01-Imaam Al-Albaaniy: Kutumia Dawa Kuzuia Hedhi Wakati Wa Hajj Au 'Umrah

 

 

Kutumia Dawa Kuzuia Hedhi Wakati Wa Hajj Au 'Umrah

 

 Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, inaruhusiwa mwanamke kutumia dawa za kuzuia kumfikia hedhi yake ili aweze kutekeleza taratibu za Hajj au 'Umrah kwa wepesi?

 

JIBU:

 

Sioni madhara yoyote kwa mwanamke kuchukua matibabu ya dawa kwa sharti iwe daktari wake amemruhusu kwa kuona kwamba haitomsababisha madhara yoyote kutumia dawa hizo za kuzuia hedhi. Kwa hiyo sharti ya asasi katika mas-ala haya ni kuruhusiwa na maadam jambo hili haliingii katika dhambi.

 

[Fataawa Muhimmah lin-Nisaai al-Ummah]

 

Share