06-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuomba Du'aa Ndefu Anapoanza Twawaaf Katika Mstari Wa Hajar Al-Aswad

 

Kuomba Du'aa Ndefu Anapoanza Twawaaf Katika Mstari Wa Hajar Al-Aswad

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Baadhi ya Hujaji wanapofikia mstari ambao ni alama ya kuanzia twawaaf (iliyoko sambamba na Hajar al-Aswad), husimama kwa muda mrefu kuomba du'aa wakiwazuia wenzao wasiendelee kufanya twawaaf zao. Nini hukmu ya kufanya hivyo?

 

JIBU:

 

Haifai kusimama muda mrefu katika mstari huo na kuomba du'aa. Inavyopasa ni kuelekea Hajar al-Aswad na kuliashiria kwa mkono wa kulia na kusema: “Allaahu Akbar”, kisha aanze kufanya twawaaf.

 

Wengine pia husimama na kutia niyyah kwa kutamka kwa sauti kusema "Natia niyyah kufanya twawaaf (mizunguko) saba za 'Umrah kwa ajili ya Allaah." Kutamka niyyah katika vitendo vya ‘ibaadah ni bid’ah kwani haikuthibitika kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala Maswahaba. Hivyo niyyah huwekwa moyoni na Allaah Anajua niyyah za waja Wake. (Na hivi ndivyo ilivyokuja katika mafunzo ya Sunnah).

 

 

[Daliyl al-Akhtwaa Yaqa'a fiyhaa al-Haaj wal-Mu’tamir wat-Tahdhiyr minhaa – Uk. 42].

 

Share