Shaykh Fawzaan: Tofauti Kati Ya Manhaj Na ‘Aqiydah
Tofauti Kati Ya Manhaj Na ‘Aqiydah
Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, kuna tofauti baina ya ‘Aqiydah Na Manhaj?
JIBU:
Manhaj ina maana pana zaidi kuliko ‘Aqiydah.
Manhaj inapatikana katika ‘Aqiydah na katika maadili na tabia na muamala; na katika maisha yote ya Muislamu.
Ama ‘Aqiydah hii inatokana na asili (msingi) wa Iymaan pamoja na maana ya Shahada mbili na yanayohusiana nayo. Hii ndio ‘Aqiydah.
[Al-Ajwibah Al-Mufiydah, uk. 75]