07-Fatwa: Wanawake Kuvaa Nguo Za Aina Nyingine Katika Ihraam

 

Wanawake Kuvaa Nguo Za Aina Nyingine Katika Ihraam

 

 www.alhidaaya.com

 

   

SWALI:

 

Je, mwanamke anaruhusiwa kuingia katika ihraam kwa kuvaa nguo yoyote apendayo?

 

JIBU:

 

Ndio, anaweza kuingia katika ihraam akavaa nguo yoyote apendayo. Hana haja kuvaa nguo hasa kwa ajili ya ihraam  kama wanavyofanya baadhi yao na kudhania kuwa inapasa kuvaa nguo maalum. Lakini inampasa kuvaa nguo ambayo haivutii (isiyokuwa ina rangi nyingi za kupendeza au mapambo). Hii kwa sababu atachanganyika na wanaume kwa hiyo nguo zake zisiwe za kumvutia mtazamaji. Isiwe nzuri ya kupendeza lakini iwe ya kawaida na sio ya kuleta matamanio.

 

 

[Fataawa Al-Mar-ah]

 

Share