07-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuomba Du'aa Ndefu Nyuma Ya Maqaam Ibraahiym
Kuomba Du'aa Ndefu Nyuma Ya Maqaam Ibraahiym
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kusoma du'aa ndefu nyuma ya Maqaam Ibraahiym?
JIBU:
Miongoni mwa bid’ah zinazofanywa na baadhi ya Hujaji wanaposimama nyuma ya Maqaam Ibraahiym ni kwamba wanasoma du'aa ndefu wanayoiita du'aal-Maqaam (du’aa ya kisimamo).
Hakuna dalili hiyo katika Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hii ni bid’ah iliyokatazwa na kila bid’ah humpotosha Muislamu.
Baadhi ya watu hukusanyika katika vikundi wanasoma vijitabu vya du'aa kwa sauti, akiwa mmojawao anaongoza na nyuma yake wanaitikia kwa mkarara na kusema 'Aamiyn'. Yote hayo ni bid’ah na husababisha madhara ya tashwishi kwa Hujaji wanaoswali Maqaam Ibraahiym, nalo ni jambo ovu.
[Al-Bid'u wal-Muhadathaat wa maa laa aswala lahu – Uk. 399; Fiqh al-'Ibadaat – Uk 356]