Shaykh Fawzaan: Yanayomfaa Maiti Kufanyiwa Na Yanayompatia Thawabu
Yanayomfaa Maiti Kufanyiwa Na Yanayompatia Thawabu
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Vitendo gani ambavyo vinamfaa maiti kufanyiwa na walio hai? Je kuna tofauti baina ya vitendo vya kimwili na ibada za zisizo za kimwili Tunatumai mtafafanua mas-ala haya kwetu na kutuelezea hukmu ambayo tutaweza kuitegemea tutakapokumbana na mas-ala kama haya. Tafadhali tupeni fatwa na Allah Akubarikini (katika mambo yenu)
JIBU:
Maiti anaweza kunufaika kwa vitendo vya walio hai ambavyo vinatokana na dalili sahihi inayodhihirisha kuruhusiwa kama; kumuombea du'aa, kumuombea maghfirah, kumfanyia Sadaqah, kumfanyia Hajj na 'Umrah, kumlipia madeni yake na kumtekelezea Mirathi yake ya Kiislam.
Vitendo vyote hivyo vimo katika hukmu ya shariy’ah, Na baadhi ya ‘Ulamaa wameunganisha na hayo pia vitendo vyote vengine vya ‘ibaadah ambavyo Muislamu hutenda kwa ajili ya Muislamu mwingine ambaye yu hai au amefariki. Lakini, iliyo sahihi ni kujiweka katika mipaka ya yale yaliyoruhusiwa yakiwa na dalili sahihi, kwani hivyo itakuwa ni kutokana na maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaposema:
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾
Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi. [An-Najm: 39]
Na Allaah Anajua zaidi
[Al-Muntaqaa min Fataawa Shaykh Swaalih Al-Fawzaan – Mjalada 2, Uk. 161, Fatwa Namba 139]