10-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kutamka Talbiyah Pamoja Kwa Kukariri

 

Kutamka Talbiyah Pamoja Kwa Kukariri

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kutamka talbiyah katika kikundi kwa mkarara?

 

JIBU:

 

Baadhi ya Hujaji wanatamka talbiyah pamoja kwa mkarara, aidha mmoja wao akiwa mbele yao, au katikati au nyuma yao akitamka na wengine wakikariri. Hii haikuthibitika kutoka kwa Swahaba yeyote, bali Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema:

 

"Tulikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika ‘Hijjatul-Widaa’ (Hajj Ya Kuaga) na miongoni mwetu kuna waliokuwa wakisema: “Allaahu Akbar” na wengine wakisema: “Laa Ilaah Illa Allaah” na wengine wakitamka talbiyah."

 

Hivyo ndivyo inavyopasa kuwa kila mmoja atamke talbiyah pekee  na sio kwa pamoja.

 

[Al-Bid’ah wa-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk 394 Fiqh al-Ibadaat Uk 343]

 

 

Share