Allaah (سبحانه وتعالى)  ridhaa Yake,  na kuomba Jannah na Rahma Zake, (b) Pili, mtu sharti amuombe Allaah (سبحانه وتعالى)  mwisho wa Talbiyah ambao huishia katika kutupa vijiwe vya Jamratul-‘Aqabah.

[18] Jam’ ni jina jingine la Al-Muzdalifah. Uwanja wote wa ‘Arafah ni pahala pa kukaa. Kuanzia adhuhuri ya tarehe 9 ya mwezi Dhul-Hijjah (Mfungo tatu) mpaka alfajiri ya tarehe 10 ya Dhul-Hijjah, ni lazima kila Haaji akae kwa muda fulani pale ‘Arafah. Haaji atakayeukosa huu msingi mkuu mmojawapo wa Hijjah, atakuwa kaikosa Hijjah yote. Kwa maneno mengine, hakuna Hijjah ya bila kukaa ‘Arafah.

[19] Jina la sehemu ya juu ya Makkah ni Ath-Thaaniyatul-Ulyaa, na jina la sehemu ya chini ni Ath-Thaaniyatus-Suflaa.

[20] Dhiy Twuwaa ni pahala ambapo pako ndani ya mipaka ya ukanda mtukufu na iko karibu na jiji la Makkah.

[21] Kusujudu mbele ya Hajar Al-Aswad (Jiwe Jeusi) haimaanishi kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alilisujudia Al-Hajar Al-Aswad lenyewe. Inaweza kuwa na maana mbili: (a) Ya kwanza ni kuwa alilibusu Al-Hajar Al-Aswad na akagusa paji la uso wake juu yake pia, ambayo hiyo inaashiria kuwa alikuwa akilibusu kikamilifu. (b) Ya pili, baada ya kukamilisha Twawaaf (kutufu au kuzunguka Ka’bah), Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa mbili za Swalaah ya Nafl (Sunnah) mbele ya Al-Hajar Al-Aswad.

[22] Neno linalotumika kwa lugha ya Kiarabu ni “Ashwaatw” ambao ni uwingi wa “Shawtw” na Shawtw moja ni mzunguko mmoja kamili kutufu Ka’bah.

[23] Kutembea mizunguko mine kuitufu Ka’bah

[24] Kona mbili ni Rukn Al-Yaman na Rukn Al-Hajar Al-Aswad

[25] ‘Umar amesema hivyo kwa sababu Waarabu ndiyo kwanza walikuwa wameachana na kuabudu masanamu wengi, na katika zama za Jahiliya (kabla ya Uislam) waliamini kuwa masanamu (ambayo yaliundwa kwa mawe) yalikuwa na nguvu na uwezo wa kuwapa faida wanaadamu. Kwa hivyo ‘Umar amesema vile ili kupinga dhana ile ya kuzaliwa nayo ya Waarabu ili wasipotoke.

[26] Abuu Atw-Twufayl ndiye ‘Aamir bin Wathila Al-Layth Al-Kinaan. Aliishi miaka minane ya mwisho ya uhai wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alifia Makkah mnamo mwaka wa 100 A.H. au 102 au mwaka wa 110 A.H., na alikuwa Swahaba wa mwisho kufariki dunia.  

[27] Hii ni fimbo ya kutembelea yenye mshikio uliopinda.

[28] Hadiyth hii inatufahamisa kuwa endapo mtu anashindwa kulifikia Al-Hajar Al-Aswad (Jiwe Jeusi) kwa sababu ya watu wanaolizunguka ni wengi mno, basi inaruhusiwa kuligusa jiwe lile kwa fimbo kisha akaibusu hiyo fimbo. Lakini kwa zama hizi hata hivo haiwezekani kutokana na zahma kubwa mno. Hivyo inatosheleza mtu anapofikia mstari wa Al-Hajar Al-Aswad aashirie tu mkono wake akiwa mbali na kusema: Allaahu Akbar bila ya kubusu mkono, kwani kubusu mkono kila unapofikia hapo ni bid’ah.

[29] Ya’laa bin Umayyah ndiye Abuu Safwaan At-Tamimi Al-Makki, rafiki wa Maqurayshi na Swahaba aliyesilimu wakati wa kutekwa Makkah. Alishuhudia vita vya Hunayn, Twaaif na Tabuwk; na alimtumikia Abuu Bakar na ‘Umar, na ‘Uthmaan. Aliishi hadi kufikia miaka ya hamsini ya Al-Hijrah.

[30] Hadiyth hii inadhihirisha desturi ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuvaa shuka. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichukua shuka kutoka chini ya kwapa yake ya kuume na akaiweka juu ya bega lake la kushoto. Alifanya hivyo ili kuonyesha afya yake nzuri na nguvu zake. Tendo hilo linafanana na lile tendo la kukimbia wakati akitufu kuzunguka Ka’bah. Haya hayakutakikana baada ya ushindi wa Uislam; lakini tendo la Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) likawa Sunnah milele.

[31] Mtu huruhusiwa kutamka Takbiyra, lakini ni bora kutamka Talbiyah.

[32] Kisheria, Haaji sharti akeshe usiku mzima pale Muzdalifah: Akae Al-Mash’aral-Haraam baada ya kuswali Swalaah ya Alfajiri, kisha ndipo aendelee kutokea pale. Lakini imeruhusiwa kwa watu dhaifu, wazee, wagonjwa na wanawake kuondoka kutoka Muzdalifah baada ya kukaa pale Muzdalifah kwa sehemu kubwa ya usiku, ili wapate kuwahi kufika Minaa na wakamilishe kitendo kingine cha lazima cha kutupa vijiwe, kabla watu wote hawajafika kule kwani kunajaa watu wengi mno.

[33] Sawdah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) ni Ummul-Mu-uminiyn (Mama wa Waumini) ndiye Sawdah bint Zam’a bin ‘Abd-Shams Al-Qurayshiyyah Al-Aamiriya. Alisilimu kule Makkah mapema na kuhamia Uhabeshi na mume wake alifia kule. Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuoa huko Makkah, baada ya kifo cha Khadija na kabla ya kumchumbia ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا). Alifariki mwaka 55 A.H.

[34] Kwa ujumla, watu hawaruhusiwi kutupa vijiwe kule Jamaraat kabla ya jua kuchomoza, lakini watu wenye vilema wanaruhusiwa kutupa.

[35] Hii ni Twawaaf Al-Ifaadhwah.

[36] Ni ‘Urwah bun Mudhwarris bin Aws bin Haarith bin Lam Atta’I aliyekuwa Swahaba aliyeshuhudia Hijjatul-Wadaa na alilowea Kufa. Ndiye ameipokea Hadiyth hii.

[37] Sehemu muhimu ya Hijjah ambayo ndiyo kule kusimama pale ‘Arafah.

[38] Neno Tafathah maana yake ni taka au uchafu. Hapa neno hilo lina maana hiyo hiyo, kwani watu huenda kunyoa nywele na kuoga taka zote baada ya kukamilisha Hijjah. Huko kujitakasa kunaashiria mwisho wa Hijjah, kila anayetekeleza taratibu zote hizi, Hijjah yake inakuwa imetimilika.

[39] Thabiyr ni moja ya milima mirefu sana Makkah ulioko upande wa kushoto wa barabara iendayo Minaa.

[40] Hilo tendo la kurejea kutoka Muzdalifah kabla ya jua kuchomoza huhesabika kuwa ni Mashruw’ (ni haki kishariy’ah).

[41] Usaamah bin Zayd ndiye Abuu Muhammad au Abuu Zayd Usaamah bin Zayd bin Haarith bin Sharaahil Al-Kalbiy, aliyekuwa kipenzi cha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), mtumwa wake aliyemuacha huru na pia ni mtoto wa mtumwa wake aliyemuacha huru. Mama yake alikuwa ni Umm Ayman aliyemlea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Siku chache kabla hajafa, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimteua aongoze jeshi walimokuwemo Abuu Bakar na ‘Umar, wakati akiwa na umri wa miaka 18 tu. Hata hivyo jeshi lile halikuwahi kupelekwa kwa sababu ya kifo cha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na baadae Abuu Bakr alilipeleka. Usaamah alikufa baada ya kifo cha ‘Uthmaan, mwaka wa 54 H.

[42] Haaji sharti atamke Talbiyah hadi akishatupa vijiwe vya kwanza katika Jamratul-‘Aqabah. Kule kutupa vijiwe vya kwanza ndiko kunaashiria mwisho wa Talbiyah, kwa mujibu wa maoni ya Wanazuoni wengi.

[43] Jamratal-‘Aqabah ndiyo mahala pakubwa pale Minaa ambapo mahujaji hutupa vijiwe kwanza siku ya kuchinja, tarehe 10 ya mwezi wa Dhul-Hijjah.

[44] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitaja Aayah katika Suwratul-Baqarah kwa sababu Aayah zake nyingi zinatoa maamrisho na makatazo kuhusu Hajj.

[45] Haaji ni sharti akamilishe kutupa vijiwe kabla ya kupinduka jua katika siku ya ‘Iyd, ajizuie kutupa vijiwe saa sita mchana. Baada ya jua kupinduka, Ibaada hii inaweza kutekelezwa.

[46] Neno la kiarabu la Ad-Dunyaa linaweza kutafsiriwa kuwa ni “karibu”. Kwa kuwa hio iko karibu na Msikiti wa Khaaif inaitwa Jamratad-dunyaa, lakini pia inaitwa Jamratul-Uwlaa.

[47] Hapa neno la kiarabu Sahl linatumika kwa kipande cha ardhi laini. Hii ina maana kuwa, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akitaka kutupa vijiwe katika Jamaraat, hakusimama pale bali alijitokeza nje waziwazi, akasimama pale na kisha akaomba du’aa kwa Allaah (عزّ وجلّ).

[48] Ni muhimu kukata nywele baada ya kutekeleza Hijjah au ‘Umrah. Kunyoa nywele zote na hata kupunguza zenyewe kunaruhusiwa. Hata mtu ambaye hana nywele kichwani anatakiwa apitishe kijembe kichwa kizima.

[49] Wanaohiji wana mambo manne muhimu katika siku ya ‘Iyd: (a) Kurusha vijiwe katika Jamrah (Al-‘Aqabah) (b) Kuchinja mnyama, (c) Kunyoa nywele za kichwa, (d) Kutufu Ka’bah.  Mpangilio wa kuvitekeleza vitendo hivi vinne ni kama ulivyoonyeshwa hapa, kwa mujibu wa Shariy’ah za Kiislam. Kutimiza mpangilio huu ni Sunnah. Hakuna madhara ikiwa mpangilio huu hautozingatiwa kwa sababu ya kutojua. Lakini iwapo mtu anafanya hivyo kwa makusudi, itakuwa dhambi ingawa haina adhabu.

[50] Al-Miswar bin Makhramah ni Mzuhri na Mquraysh. Alikuwa miongoni mwa watu waadilifu sana. Alihamia Makkah baada ya kuuliwa kwa ‘Uthmaan. Alipigwa kwa silaha akafa wakati akiswali wakati Yaziyd bin Mu’aawiyah aliizingira Makkah mnamo mwaka wa 64 A.H.

[51] Hii inaweka wazi kuwa, baada ya kutupa vijiwe katika Jamrah Al-‘Aqabah na kunyoa nywele za kichwa, inahusiana kila kitu isipokuwa kujamiiana. Hiyo huruhusiwa baada ya Twawaaf Al-Ifaadhwah tu.

[52] Hii inatufahamisha kuwa wanawake hawana haja ya kunyoa nywele zote, bali lazima wapunguze kidogo nywele zao za chini.

[53] Ni Waajib (lazima) kwa Hujaji kuwapo Minaa usiku ule. Endapo Haaji hawezi kuwepo Minaa usiku mzima, basi awepo angalau kwa sehemu kubwa ya usiku.

[54] ‘Aaswim bin ‘Adiyy ndiye mwenye jina la utani la Abuu ‘Ubaydillaah au Abuu ‘Amr, na alikuwa rafiki wa Banu ‘Amr bin ‘Awf wa Answaar. Alishuhudia vita vya Badri na vita vilivyofuata. Alikuwa ndiye kamanda wa makabila ya Al-‘Aaliyah wakati wa vita vya Badr, kwa hivyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa sehemu moja ya ngawira. Alikufa mnamo mwaka wa 45 A.H. Pia inasemekana alikufa shahidi katika vita vya Al-Yamaamah akiwa katika umri wa miaka 120.

[55] Huyu ndiye Sarraa bint Nabhaan Al-Ghanawiyyah, ambaye ni Swahaba, naye Rabiy’a bin Abiy ‘Abdir-Rahmaan ameipokea Hadiyth hii kutoka kwake.

[56] Hii ni Yawm Ar-Ru-uws (siku ya Vichwa) ni jina la siku ifuatiayo siku ya ‘Iyd

[57] Hadiyth hii inatuarifu, kuifanya Twawaaf moja na Sa’y moja kunatosha kwa  zote mbili yaani ‘Umrah na Hijjah kwa Haaji anayefanya Hijjah ya Qiraan. Kinyume cha hivi kwa Haaji anayefanya Hijja Tamattu’ ni sharti afanye Twawaaf mbili na Sa’y mbili kila moja mbalimbali.

[58] Kwa hivyo tunafahamishwa kwamba hakuna Ramal (kukimbia) katika Twawaaf Al-Ifaadhwah wala Twawaaf Al-Wadaa’i. Ramal hufanywa katika Twawaaf Al-Quduwm tu. Na Twawaaf Al-Quduwm ni ile ambayo hufanywa mara baada ya kuingia Makkah mara ya kwanza. Sharti kuzingatia pia kuwa Ramal (kukimbia) hufanywa na wanaume tu. Endapo Haaji ameshindwa kuifanya katika Twawaaf Al-Quduwm ni sharti aifanye wakati anaifanya Twawaaf Al-Ifaadhwah.

[59] Al-Muhasw-swab ni eneo la wazi kati ya milima miwili iliyo jirani zaidi na Minaa kuliko Makkah. Pia huitwa Abtah, Batha na Khaif Banuw Kinaanah.

[60] Hii ni Twawaaf Al-Wadaa’i (ya kuaga) inayofanywa wakati wa kuondoka Makkah.

[61] Pa kuondokea kuenda Al-Madiynah

[62] Hii ni Twawaaf Al-Wadaa’i (Kuiaga Ka’bah kwa kutufu mara ya mwisho), ambayo ni Waajib (ni lazima) kwa Hujaji kwa mujibu wa Maimaam isipokuwa Imaam Maalik. Hivyo wanawake wenye hedhi wanasamehewa. Mtu yeyote anayeikosa hiyo huwajibika kufanya kafara ya mnyama.

[63] Ibn Az-Zubayr ndiye Abuu Bakr ‘Abdillaah bin Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam Al-Qurayshiy Al-Asad. Mama yake Asmaa bint Abiy Bakr alihamia Al-Madiynah wakati yu mjamzito na akamzaa kule Qubaa, kwa hivyo akawa mtoto wa kwanza kuzaliwa baada ya Hijrah. Alikuwa akifunga Swawm na kuswali sana. Alikuwa mtu mheshimiwa ambaye hakukubali kudhulumiwa, na alikuwa mpiganaji mkali. Alikuwa mbuji, na alikuwa anakubali haki, na alikuwa hodari wa kuwaangalia warithi wake. Aliapishwa kupokea Ukhalifa baada ya kufa Yaziyd bin Mu’aawiyah mnamo mwaka wa 64 A.H. Kwa hivyo aliziteka Al-Hijaaz, ‘Iraaq zile mbili, Yaman, Misri na sehemu kubwa ya Shaam. Al-Hajjaaj bin Yuwsuf Ath-Thaqafi alimzingira Makkah, na alikufa shahidi na kusulubiwa mnamo mwezi wa Jumaada Al-Ukhraa mnamo mwaka wa 73 A.H.

[64] Imeripotiwa katika Twabaraan kuwa, Swalaah inayoswaliwa katika Msikiti wa Al-Aqswaa (Baytul-Maqdis) huzawadiwa mara 500 (mia tano), na Swalaah inayoswaliwa katika Msikiti wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) (Al-Madiynah) hulipwa mara 1,000 (elfu moja), ambapo Swalaah inayoswaliwa katika Masjid Al-Haraam (Nyumba ya Allaah pale Makkah) hulipwa mara 100,000 (elfu mia moja).

 

 

Share