Shaykh Fawzaan: Mashia Si Ndugu Zetu; Mashia Ni Ndugu Wa Shaytwaan
Mashia Si Ndugu Zetu, Mashia Ni Ndugu Wa Shaytwaan
Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Huyu (muulizaji) anasema baadhi ya Walinganiaji na Wanafunzi wanasema wanapozungumza kuhusu Mashia kuwa ni ndugu zetu; je, inajuzu kusema hivyo, na nini linalopasa kuhusiana na hilo?
JIBU:
Tunajiweka mbali nao kwa ajili ya Allaah, na tunajiweka mbali kwa Allaah kwa kauli kama hiyo; hao si ndugu zetu, Wa-Allaahi si ndugu zetu. Bali wao ni ndugu wa Shaytwaan.
Hakika wao wanamtukana Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) mke wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye Allaah kamchagua (kuwa ni mke) kwa Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ni Asw-Swiddiyqah bint Asw-Swiddiyq. Kadhaalika (hao Mashia) wanawakufurisha Abuu Bakr na ‘Umar na wanawalaani. Vilevile wanawakufurisha Maswahaba kwa ujumla, isipokuwa Ahlul-Bayt ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu), pamoja na kwamba (kiuhalisia) wao ni maadui wa ‘Aliy bin Abiy Twaalib. ‘Aliy anajiweka mbali na wao, ‘Aliy (Radhwiya anajitenga nao Allaahu ‘anhu), yuko mbali na wao. ‘Aliy ni Imaam wetu na si Imaam wao; si Imaam wa Raafidhwah (Mashia) Makhabiyth (waovu, wachafu).
Nasi tunajitenga mbali na wao kwa ajili ya Allaah. Si ndugu zetu, na anayesema hao ni ndugu zetu, basi atubu kwa Allaah na amtake Allaah maghfirah. Allaah (Jalla wa ‘Alaa) Ametuwajibisha tujitenge na kujiweka mbali na watu wapotevu na (Ametuwajibisha) tufanye ukaribu na watu wa Iymaan.
[Sauti: https://archive.org/details/Abusulaym_20131126]