02-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Mwanamke Mwenye Hedhi Anataka Kukaa Katika Eneo La Swafaa na Marwah
Mwanamke Mwenye Hedhi Anataka Kukaa Katika Eneo La Swafaa na Marwah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, anaruhusiwa mwanamke mwenye hedhi kukaa katika eneo la mas-'aa (eneo la Swafaa na Marwah)?
JIBU:
Ndio anaruhusiwa mwanamke mwenye hedhi kukaa eneo la mas-'aa kwa sababu mas-'aa haihesabiki kuwa ni sehemu ya Masjidul-Haraam. Kwa hiyo ikiwa hedhi itamuanza mwanamke akiwa ameshamaliza kufanya twawaaf na kabla ya kufanya sa'y, basi anaruhusiwa kufanya sa'y kwa sababu sa'y sio twawaaf, na kuwa katika hali ya twahara sio sharti. Kutokana na hivyo, tunasema kwamba ikiwa mwanamke mwenye hedhi amekaa katika eneo la mas-'aa anamsubiri mumewe basi hakuna madhara kufanya hivyo.
[Fataawa al-Haj wal-'Umrah waz-Ziyaarah]